Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Nilikoseaga kutuma laki 8,bahati alipokea mstaafu wa jeshi la magereza ni mtu mzito sana ,keaho yake alinipa yoote pale kibo complex,emagin alitoka gongolamboto kwaajili yangu
Mimi ni mstaafu wa jeshi moja hapa nchini, niliwahi mrudishia mtu mmoja hela yake yote laki nane pamoja na ya kutolea niliongezea pale kibo complex

Sipendi dhuluma kabisa
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote. Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650. Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

N.b. Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Mkisharogwa ndo mnakuja hapa kupapatika qumaninar, sasa omba mungu mganga aliekuroga awe hai maana kama kafa utapapatika hadi kifo, na hapo ndo mjue jasho la mtu haliliwi kizembe.


piga nyundo
 
Hii dhambi 2015 niliikataa baada ya ndugu mmoja kutuma kimakosa kwenye line yangu ya airtel laki nane na hamsini elfu (850,000/=) kwa kumrudishia yote, japo nilikuwa juu ya mawe.
Huo ndiyo utu kitu hujakitolea jasho hakuna hasara kumrudishia muhusika rudisha utapewa kwa njia nyengine

Ni ajali nimekutana nazo mara chungu mbovu ila nashukuru moyo wa tamaa umekuwa mbali na nafsi yangu mara zote nawarudishia wenyewe nachofanya nakata zile charges za miamala tu kati ya mtandao kwa mtandao
 
Roho iliniuma nilipata ela Kwa tabu aisee
Uaminifu ni kitu muhimu na una baraka zake.
Sadaka: Juzi niliona bibi kakaa barabarani kajikunyata nikamfuata vipi mbona hupandi gari akasema anasubiri walipwe hela ya kibarua buku nne ya kufagia barabara ilibaki nusu nilie. Nikampa elf 20. Siku hiyo jioni yake nikapata hiyo mara 30. Niliconnect.
 
Kuna jamaa niliwahi kumtumia hela ya Michango ya msiba kimakosa,jamaa baada ya kuzungumza akaniambia anaishi Manzese Dar es salaam na akasema atanirejeshea.

Kuepusha lawama msibani wasidhani pesa nimetumia ikabidi nikope niitume halafu mimi nibaki kupambania deni,yule jamaa hela hakuirudisha na nikawa nampigia simu ananiambia nisimsumbue,aiseee ile haikuwa kubwa sana lakini nilisema lazima nimshikishe jamaa adabu.

Unajua kuna watu huwa hawajali pesa wanayopoteza,tatizo huwa linakuja kwa wapokea pesa,huwa wanakera na kuudhi sana hata kama hujafikiria kufanya jambo baya inakubidi ufanye jambo ili heshima iwepo.

Yule jamaa mwanzo nilimwambia asiponirudishia hiyo hela kwenye akaunti yangu atajuta kuzaliwa akadhani utani,safari hii sikutaka kutumia nguvu za Kikurya,nilipanga nitumie nguvu za wenye uwezo mbadala.

Kufupisha,Jamaa alikuwa ananitafuta baada ya kumkarabati analia nikamwambia sina muda yeye aendelee kula matanuzi!.

Aiseee baada ya kubembelezwa sana ndugu zake na hii ni baada ya miezi 7 ndipo tukaonana pale Rombo Green View wakanirudishia hela yangu nikachafua zangu,ingawa walidai wanilipe fidia mimi nikakataa nikawaambia sihitaji dhuruma nahitaji pesa nilikosea kutuma!.

Jamaa hata kaa anisahau hadi anaingia kaburini na hiyo pia itakuwa imempa funzo!.


MIMI SEHEMU YA NGUVU HUWA NATUMIA NGUVU ILA SEHEMU YA WAJUBA HUWA NAWAACHA WAJUBA WAFANYE KAZI YAO!.
 
Back
Top Bottom