Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Kuna mtu alikoseaga kutuma pesa kwangu,ilikuwa kama 25,000 nikampigia nikamwambia arudishe pesa yake kakosea kutuma, nikamwambia mie lain yangu imefungiwa upande wa mihamala

Aisee alinitukana yule mbaba,akaniambia nirudishe pesa yake,mimi ni mwizi,nikamuuliza ningekuwa mwizi nisingekujulisha kama umekosea kutuma pesa? nikamwambia sina shida ya pesa na naomba ufanye uirejeshe kwako,

Akairejesha, siku ya pili akanitafuta na kuniomba msamaha,
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote. Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650. Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

N.b. Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Itakua jamaa kamuendea kwa sangoma 😋😋
 
Nilikosea kutuma laki 6 kwenye namba tofauti nikampigia jamaa mwenye namba alivyopokea tu akaanza kucheka, nikamuomba anirudishie hata laki 4 akawa ananizungusha mara subiri kidogo niko sehemu mbaya nikiwa poa nitairudisha, nahisi alikuwa ana buy time akaitoe, ghafla akili ikanijia nikatumia simu nyingine kuwapigia TigoPesa wakai block ile transaction na ndio muda huohuo nahisi jamaa alikuwa ameshafika kwa wakala akanipigia anacheka akasema bahati yangu! Next day jioni pesa ikarudishwa kwenye Account yangu.
 
RAIA hawanaga huruma
 
Mm nilitumiwa pesa tar.7/07/2023 nikajua ataomba muamala urudishwe Kumbe hakurudisha , Jana nikakumbuka nikampigia Simu kapokea nikamielekeza akasema Kweli nilikosea ila mm mwenye hapa nilipo nipo taaban ninaumwa kwahiyo nilishindwa hata kuirudisha hiyo pesa.Kwa nilivyokuwa naongea nae nikweli anaonekana yupo hoi,basi nimemrudishia ameshukuru kweli.

Niwaombe mtu akituma pesa kimakosa irejeshe

Sent from my Infinix X6511E using JamiiForums mobile app
Mkuu hiyo tarehe umeiangalia vzr ??
 
Haki huinua taifa, haki huinua familia, haki huinua mtu binafsi mpaka vizazi vyao, mtu mwenye haki yake akikushitakia kwa Mungu lazima ukipate hata kipindi kikipita muda mrefu, jitahidi umpate umuombe musamaha kwa faida yako na kizazi chako, ila ukimkosa kabisa basi fanya toba ya kuvunja bonds na hizo pesa na ukazitoe kwenye mikono yako kwa kuzitoa zitakaswe zikatumike huko.
 
Binafsi nina visa viwili

1) Mwaka 2009 nimemaliza kidato cha 4 nimerudi zangu kijijini nimetulia nawapigia pindi madogo wa primary na wale waliokua wanajiandaa kwenda form one, cku moja jioni nikiwa class na madogo wa darasa la Saba tunapiga pindi la namba ikaingia meseji ya Mpesa nilikua natumia kisimu cha Nokia cha bi mkubwa nimeweka laini yangu maana bi mkubwa hakua na mambo mengi ya cmu.
Lkn pia nilimpanga kua naomba nikae na cmu ili iwe rahisi mm kufuatilia matokeo.

Kucheki muamala ni tsh. 5000/, naomba nieleweke wakuu ilikua elfu 5000/
Hali niliyokua nayokiuchumi nyie acheni maana ile hela niliona kama jamaa katuma elfu 50. Basi bwana nikiwa naendelea na pindi ikaingia namba ngeni kupokea ni mshkaji analia anasema nakuomba ndugu yangu nimekosea kutuma pesa, na hii pesa nilikua namtumia mdogo wangu Yuko chuo cha ualimu sehemu fulani naomba unisaidie maana hana hela ya kula kabisa nakuomba sana ndugu yangu.

Huruma ikaniingia nikamwambia ndugu kwenye smu yangu sikua na pesa yoyote hivyo sitaweza kuituma elfu 5000/ hivyo nitatuma kiasi cha tsh. 4500/. Jamaa akasema sawa ila hakuamini kama nitairejesha ile pesa alifikia hatua akanitumia namba ya mdogo wake na akamtumia pia namba yangu ili anibembeleze nirudishe muamala.
Nilifanya hivyo jamaa alinishukuru Sana na hata yule Binti alinishukuru Sana jamani acheni haya maisha haya.
 
