2020 nilikosea kumtumia mtu 206,000. Ilikuwa ni malipo ya hela ya Chakula ya vibarua kwenye site yangu.
Nilikuwa busy kidogo, ilipofika tu jamaa niliyempigiaa simu akapiga. Nikamuandikia ujumbe kuwa tayari nimeshatuma. Niliamini ni fundi anauliza. Jamaa, akaniandikia pokea mara moja.
Akapiga lakini niligundua si sauti ya fundi. Akaniambia kuna fedha nimemtumia ila anaomba asirudishe. Nilipanick kidogo, jamaa akanielezea story ya magumu anayopitia. Anaomba sana nimuachie kiasi kile cha hela. Akaniambia kama sitaridhia atarudisha kiasi hicho punde baada ya kukata simu.
Lakini kwa magumu yale, niliridhia kumuachia kiasi hicho cha pesa. Ukweli ni kuwa niliokoa maisha ya mwanae. Na maombi yake yalijibiwa kupitia mimi. Nilifanya alternative nyingine kuwesesha kule site.
Jioni nilipata dili zuri mno. Nikajua tu ni Mungu ananilipa kwa Sadaka yangu ya asubuhi.