Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nakumbuka wakati nipo chuo 2010s nilituma pesa kimakosa, ile pesa nilikuwa namtumia mwenye uhitaji tena kwa haraka.Haya mambo ya hela za mtandao mimi huwa nayaheshimu sana, hujui aliyetuma huko alikokusudia kutuma ilikuwa ikafanye kazi gani?je mgonjwa yupo mahututi?msiba au ada?
Mwaka 2003 kipindi hiko hakuna pesa za kwenye simu jamaa yangu mama yake alikuwa na historia ya maradhi ya mara kwa mara na ya ghafla so yeye ndiyo mkubwa akawa yupo town anatafuta ndugu zake wapo Arusha,alikuwa mlinzi muajiriwa wa wanaokumbuka kampuni ya GOHA SECURITY hawa walikuwa Magomeni Mapipa,siku moja ikapigwa simu nipo nae ilikuwa jioni ya 16:00 mama ameumwa tena na inatakiwa haraka hela kwa ajili ya dawa na huduma nyinginezo.
Jamaa alikuwa na akiba yake Tsh 50,000/= so ikabidi anunue voucher za Voda kisha nduguze kule kijijini wa-make deal na muuza vocha na mpigisha simu wa kijiji vocha itumwe kwake awe anaiuza kwa kurusha then akate itakayomtosha baki wapewe wakamuhudumie mama yao,jamaa akakosea namba moja mtu yupo Kigoma aloo ilikuwa balaa.
To cut a long story jamaa alikataa kurudisha hela huku ndugu wa jamaa wanapiga mama anakufa hospital wamekataa kumuhudumia ikabidi apige tena simu Kigoma kwa jamaa huku analia kama mtoto akimuomba arudishe japo kidogo maana hela ilikuwa ni kwa ajili ya matibabu ndiyo kidogo jamaa akawa na huruma akarudisha japo sikumbuki kama alirudisha hata 40K,hii ilituumiza hata sisi kwa ile hali jamaa alikuwa anapitia.
So kwa yeyote atakaesoma hapa ajue anaweza akawa sababu za kifo cha mtu tujifunze kutokula visivyotuhusu.(nimekazia sana kwenye suala la kifo kwa sababu ndiyo sehemu pekee isiyokuwa na option ya subira)
Mungu mkubwa,miujiza hii,but Mungu ndiye anaejua.[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]2020 nilikosea kumtumia mtu 206,000. Ilikuwa ni malipo ya hela ya Chakula ya vibarua kwenye site yangu.
Nilikuwa busy kidogo, ilipofika tu jamaa niliyempigiaa simu akapiga. Nikamuandikia ujumbe kuwa tayari nimeshatuma. Niliamini ni fundi anauliza. Jamaa, akaniandikia pokea mara moja.
Akapiga lakini niligundua si sauti ya fundi. Akaniambia kuna fedha nimemtumia ila anaomba asirudishe. Nilipanick kidogo, jamaa akanielezea story ya magumu anayopitia. Anaomba sana nimuachie kiasi kile cha hela. Akaniambia kama sitaridhia atarudisha kiasi hicho punde baada ya kukata simu.
Lakini kwa magumu yale, niliridhia kumuachia kiasi hicho cha pesa. Ukweli ni kuwa niliokoa maisha ya mwanae. Na maombi yake yalijibiwa kupitia mimi. Nilifanya alternative nyingine kuwesesha kule site.
Jioni nilipata dili zuri mno. Nikajua tu ni Mungu ananilipa kwa Sadaka yangu ya asubuhi.