Nini kilichoendelea na binti? Kwa bongo movie tayari hii stori yako inatengeneza movie.
 
Mimi nilitumiwa kimakosa 250k alafu mbaya zaidi nipo kwenye kikao, simu na sms zikiingia simu inavibrate mimi wala sikuwa nahangaika nayo. Yule dada alipiga zaidi ya mara 20 na sms kibao mimi wala sikuwa najishugurisha na simu. Ulipofika muda wa lunch ndipo nikajiambia ngoja niangalie waliokuwa wananitafuta, gafra nakuta muamala wa laki mbili na nusu kutoka kwa wakala, pia missed calls number moja ikiwa inaongoza kunipigia mara nyingi. Nikaipiga ile number, masikini ya Mungu dada wa watu analia mama ake anaumwa sana Kigoma na mpaka muda huo ndugu wameshampigia sana simu wakimlaumu kwakuchelewesha hiyo pesa. Huruma ilinijaa, nikamwambia anipe number aliyokuwa anakusudia kuirusha hiyo pesa na kumuelewesha kuwa sikufanya makusudi kutopokea simu zake nilikuwa kwenye kikao. Yule dada alikuwa akiitikia kwa wasiwasi tu maana yalishapita zaidi ya masaa manne.
Aluponipa tu number muda huo huo nikairusha ile fedha bila kupunguza hata senti tano pamoja na kukatwa hela ya kurushia kwenye akaunti yangu. Nilipigiwa simu mpaka na ndugu zake wa huko Kigoma wakinishukuru sana na kuniombea baraka tele. Yule dada tuliendelea kuwasiliana bila kujuana baada ya muda mawasiliano yakafifia na kupotezana mpaka leo.
Somo; HUWEZI JUA HIYO PESA ILIYOKOSEWA DESTINATION IKAJA KWAKO ILITAKIWA KUFANYA NINI, KWAKUIRUDISHA UNAWEZA UKAWA UMEOKOA MAISHA YA MTU AU KUMTOA MTU KWENYE TATIZO LINALOMKABILI NA MUNGU AKAKUBARIKI.
 
Niliwahi ingiziwa milioni 4kwenye akaunti yangu ya benki kimakosa nilikuwa naangalia tu.

Kwanza nilihisi mtego huu.

Sikujisumbua nayo.

Nilikuwa na uwezo wa kwenda ikomba yote muda huo huo.

Ila nikajiamba achana nayo

Kesho asubuhi nikakuta haipo wameirudisha
Uwoga wako ndiyo Umasikini wako!! Hiyo ungechukua ukafanyie Mambo yako,alafu wakisanuka mnakaa chini mnaelewana kulipa Deni bila riba na kwa kuzingatia kipato chako pia!!!
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote. Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650. Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

N.b. Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Pumbafu zenu matapeli, sitasahau nilipigwa 375,000 hivi hivi nikimtumia mfanyakazi wangu alikuwa na shida.
Mpokeaji alipokea akazutia na kunitukana sana.

Mbwa nyie wenye tamaa, wakati mimi nilitumiwa 1,500,000 ikakaa siku 2 nikisubiria mwenyewe azirudishe.
 
Kuna watu wapuuzi hii dunia basi tu Uchungu nilionao Mungu ndo anajua [emoji24][emoji24]. Juzi tar 19/06/2023 Nilikua nalipia ticket yangu ya ndege off to Amsterdam muda wa booking ulikua unakaribia kuisha nimebakiza 5 minutes, fare yangu iwe cancelled nikatuma pesa mara 2, Jm travel services, muamala wa kwanza million 1 na laki 6, na wa 2 million 1 na laki 6, nimeshtuka yote imeenda message zilichelewa kurudi.

Nikapiga simu tigo nikawambia nimekosea kutuma mara 2 inatakiwa wakate muamala mmoja, imagine tigo wakathibisha miamala yote imefika kwa muhusika hawawezi kurudisha niwasiliane na Jm travel services.

Nikapiga simu nikatumiwa ticket yangu lakini muamala hawakurudisha na hapo ni jioni saa 10 na mimi Natakiwa kuondoka usiku saa 5 na KLM.

Nimepiga simu mpaka saa 2 usiku wanajibu kua wanashughulikia mpaka sasa sijapokea hela yangu, na sina uwezo wa kuwafikia jamaa namtafuta whatsp ni muhindi anasema wanashughulikia dah [emoji24][emoji24][emoji24].

