Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Waalimu jamani shida snaaaa...yani kakodi boda kwendaa kutoa helaa isiyokuwa yakeee
Hapana mimi sio mwalimu ila ndivyo nilivyo ukikosea tu kunitumia kuanzia buku hata ufanye nini sikurudishii humu ndani musijifanye watakatifu wengi wenu mumewakopa tala na hamukulipa hadi leo je hiyo nayo sio dhulma? Hivi mimi na viongozi wa serikali wanaofisadi pesa ya umma tuna tofauti gani? Mimi na mzinifu tuna tofauti gani? Mimi na anaecheza kamari tuna tofauti gani? Mimi na ninyi munaokesha bar tunatofauti gani? Acheni unafiki
 
mwezi wa 4 mwaka huu nilituma 650,000 kimakosa-nimekuja kukumbuka dakika 5 zimekwisha jamaa amisha toa hela.dah niliumia sana
 
Mimi kuna mtu nilimuahidi kumchangia Harusi halafu sikumchangia... kiukweli roho iliniuma Sana kila ninapo kutana nae...
Kama ningejua ningemchangia tu...
Imeniumiza kuliko hela ambayo ningemchangia
Pole mkuu,chakufanya hiiyo hela uliyoplan kumpatia nunua zawadi ya mtoto kama tayari amepata mtoto kama bado nunua hata kitenge mpelekee.
 
22/8/2022 iliingia hela kimakosa kwenye Account ya KCB 765,000/= mpka Leo sijawahi tafutwa
 
Tatizo ukute unaludisha pesa kwa kigogo Fulani ,kumbe hio pesa ni ya mfuko wa shati Alikua anamtumia kimada ya kwenda club[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote.

Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650.

Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

NB: Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Karma is real
 
Mimi nisharudisha miamala mara 2, tena wa mara ya kwanza nilikuwa apeche alolo sina mia mbovu. Lakini yule niliyemrudishia kuna siku nyingine akaja kunitumia 18,000 akasema chukua hiyo mwanangu ile siku ulinisaidia sana.

Ila kuna tukio nilipiga utotoni linaniuma. Maza alikuwa anafanya kazi mbeya, wakati wa likizo alikuja home. Siku anataka kuondoka akanituma kijiji cha karibu nikachukue ulezi kwa mama fulani ili maza aende nao Mbeya kwa mtoto wa yule mama.
Nilipofika kwa yule mama akaniminia ulezi kwenye mfuko wa rambo nikaondoka na kibaiskeli changu.
Wakati narudi ule mfuko ukatoboka ukawa unamwaga ulezi, ikabidi nisimame ili kuweka sawa.

Ndugu zangu wakati naangalia vizuri kwenye tobo, nikakuta noti za 5000 nyingi. Ikabidi niufungue ule mfuko niupige sachi wote ili nipate hela zote. Baada ya kujiridhisha kuwa sijaacha kitu, nikaanza kurudi kwa mguu hadi mahali ulezi ulipoanza kumwagika ili kutafuta kama kuna hela ilidondoka.

Ile pesa kitu cha maana nilichofanya ni kulipa ada TZS 4000 tu mwaka 2000.
 
Haya mambo ya hela za mtandao mimi huwa nayaheshimu sana,hujui hiyo hela aliyetuma huko alikokusudia kutuma ilikuwa ikafanye kazi gani?je mgonjwa yupo mahututi?msiba au ada?

Mwaka 2003 kipindi hiko hakuna pesa za kwenye simu jamaa yangu mama yake alikuwa na historia ya maradhi ya mara kwa mara na ya ghafla so yeye ndiyo mkubwa akawa yupo town anatafuta maisha ndugu zake wapo Arusha,alikuwa mlinzi muajiriwa wa wanaokumbuka kampuni ya GOHA SECURITY hawa walikuwa Magomeni Mapipa,siku moja ikapigwa simu nipo nae ilikuwa jioni ya 16:00 mama ameumwa tena na inatakiwa haraka hela kwa ajili ya dawa na huduma nyinginezo.

Jamaa alikuwa na akiba yake Tsh 50,000/= so ikabidi anunue voucher za Voda kisha nduguze kule kijijini wa-make deal na muuza vocha na mpigisha simu wa kijiji vocha itumwe kwake awe anaiuza kwa kurusha then akate itakayomtosha baki wapewe wakamuhudumie mama yao,jamaa akakosea namba moja mtu yupo Kigoma aloo ilikuwa balaa.

To cut a long story jamaa alikataa kurudisha hela (zile vocha) huku ndugu wa jamaa wanapiga simu mama anakufa hospital wamekataa kumuhudumia ikabidi apige tena simu Kigoma kwa jamaa huku analia kama mtoto akimuomba arudishe japo kidogo maana hela ilikuwa ni kwa ajili ya matibabu ndiyo kidogo jamaa akawa na huruma akarudisha japo sikumbuki kama alirudisha hata 40K,hii ilituumiza hata sisi tuliokua nae kwa ile hali jamaa alikuwa anapitia na toka siku ile nilijifunza mengi sana hasa kuheshimu hisia za watu nisiowaona.

So kwa yeyote atakaesoma hapa ajue anaweza akawa sababu za kifo cha mtu tujifunze kutokula visivyotuhusu.(nimekazia sana kwenye suala la kifo kwa sababu ndiyo sehemu pekee isiyokuwa na option ya subira)
So sad mkuu inaumiza

Hii inatupa taswira kwanini watu mioyo imegeuka haina huruma unajiuliza kwanini kumbe vyanzo ni huku

Mtu kama huyu unafikiri atamuonea huruma mwizi anaepigwa? Au wale wa tuma kwenye namba hii? Jina fulani

Mara nyingine sio kuwa tumezaliwa na roho ngumu bali dunia inazikomaza roho
 
Uaminifu ni kitu muhimu sana kwenye maisha, wazungu wanaita "honesty"tatizo Ngozi nyeusi wengi wamekosa kitu hicho kutokana na malezi.
Hii kitu sijui source ni nini

Lakini malezi sidhani kama ni sababu ikumbukwe malezi ya western people ndio tunayoyaponda kwa kuwa ni mabovu na tabia chafu zinatoka kwao

Issue ya kuwa na credibility Africa tumeshindwa , nahisi ni mapokezi kutoka kwa waliotutangulia hata mifumo ya uongozi hatuongozwi na sheria ila sheria imewekwa kama kivuli cha kusingizia. Ukiingia kwenye uongozi unakuta watu wameweka mizizi imara ambayo huwezi kuitoa kirahisi na ukijaribu utakufa wewe
 
Mbona kama Chai, yaani Wakala akosee afu aanze sumbuka kukupigia?

Wakala akikosea anawahi kuwapigia wenye mtandao hela inazuiwa.
Huwezi jua mazingira ya mtumaji .Unaweza tuma hela ukiwa safarini au stendi unaendelea na safar Sasa wakala utampataje?
 
Back
Top Bottom