Nazani bila kusema jeneza au msiba isingeludi hiyo Hela [emoji1]Kuna siku saa kumi na moja asubh nasikia simu inaita nkapokea nko na usngz namba ngen inaniulza mshaanza safar nkamjbu apana nkakata cm nkaendelea kulala kumbe aliendelea kupga akatuma na hela 350000 ma msg za kutosha kua tupitie jeneza tuje nalo, naamka sa mbil ndio naona msg na miscal za kutosha kupga ipe simu haipatikan nikaanza kuumiza kichwa huu msba wa wap nije na jeneza wap inafka sa sita simu inapgwa tena jamaa anaongea kilugha kwa ukali hatar nkamwambia mm skuelew unasema nn ndio akaanza kuongea kiswahil kua wanasubr jeneza mazish ni saa nane mchana nkamwambia itakua mmekosea namba mm nko mkoa flan jamaa akanza kuomba nimrudishie iko kias kwa haraka kabisa nkasema sawa nakutumia nkaMrushia kias chao japo ilkua imekatwa mpawa 18000 nkaenda kuiongezea kwa wakala.. usile kisicho kua cha haki yako wazee
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hela za tala na branch hazina dhambi zile. Sijawah juta
😁😁 Kwanza asingetuma msg angekuta nshalewa sana imebak labda 72000Nazani bila kusema jeneza au msiba isingeludi hiyo Hela [emoji1]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16] Kwanza asingetuma msg angekuta nshalewa sana imebak labda 72000
Mungu anakupima imani yako,Mungu anisamehe sana inawezakana ndo mana ridhiki zangu haziji
Watu walishawahi kosea kwangu =
150,000
95,000
80,000
Hizi 50,000 na zaidi ya mara 4
Sikuwahi kurudisha hata mia nliishia kuwablock
daah kuna mtu nakumbuka nilkosea kutuma hela kwakwe sh 52,000 ilikuwa namtumia mchepuko, nikapiga huduma kwa wateja kwasababu ile no ilikuwa Mtandao tofaut na mm.
niliambiwa nisubili masaa 72, ilikuwa jmos basi nikampigia yule jamaa nikamwambia nikosea kutuma hela kwakwe aniludishie walau 30,000 tuh, jamaa kweli akarudisha 30,000 nikamshukuru.
Nimekaa j3 sina mpango wowote naona messag ya muhamala unaiangia kwenye simu yangu hela imerudishwa, walah sikulemba nikaihamisha ile hela jamaa alipiga mara 3 sikupokea ila hakupiga tena
Hatimaye nimekutana na hii comment,,Hii thd kila mtu ni mwema na kila mtu ni muaminifu,unaweza kufikiri wachangiaji wa leo kwenye hii thd wote ni malaika wema kutoka peponi.
😀 😀
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Na sisi tuliotumiwa kimakosa halafu songesha wakakata chao tunaruhusiwa kurejesha?[emoji23]
TeacherrrKunamtu nilikosea kumtumia laki na nusu aisee halafu nilikuwa nalipa deni la mtu, nilipitia kipindi kigumu yule dada alikataa kurudisha. Kuwapigia tigo wakasema ashaitoa namba yake ninayo Hadi Leo.
Ila ipo siku
Nataka nifanye hivoMungu anakupima imani yako,
Wewe hauna huruma,
Omba msamaha,jutia
Kama mimi tuMimi kuna mtu nilimuahidi kumchangia Harusi halafu sikumchangia... kiukweli roho iliniuma Sana kila ninapo kutana nae...
Kama ningejua ningemchangia tu...
Imeniumiza kuliko hela ambayo ningemchangia
Mtaua watu kwa presha.iliwahi kunitokea hiyo mwaka 2011 meseji imeingia kucheki laki 7 imeingia na ukifikiria sikuwa na kitu mfukoni aisee nilikodi bodaboda kwenda kijiji cha jirani kuitoa pesa njiani akawa ananipigia nikamwambia nipo barabarani nikifika nakurudishia hela yako ondoa shaka nilipofika kwa wakala nikaichomoa yote
Wale lazima wadhurumiwe sababu riba zao ni za dhurumaHuwa najiuliza, hivi wanaojisifu kudhulumu hela za mikopo ya hizi apps kama tala na branch wanatoa wapi ujasiri? Hivi hela uchukue bure na mwenye hela aridhike tu? Tafakari
Tubu aisee,Nataka nifanye hivo
Nitajaribu kutubu, vipi baba Ako mdogo aliacha tabia yake yakula kitimoto ?Tubu aisee,