Kuna jamaa niliwahi kumtumia hela ya Michango ya msiba kimakosa,jamaa baada ya kuzungumza akaniambia anaishi Manzese Dar es salaam na akasema atanirejeshea.
Kuepusha lawama msibani wasidhani pesa nimetumia ikabidi nikope niitume halafu mimi nibaki kupambania deni,yule jamaa hela hakuirudisha na nikawa nampigia simu ananiambia nisimsumbue,aiseee ile haikuwa kubwa sana lakini nilisema lazima nimshikishe jamaa adabu.
Unajua kuna watu huwa hawajali pesa wanayopoteza,tatizo huwa linakuja kwa wapokea pesa,huwa wanakera na kuudhi sana hata kama hujafikiria kufanya jambo baya inakubidi ufanye jambo ili heshima iwepo.
Yule jamaa mwanzo nilimwambia asiponirudishia hiyo hela kwenye akaunti yangu atajuta kuzaliwa akadhani utani,safari hii sikutaka kutumia nguvu za Kikurya,nilipanga nitumie nguvu za wenye uwezo mbadala.
Kufupisha,Jamaa alikuwa ananitafuta baada ya kumkarabati analia nikamwambia sina muda yeye aendelee kula matanuzi!.
Aiseee baada ya kubembelezwa sana ndugu zake na hii ni baada ya miezi 7 ndipo tukaonana pale Rombo Green View wakanirudishia hela yangu nikachafua zangu,ingawa walidai wanilipe fidia mimi nikakataa nikawaambia sihitaji dhuruma nahitaji pesa nilikosea kutuma!.
Jamaa hata kaa anisahau hadi anaingia kaburini na hiyo pia itakuwa imempa funzo!.
MIMI SEHEMU YA NGUVU HUWA NATUMIA NGUVU ILA SEHEMU YA WAJUBA HUWA NAWAACHA WAJUBA WAFANYE KAZI YAO!.