Mungu yupo huyu muhindi japo sibagui watu ila nikirudi bongo ntamuwashia moto. Ndo akiba Nilikua nategemea inisaidie safarini lakini ameamua kunidhulumu sawa tu.

Note nina vielelezo vyote

Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:724726 Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 1,892,567. Muamala: 36246309377. 19/06/23 15:55.

Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:BWTAZM Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 289,167. Muamala: 86426520238. 19/06/23 15:56.
 
2) kisa cha pili.
Nilifanikiwa kufaulu na kujiunga na chuo cha ufundi Arusha (Arusha tec), nikafanikiwa kumaliza diploma ya civil.
Nikiwa nimerudi zangu pande za mkoa wa mara nikisubiri sherehe za kupewa gamba. Nilifanikiwa kukutana na Mhandisi mmoja alikua anafanya kazi kwenye COMPANY moja pale bunda lkn alikua anafanya kazi kwa mkataba maalum kulingana na kazi ambazo kampuni imepata yaani alikua anasimamia kazi ambazo ni kiwango cha Rami na sio zile za kiwango cha changarawe.
Basi bwana cku moja nimeamka nikatumia transcript zangu nikafika pale mwamba akanipeleka site maana kulikua na kazi pale mjini bunda kweli engineer akanikubali na kuniombea kwenye kampuni nisaidiane nae. Lkn sikupewa mkataba wowote hivyo mm nili TAKE advantage ya kujifunza kazi maana engineer alikua vzr Sana kwenye survey, barabara na structure za barabara .
Sasa bwana kutokana na kuonekana ndo nimetoka chuo mwamba aliekua anahusika na malipo kwa wafanyakazi hakua fair kwangu cku akijisikia napewa elfu 10 wakati mwingine elfu 15 na hata elfu 5 au naondoka mswaki, na nyakati zingine inafikia mahala engineer wangu anatoa hela yake maana alinikubali Sana kwenye kazi hata asipokuepo site anajua ameacha mtu sahihi.

Sasa bwana niende kwenye kisa chenyewe
Cku moja nimeamka asubuhi na mapema ilikua ni kawaida yangu, nimefika ofisini nikakuta dogo aliekua anahusika na usafi bahati nzuri keshafika na kesha maliza usafi,
Nimeingia nimepitia work plan ya cku hiyo na kufanya yaliyotakiwa kufanyika cku hiyo pale ofisini kabla ya kwenda site au kusubiri Mhandisi afike atoe maelekezo mengine. Bahati nzuri Mhandisi amefika hakuna mabadiliko ktk mpango kazi, hivyo tukajiandaa kwenda site.
Nikajiambia ngoja nitoke nje niote ka jua kidogo wakati tunasubiri gari ya site ifike, hapo mfukoni Nina elfu 5000/ tuu 2013 hiyo wakuu, natupa jicho pembeni kidogo namuona Binti mjamzito akiwa amekaa pembezoni kwenye ukuta wa ofisini amejikunyata na alionekana mwenye mawazo na njaaa iliyoambatana na uchovu, nikapata shauku ya kujua nn hasa kimemuweka pale, lkn kabla ya kufanya hivyo ikabidi nimuite yule dogo wa usafi nikamuuliza vipi kuhusu huyu Binti mbona sielewi, na amekuepo hapa nje kwa muda gani hiyo ni saa mbili inaelekea saa 3 asubuhi. Dogo akanambia yy amefika pale mapema Sana na amemkuta Binti akiwa pale amelala hapo hapo nje ikabidi amwamshe alivyojaribu kumuuliza Binti hakutoa ushirikiano zaidi ya kulia.

Basi ikabidi nirudi kwa Binti nikamuuliza taratibu na kwa sauti ya upole, baada ya muda ikabidi Binti anifungukie huku akilia na kujuta kufika ktk ule mji wa bunda.

