Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

2) kisa cha pili.
Nilifanikiwa kufaulu na kujiunga na chuo cha ufundi Arusha (Arusha tec), nikafanikiwa kumaliza diploma ya civil.
Nikiwa nimerudi zangu pande za mkoa wa mara nikisubiri sherehe za kupewa gamba. Nilifanikiwa kukutana na Mhandisi mmoja alikua anafanya kazi kwenye COMPANY moja pale bunda lkn alikua anafanya kazi kwa mkataba maalum kulingana na kazi ambazo kampuni imepata yaani alikua anasimamia kazi ambazo ni kiwango cha Rami na sio zile za kiwango cha changarawe.
Basi bwana cku moja nimeamka nikatumia transcript zangu nikafika pale mwamba akanipeleka site maana kulikua na kazi pale mjini bunda kweli engineer akanikubali na kuniombea kwenye kampuni nisaidiane nae. Lkn sikupewa mkataba wowote hivyo mm nili TAKE advantage ya kujifunza kazi maana engineer alikua vzr Sana kwenye survey, barabara na structure za barabara .
Sasa bwana kutokana na kuonekana ndo nimetoka chuo mwamba aliekua anahusika na malipo kwa wafanyakazi hakua fair kwangu cku akijisikia napewa elfu 10 wakati mwingine elfu 15 na hata elfu 5 au naondoka mswaki, na nyakati zingine inafikia mahala engineer wangu anatoa hela yake maana alinikubali Sana kwenye kazi hata asipokuepo site anajua ameacha mtu sahihi.

Sasa bwana niende kwenye kisa chenyewe
Cku moja nimeamka asubuhi na mapema ilikua ni kawaida yangu, nimefika ofisini nikakuta dogo aliekua anahusika na usafi bahati nzuri keshafika na kesha maliza usafi,
Nimeingia nimepitia work plan ya cku hiyo na kufanya yaliyotakiwa kufanyika cku hiyo pale ofisini kabla ya kwenda site au kusubiri Mhandisi afike atoe maelekezo mengine. Bahati nzuri Mhandisi amefika hakuna mabadiliko ktk mpango kazi, hivyo tukajiandaa kwenda site.
Nikajiambia ngoja nitoke nje niote ka jua kidogo wakati tunasubiri gari ya site ifike, hapo mfukoni Nina elfu 5000/ tuu 2013 hiyo wakuu, natupa jicho pembeni kidogo namuona Binti mjamzito akiwa amekaa pembezoni kwenye ukuta wa ofisini amejikunyata na alionekana mwenye mawazo na njaaa iliyoambatana na uchovu, nikapata shauku ya kujua nn hasa kimemuweka pale, lkn kabla ya kufanya hivyo ikabidi nimuite yule dogo wa usafi nikamuuliza vipi kuhusu huyu Binti mbona sielewi, na amekuepo hapa nje kwa muda gani hiyo ni saa mbili inaelekea saa 3 asubuhi. Dogo akanambia yy amefika pale mapema Sana na amemkuta Binti akiwa pale amelala hapo hapo nje ikabidi amwamshe alivyojaribu kumuuliza Binti hakutoa ushirikiano zaidi ya kulia.

Basi ikabidi nirudi kwa Binti nikamuuliza taratibu na kwa sauti ya upole, baada ya muda ikabidi Binti anifungukie huku akilia na kujuta kufika ktk ule mji wa bunda.

Binti anasema alipigiwa cmu na bwana ake ambae ndie mhusika wa ule ujauzito ambao kwa makadirio ulikua ni wa miezi sita hadi Saba, Binti anasema nyumbani kwao ni Kijiji kinaitwa PIDA yaani ukitoka bunda unaelekea bitaraguru, mwibagi then unafika PIDA kwa wenyeji wa maeneo hayo watanielewa, anasema alifanikiwa kupata nauli tuu ya kumtoa kwao hadi bunda ambayo ni kiasi cha tsh. 1500/ kwa miaka hiyo ya 2013 na baada ya kufika bunda jamaa akazima cmu na wakati huo Binti hakua na cmu Bali alikua anatumia ya rafiki yake pale kijijini na kwenye gari aliomba apigiwe namba aliyokua ameandika kwenye karatasi na hata mm nilivyojaribu kuipiga haikupatika

Binti anasema toka alivyofika Jana majira ya saa nane mchana na kujaribu kumtafuta mwamba bila mafanikio akajikuta ucku unamkuta akiwa maeneo Yale ya ofisini na alikua hajala na wala hakua na mahala pa kulala hivyo ikambidi alale pale tulipomkuta. Ombi lake kwangu lilikua moja tuu nimsaidie apate kula na nauli ya kurudi kwao,, aiseee nilikua kama vile nimepigwa na kitu kizito kichwani.

