Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Jugado

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2021
Posts
1,446
Reaction score
3,184
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote.

Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650.

Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

NB: Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
 
Haya mambo ya hela za mtandao mimi huwa nayaheshimu sana,hujui hiyo hela aliyetuma huko alikokusudia kutuma ilikuwa ikafanye kazi gani?je mgonjwa yupo mahututi?msiba au ada?

Mwaka 2003 kipindi hiko hakuna pesa za kwenye simu jamaa yangu mama yake alikuwa na historia ya maradhi ya mara kwa mara na ya ghafla so yeye ndiyo mkubwa akawa yupo town anatafuta maisha ndugu zake wapo Arusha,alikuwa mlinzi muajiriwa wa wanaokumbuka kampuni ya GOHA SECURITY hawa walikuwa Magomeni Mapipa,siku moja ikapigwa simu nipo nae ilikuwa jioni ya 16:00 mama ameumwa tena na inatakiwa haraka hela kwa ajili ya dawa na huduma nyinginezo.

Jamaa alikuwa na akiba yake Tsh 50,000/= so ikabidi anunue voucher za Voda kisha nduguze kule kijijini wa-make deal na muuza vocha na mpigisha simu wa kijiji vocha itumwe kwake awe anaiuza kwa kurusha then akate itakayomtosha baki wapewe wakamuhudumie mama yao,jamaa akakosea namba moja mtu yupo Kigoma aloo ilikuwa balaa.

To cut a long story jamaa alikataa kurudisha hela (zile vocha) huku ndugu wa jamaa wanapiga simu hali ya mama imezidi kuwa mbaya anakufa hospital wamekataa kumuhudumia ikabidi apige tena simu Kigoma kwa jamaa huku analia kama mtoto akimuomba arudishe japo kidogo maana hela ilikuwa ni kwa ajili ya matibabu ndiyo kidogo jamaa akawa na huruma akarudisha japo sikumbuki kama alirudisha hata 40K,hii ilituumiza hata sisi tuliokua nae kwa ile hali jamaa alikuwa anapitia na toka siku ile nilijifunza mengi sana hasa kuheshimu hisia za watu nisiowaona.

So kwa yeyote atakaesoma hapa ajue anaweza akawa sababu ya kifo cha mtu tujifunze kutokula visivyotuhusu.(nimekazia sana kwenye suala la kifo kwa sababu ndiyo sehemu pekee isiyokuwa na option ya subira)
 
Nilikoseaga kutuma laki 8,bahati alipokea mstaafu wa jeshi la magereza ni mtu mzito sana ,keaho yake alinipa yoote pale kibo complex,emagin alitoka gongolamboto kwaajili yangu
Uaminifu ni kitu muhimu sana kwenye maisha, wazungu wanaita "honesty"tatizo Ngozi nyeusi wengi wamekosa kitu hicho kutokana na malezi.
 
Back
Top Bottom