Binti anasema alipigiwa cmu na bwana ake ambae ndie mhusika wa ule ujauzito ambao kwa makadirio ulikua ni wa miezi sita hadi Saba, Binti anasema nyumbani kwao ni Kijiji kinaitwa PIDA yaani ukitoka bunda unaelekea bitaraguru, mwibagi then unafika PIDA kwa wenyeji wa maeneo hayo watanielewa, anasema alifanikiwa kupata nauli tuu ya kumtoa kwao hadi bunda ambayo ni kiasi cha tsh. 1500/ kwa miaka hiyo ya 2013 na baada ya kufika bunda jamaa akazima cmu na wakati huo Binti hakua na cmu Bali alikua anatumia ya rafiki yake pale kijijini na kwenye gari aliomba apigiwe namba aliyokua ameandika kwenye karatasi na hata mm nilivyojaribu kuipiga haikupatika

Binti anasema toka alivyofika Jana majira ya saa nane mchana na kujaribu kumtafuta mwamba bila mafanikio akajikuta ucku unamkuta akiwa maeneo Yale ya ofisini na alikua hajala na wala hakua na mahala pa kulala hivyo ikambidi alale pale tulipomkuta. Ombi lake kwangu lilikua moja tuu nimsaidie apate kula na nauli ya kurudi kwao,, aiseee nilikua kama vile nimepigwa na kitu kizito kichwani.

Wakuu mkumbuke nilivyoeleza hapo awali kuhusu malipo na uhakika wa kupata chochote maana kuna wakati nilikua nashinda bila kula na kazi napiga na kuhusu hiyo elfu 5 niliyokua nayo naipigia hesabu ya kupata lunch na maji ili nibakize chenji kesho mambo yaende, alafu mwanadada ananiletea pigo za style hiyo aiseee nikaishiwa pozi huku huruma inatawala na shida zangu zinasumbua.
Ikabidi nimshirikishe Mhandisi wangu juu ya lile swala, Mhandisi ananiambia yy hayuko vzr kabisa,
Kidume nikakata shauri juu ya kumsaidia huyu Binti nikasema ngoja nikamnunulie chakula alafu nauli atajiongeza,
Nika mpeleka mgahawani upande wa pili wa barabara kuu ya mwanza MUSOMA via Bunda,, nikaagiza wali maharage na chai 2500/ aisee yule Dada alikula hadi nikaogopa na alivyomaliza tuu alishusha pumzi na kutoa shukrani sio ya nchi hii.
Basi bwana Binti akaomba maji na akasema anaomba Sana nimsaidie nauli arudi home ikumbukwe mm hata chai kavu sijapata nikamnunulia maji na kumpandisha kwenye gari nami nikabaki mweupe bila hata mia yaani ile elfu tano ilitumika yote na wenzangu walishatangulia site.
Binti akaondoka nami ikanibidi nitembee kwa mguu kwenda site maana ilikua sio mbali kampuni ilikua imepata mradi wa kuboresha barabara za mitaa kwa kiwango cha Rami ikiwemo barabara ya bomani.
Yule Dada niliamini alifika kwao salama nami nikaendelea na maisha yangu.

Kubwa zaidi baada ya cku hiyo yaani kesho yake nilitafutwa na rafiki yangu fulani hivi kua kuna ndugu yake ameomba tenda ya kukarabati barabara ya changarawe yenye urefu wa km 46.6 na alihitaji mtu wa kumfanyia ( BOQ ) makisio ya kukarabati hiyo barabara aisee nilifurahi Sana na ile kazi niliifanya ucku uleule iliponikia na kesho yake nikaenda kuwasilisha hiyo tender document na baada ya wiki nilikwenda kusaini mkataba maana ile kampuni ilishinda ile tender na tayari nilishalipwa pesa yangu laki na nusu ya kitanzia toka cku niliyopewa ile kazi rafiki yangu na ndugu yake walinishukuru.
Kwa kumalizia tuu ni kwamba ile pesa ilinisaidia Sana na niliona nimelipwa milioni moja na nusu na sio laki na nusu na nilimshukuru Sana Mungu lkn pia nilimshukuru Sana yule Binti maana naamini aliniombea Sana pale nipokua nimetoa kwa ajili yake

Najua imekua ndefu naomba mnisamehe kwa mliokwazika
 
Nini kilichoendelea na binti? Kwa bongo movie tayari hii stori yako inatengeneza movie.
Hapana mkuu maana hata cmu nilikua CNA hivyo nilivyoondoka kwenda shule 2010 ikumbukwe ulikua ukichaguliwa kwenda vyuo vya ufundi unakaa karibia mwaka mzima toka umehitimu cmu ilikua ya bi mkubwa Wala ckuwahi kufikiria juu yake maana niliona nilichokifanya ni kitu cha kawaida Sana na niliona Niko na deni la kulipa kwani badala ya kutuma elfu 5 nikatuma 4500/
 
Back
Top Bottom