Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Nami kuna mtu namsaka mpaka kesho nimrejeshee pesa yake sijawahi kumpata, nilianzisha uzi humu hajatokea.
 
Hii dhambi 2015 niliikataa baada ya ndugu mmoja kutuma kimakosa kwenye line yangu ya airtel laki nane na hamsini elfu (850,000/=) kwa kumrudishia yote, japo nilikuwa juu ya mawe.
Wewe ni tajiri. Utajiri unaanzia rohoni baadae unakuja kwenye Vitu na umaskini nao ni hivyo hivyo.
 
Mimi ni mstaafu wa jeshi moja hapa nchini, niliwahi mrudishia mtu mmoja hela yake yote laki nane pamoja na ya kutolea niliongezea pale kibo complex

Sipendi dhuluma kabisa
Hongera sana wengi wanatamani wawe Kama wewe na wengi hawawezi generation hii Ina baadhi ya watu Wana tamaa sana
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote.

Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650.

Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

NB: Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Utu
 
Niliwahi kutuma hela kimakosa, hela dogo sana kimuonekano (16,000) lkn kubwa sana kimajukumu, ikapokelewa na hawa ndg zenu wa Kaskazini, nilimnasihi sana na kumweleza mazingira ya hela yenyewe huwezi amini akaniambia " unayo nyengine uniongezee aisee"
Nilichoka nikalazimika kutafuta nyengine.
Aisee huyo mtu daah
 
Mimi ni mstaafu wa jeshi moja hapa nchini, niliwahi mrudishia mtu mmoja hela yake yote laki nane pamoja na ya kutolea niliongezea pale kibo complex

Sipendi dhuluma kabisa
Unaweza kutuambia ilikuwa mwaka gani!?
 
Kuna jamaa niliwahi kumtumia hela ya Michango ya msiba kimakosa,jamaa baada ya kuzungumza akaniambia anaishi Manzese Dar es salaam na akasema atanirejeshea.

Kuepusha lawama msibani wasidhani pesa nimetumia ikabidi nikope niitume halafu mimi nibaki kupambania deni,yule jamaa hela hakuirudisha na nikawa nampigia simu ananiambia nisimsumbue,aiseee ile haikuwa kubwa sana lakini nilisema lazima nimshikishe jamaa adabu.

Unajua kuna watu huwa hawajali pesa wanayopoteza,tatizo huwa linakuja kwa wapokea pesa,huwa wanakera na kuudhi sana hata kama hujafikiria kufanya jambo baya inakubidi ufanye jambo ili heshima iwepo.

Yule jamaa mwanzo nilimwambia asiponirudishia hiyo hela kwenye akaunti yangu atajuta kuzaliwa akadhani utani,safari hii sikutaka kutumia nguvu za Kikurya,nilipanga nitumie nguvu za wenye uwezo mbadala.

Kufupisha,Jamaa alikuwa ananitafuta baada ya kumkarabati analia nikamwambia sina muda yeye aendelee kula matanuzi!.

Aiseee baada ya kubembelezwa sana ndugu zake na hii ni baada ya miezi 7 ndipo tukaonana pale Rombo Green View wakanirudishia hela yangu nikachafua zangu,ingawa walidai wanilipe fidia mimi nikakataa nikawaambia sihitaji dhuruma nahitaji pesa nilikosea kutuma!.

Jamaa hata kaa anisahau hadi anaingia kaburini na hiyo pia itakuwa imempa funzo!.


MIMI SEHEMU YA NGUVU HUWA NATUMIA NGUVU ILA SEHEMU YA WAJUBA HUWA NAWAACHA WAJUBA WAFANYE KAZI YAO!.
[emoji3] duh
 
Back
Top Bottom