Wakuu mkumbuke nilivyoeleza hapo awali kuhusu malipo na uhakika wa kupata chochote maana kuna wakati nilikua nashinda bila kula na kazi napiga na kuhusu hiyo elfu 5 niliyokua nayo naipigia hesabu ya kupata lunch na maji ili nibakize chenji kesho mambo yaende, alafu mwanadada ananiletea pigo za style hiyo aiseee nikaishiwa pozi huku huruma inatawala na shida zangu zinasumbua.
Ikabidi nimshirikishe Mhandisi wangu juu ya lile swala, Mhandisi ananiambia yy hayuko vzr kabisa,
Kidume nikakata shauri juu ya kumsaidia huyu Binti nikasema ngoja nikamnunulie chakula alafu nauli atajiongeza,
Nika mpeleka mgahawani upande wa pili wa barabara kuu ya mwanza MUSOMA via Bunda,, nikaagiza wali maharage na chai 2500/ aisee yule Dada alikula hadi nikaogopa na alivyomaliza tuu alishusha pumzi na kutoa shukrani sio ya nchi hii.
Basi bwana Binti akaomba maji na akasema anaomba Sana nimsaidie nauli arudi home ikumbukwe mm hata chai kavu sijapata nikamnunulia maji na kumpandisha kwenye gari nami nikabaki mweupe bila hata mia yaani ile elfu tano ilitumika yote na wenzangu walishatangulia site.
Binti akaondoka nami ikanibidi nitembee kwa mguu kwenda site maana ilikua sio mbali kampuni ilikua imepata mradi wa kuboresha barabara za mitaa kwa kiwango cha Rami ikiwemo barabara ya bomani.
Yule Dada niliamini alifika kwao salama nami nikaendelea na maisha yangu.

Kubwa zaidi baada ya cku hiyo yaani kesho yake nilitafutwa na rafiki yangu fulani hivi kua kuna ndugu yake ameomba tenda ya kukarabati barabara ya changarawe yenye urefu wa km 46.6 na alihitaji mtu wa kumfanyia ( BOQ ) makisio ya kukarabati hiyo barabara aisee nilifurahi Sana na ile kazi niliifanya ucku uleule iliponikia na kesho yake nikaenda kuwasilisha hiyo tender document na baada ya wiki nilikwenda kusaini mkataba maana ile kampuni ilishinda ile tender na tayari nilishalipwa pesa yangu laki na nusu ya kitanzia toka cku niliyopewa ile kazi rafiki yangu na ndugu yake walinishukuru.
Kwa kumalizia tuu ni kwamba ile pesa ilinisaidia Sana na niliona nimelipwa milioni moja na nusu na sio laki na nusu na nilimshukuru Sana Mungu lkn pia nilimshukuru Sana yule Binti maana naamini aliniombea Sana pale nipokua nimetoa kwa ajili yake

Najua imekua ndefu naomba mnisamehe kwa mliokwazika
Ubarikiwe sana. Kisa hiki kimenigusa sana.
 
Shida hali ngumu kila Jambo tunaona furusa, hata ukizimikiwa na gari barabarani kwa bahati mbaya,watakao jitokeza kusaidia ni wale wa furusa la sivyo wanakuacha hapo hapo!!
Kweli kabisa.
 
Wanadamu tunatofautiana pakubwa sana
Wengine sijui tunaishi maisha gani

Watu wamekua watu wa hovyo hovyo tu
Imani 0
Utu 0
Upendo 0
Yaani tunaishi kama wanyama

Juzi tupo ofsin secretary wetu (mdada) anajisifia alivyo kimbia na laki ya watu kweli?

Ilikua hivi alikua na shida na hela kiasi cha laki moja hivi
Akaenda kwa wakala kuitoa wakala alidai hakuna mtandao hivyo aje wakati mwingine
Kwakua alikua na shida ya haraka basi akaomba apewe laki moja ili aitumie
Yule dada ki uungwana akampa kwakua anafahamika
After siku chache akaenda kutoa 200000 ili arudishe deni na abaki na 100,000
Yule dada akampa yote 200000 dada akageuka akaondoka
Hadi leo Yule sister hajakumbuka kitu
Na yapata muda mrefu sana

Watu hawana maana
Hovyo kabisa
 
Kuna watu wapuuzi hii dunia basi tu Uchungu nilionao Mungu ndo anajua [emoji24][emoji24]. Juzi tar 19/06/2023 Nilikua nalipia ticket yangu ya ndege off to Amsterdam muda wa booking ulikua unakaribia kuisha nimebakiza 5 minutes, fare yangu iwe cancelled nikatuma pesa mara 2, Jm travel services, muamala wa kwanza million 1 na laki 6, na wa 2 million 1 na laki 6, nimeshtuka yote imeenda message zilichelewa kurudi.

Nikapiga simu tigo nikawambia nimekosea kutuma mara 2 inatakiwa wakate muamala mmoja, imagine tigo wakathibisha miamala yote imefika kwa muhusika hawawezi kurudisha niwasiliane na Jm travel services.

Nikapiga simu nikatumiwa ticket yangu lakini muamala hawakurudisha na hapo ni jioni saa 10 na mimi Natakiwa kuondoka usiku saa 5 na KLM.

Nimepiga simu mpaka saa 2 usiku wanajibu kua wanashughulikia mpaka sasa sijapokea hela yangu, na sina uwezo wa kuwafikia jamaa namtafuta whatsp ni muhindi anasema wanashughulikia dah [emoji24][emoji24][emoji24].

Mungu yupo huyu muhindi japo sibagui watu ila nikirudi bongo ntamuwashia moto. Ndo akiba Nilikua nategemea inisaidie safarini lakini ameamua kunidhulumu sawa tu.

Note nina vielelezo vyote

Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:724726 Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 1,892,567. Muamala: 36246309377. 19/06/23 15:55.

Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:BWTAZM Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 289,167. Muamala: 86426520238. 19/06/23 15:56.
Pole,wanaweza rudisha
 
Hii mambo ya miamala bn!

Likizo moja hv mzee aliniachia office nkawa nafanya miamala jioni yy anafanya mahesabu, siku hyo mzee alinambia nimtumie mtu hela 450k nikamtumia mara ya kwanza hamna response nliyoona wala feedback nkarudia!

Jioni mzee akawa anapiga hesabu zake akanambia Kuna shoti ya 450k nkajua kbs hii imeenda kwa ile namba alonipa yeye! Nkamweleza aisee alichukia kinoma siku ya pili nikabadilishwa pa kwenda nkawa natembea na watu wa chenso tunakata miti, Kuna tawi la mti lilidondokea sehemu ya nyumba ya watu wakati tunaudondosha! Sikurudi home wiki[emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]saaa ikawaje pesa ilirudi??
 
Wanadamu tunatofautiana pakubwa sana
Wengine sijui tunaishi maisha gani

Watu wamekua watu wa hovyo hovyo tu
Imani 0
Utu 0
Upendo 0
Yaani tunaishi kama wanyama

Juzi tupo ofsin secretary wetu (mdada) anajisifia alivyo kimbia na laki ya watu kweli?

Ilikua hivi alikua na shida na hela kiasi cha laki moja hivi
Akaenda kwa wakala kuitoa wakala alidai hakuna mtandao hivyo aje wakati mwingine
Kwakua alikua na shida ya haraka basi akaomba apewe laki moja ili aitumie
Yule dada ki uungwana akampa kwakua anafahamika
After siku chache akaenda kutoa 200000 ili arudishe deni na abaki na 100,000
Yule dada akampa yote 200000 dada akageuka akaondoka
Hadi leo Yule sister hajakumbuka kitu
Na yapata muda mrefu sana

Watu hawana maana
Hovyo kabisa
Hajielewi
 
Mbona kama Chai, yaani Wakala akosee afu aanze sumbuka kukupigia?

Wakala akikosea anawahi kuwapigia wenye mtandao hela inazuiwa.
Dah we Himars embu tanua uwezo wako wa kufikiri katika hili kidogo tu. Aliyekuwa ananipigia sio wakala bali dada aliyeenda kutuma hiyo pesa. Aliyekosea si wakala, wakala alipewa namba akatuma kwenye hiyo number ikiwa tayari imekosewa then huyo dada akaondoka zake. Wamekuja kugundua kuwa wamekosea baada ya kuuliza huko inapotakiwa kwenda kuwa haijafika, baada ya kuangalia number ndio wakagundua kuna digit wamekosea na kuanza kunipigia.
 
Mungu ana njia nyingi sana za kumpa Mtu riziki yake amtakae,Sasa fikiria Kama Mwalimu ndiyo angekua anataka mkopo wa m9 hayo mashariti na riba angepewa na Bank mwenyewe angeshindwa!!
Asingeweza abadan.... Hakika ni Mungu.....
 
Dah we Himars embu tanua uwezo wako wa kufikiri katika hili kidogo tu. Aliyekuwa ananipigia sio wakala bali dada aliyeenda kutuma hiyo pesa. Aliyekosea si wakala, wakala alipewa namba akatuma kwenye hiyo number ikiwa tayari imekosewa then huyo dada akaondoka zake. Wamekuja kugundua kuwa wamekosea baada ya kuuliza huko inapotakiwa kwenda kuwa haijafika, baada ya kuangalia number ndio wakagundua kuna digit wamekosea na kuanza kunipigia.
Umesema kuwa muamala umetoka kwa wakala,sasa wakala akikosea mbona ni zoezi dogo tu anawasiliana na huduma kwa wateja
 
Mbona kama Chai, yaani Wakala akosee afu aanze sumbuka kukupigia?

Wakala akikosea anawahi kuwapigia wenye mtandao hela inazuiwa.
Hivi unadhani hilo swala limetokea mwaka huu au mwaka jana? Hiyo ilikuwa 2008 mkuu, kipindi hiko ukikosea wee ongea vizuri tu uliyemtumia akurudishie fedha zako. Mambo ya kurudisha muamala uliokosewa imeaanza miaka ya karibu ru
 
Umesema kuwa muamala umetoka kwa wakala,sasa wakala akikosea mbona ni zoezi dogo tu anawasiliana na huduma kwa wateja
Sijui kama baada ya kukosea wakurudi kwa wakala au hawakurudi, mimi nilipigiwa simu na mhusika akiwa Chunya kuwa wamekosea kutuma hela na kunieleza lengo la hilo hela so niwarudishie.
 
We tunza meseji hiyo hela atairudisha tu.
Kwa kipindi hicho angelipa milioni kumi na sita ikiwa ni pamoja na riba!
Kuna watu wapuuzi hii dunia basi tu Uchungu nilionao Mungu ndo anajua [emoji24][emoji24]. Juzi tar 19/06/2023 Nilikua nalipia ticket yangu ya ndege off to Amsterdam muda wa booking ulikua unakaribia kuisha nimebakiza 5 minutes, fare yangu iwe cancelled nikatuma pesa mara 2, Jm travel services, muamala wa kwanza million 1 na laki 6, na wa 2 million 1 na laki 6, nimeshtuka yote imeenda message zilichelewa kurudi.

Nikapiga simu tigo nikawambia nimekosea kutuma mara 2 inatakiwa wakate muamala mmoja, imagine tigo wakathibisha miamala yote imefika kwa muhusika hawawezi kurudisha niwasiliane na Jm travel services.

Nikapiga simu nikatumiwa ticket yangu lakini muamala hawakurudisha na hapo ni jioni saa 10 na mimi Natakiwa kuondoka usiku saa 5 na KLM.

Nimepiga simu mpaka saa 2 usiku wanajibu kua wanashughulikia mpaka sasa sijapokea hela yangu, na sina uwezo wa kuwafikia jamaa namtafuta whatsp ni muhindi anasema wanashughulikia dah [emoji24][emoji24][emoji24].

Mungu yupo huyu muhindi japo sibagui watu ila nikirudi bongo ntamuwashia moto. Ndo akiba Nilikua nategemea inisaidie safarini lakini ameamua kunidhulumu sawa tu.

Note nina vielelezo vyote

Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:724726 Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 1,892,567. Muamala: 36246309377. 19/06/23 15:55.

Malipo JMD Travel Services yamekamilika, No. ya kampuni: 724726. Kiasi TSh 1,600,000. Kumbukumbu:BWTAZM Ada TSh 3,400. VAT TSh 519. Salio jipya TSh 289,167. Muamala: 86426520238. 19/06/23 15:56.
Ushauri wa bure, tafuta mwanasheria mpe 50000. Aandae barua awaandikie kua wa natakiwa kutudisha hiyo hela na unawapa siku 7
1. Warudishe hela ndani ya siku 7 bila riba
2. Warudishe hela baada ya siku 7 na riba maybe 300000 na gharama za Wakili 500000
3. Mwende mahakamani udai hela yako na riba na gharama za Wakili zote atakazoingia.
Hela utapata chap
 
Back
Top Bottom