Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Niliwahi kutuma hela kimakosa, hela dogo sana kimuonekano (16,000) lkn kubwa sana kimajukumu, ikapokelewa na hawa ndg zenu wa Kaskazini, nilimnasihi sana na kumweleza mazingira ya hela yenyewe huwezi amini akaniambia " unayo nyengine uniongezee aisee"
Nilichoka nikalazimika kutafuta nyengine.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
iliwahi kunitokea hiyo mwaka 2011 meseji imeingia kucheki laki 7 imeingia na ukifikiria sikuwa na kitu mfukoni aisee nilikodi bodaboda kwenda kijiji cha jirani kuitoa pesa njiani akawa ananipigia nikamwambia nipo barabarani nikifika nakurudishia hela yako ondoa shaka nilipofika kwa wakala nikaichomoa yote
[emoji23] kmmqe
 
Mwaka 2014 kuna jamaa alituma kwangu laki tisa na 80 kimakosa. Baada ya kama dakika kumi akapiga nikamrudishia laki tisa na 50 nilimwambia nilikuwa na deni la elfu kumi na tano songesha wamekata halafu na Mimi ninakukata sh elfu kumi na tano ili next time usiwe mzembe tena jamaa alicheka hatari anyway nilimkata.
 
Uaminifu ni kitu muhimu na una baraka zake.
Sadaka: Juzi niliona bibi kakaa barabarani kajikunyata nikamfuata vipi mbona hupandi gari akasema anasubiri walipwe hela ya kibarua buku nne ya kufagia barabara ilibaki nusu nilie. Nikampa elf 20. Siku hiyo jioni yake nikapata hiyo mara 30. Niliconnect.
Hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
 
Kuna jamaa niliwahi kumtumia hela ya Michango ya msiba kimakosa,jamaa baada ya kuzungumza akaniambia anaishi Manzese Dar es salaam na akasema atanirejeshea.

Kuepusha lawama msibani wasidhani pesa nimetumia ikabidi nikope niitume halafu mimi nibaki kupambania deni,yule jamaa hela hakuirudisha na nikawa nampigia simu ananiambia nisimsumbue,aiseee ile haikuwa kubwa sana lakini nilisema lazima nimshikishe jamaa adabu.

Unajua kuna watu huwa hawajali pesa wanayopoteza,tatizo huwa linakuja kwa wapokea pesa,huwa wanakera na kuudhi sana hata kama hujafikiria kufanya jambo baya inakubidi ufanye jambo ili heshima iwepo.

Yule jamaa mwanzo nilimwambia asiponirudishia hiyo hela kwenye akaunti yangu atajuta kuzaliwa akadhani utani,safari hii sikutaka kutumia nguvu za Kikurya,nilipanga nitumie nguvu za wenye uwezo mbadala.

Kufupisha,Jamaa alikuwa ananitafuta baada ya kumkarabati analia nikamwambia sina muda yeye aendelee kula matanuzi!.

Aiseee baada ya kubembelezwa sana ndugu zake na hii ni baada ya miezi 7 ndipo tukaonana pale Rombo Green View wakanirudishia hela yangu nikachafua zangu,ingawa walidai wanilipe fidia mimi nikakataa nikawaambia sihitaji dhuruma nahitaji pesa nilikosea kutuma!.

Jamaa hata kaa anisahau hadi anaingia kaburini na hiyo pia itakuwa imempa funzo!.


MIMI SEHEMU YA NGUVU HUWA NATUMIA NGUVU ILA SEHEMU YA WAJUBA HUWA NAWAACHA WAJUBA WAFANYE KAZI YAO!.
Hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
 
2020 nilikosea kumtumia mtu 206,000. Ilikuwa ni malipo ya hela ya Chakula cha vibarua kwenye site yangu.

Nilikuwa busy kidogo, ilipofika tu jamaa niliyemtumia hela akapiga. Nikamuandikia ujumbe kuwa tayari nimeshatuma. Niliamini ni fundi anauliza. Jamaa, akaniandikia pokea mara moja.

Akapiga lakini niligundua si sauti ya fundi. Akaniambia kuna fedha nimemtumia ila anaomba asirudishe. Nilipanick kidogo, jamaa akanielezea story ya magumu anayopitia. Anaomba sana nimuachie kiasi kile cha hela. Akaniambia kama sitaridhia atarudisha kiasi hicho punde baada ya kukata simu.

Lakini kwa magumu yale, niliridhia kumuachia kiasi hicho cha pesa. Ukweli ni kuwa niliokoa maisha ya mwanae. Na maombi yake yalijibiwa kupitia mimi. Nilifanya alternative nyingine kuwesesha kule site.

Jioni nilipata dili zuri mno. Nikajua tu ni Mungu ananilipa kwa Sadaka yangu ya asubuhi.
Hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote.

Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650.

Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

NB: Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Kuna watu ambao hawadhulumiwi/ibiwi
 
mtu mweusi kaumbwa na roho mbaya sana tena sana. sijui ndo laana. yani haaminiki kamwe!

hata hawa wanaodai wamerudishia watu ela izo ni porojo tu. na huyu anayetafuta mtu ampe ela unaeza kuta keshaona mambo yake yote yanagota kaamua ajisalimishe. nyambaff mkubwa.
 
Mimi ukikosea kutuma kwangu hata sikurudishii kwanza ikiingia tu nanunua bando la 2000 tu hapo hata iweje watu wa mtandao hawawezi kuizuia tena
 
mtu mweusi kaumbwa na roho mbaya sana tena sana. sijui ndo laana. yani haaminiki kamwe!

hata hawa wanaodai wamerudishia watu ela izo ni porojo tu. na huyu anayetafuta mtu ampe ela unaeza kuta keshaona mambo yake yote yanagota kaamua ajisalimishe. nyambaff mkubwa.
Mimi niwe mkweli ukikosea tu imekula kwako
 
Nilikoseaga kutuma laki 8, bahati alipokea mstaafu wa Jeshi la magereza ni mtu mzito sana, kesho yake alinipa yoote pale kibo complex, imagine alitoka Gongo la mboto kwaajili yangu.
Huyo muhuri tu,kwa nini asingekurushia kwa simu?
 
Kuna siku ilinitokea mm nikatuma hela kimakosa ikaenda kwa jamaa yupo ukerewe,na ilikua laki nane ila jamaa alikua mwema akaludisha nilimshukuru sana nilitaka nimlipe kidogo aka kataa kabisa Mungu ampe maisha malefu huko aliko.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Rafiki yangu alitumiwa pesa kimakosa kwenye no. yake ya mpesa inayoishia na 8650. Baada ya kutumiwa hiyo hela huyo rafiki yangu aliitoa yote.

Alipigiwa na aliyekosea mwamala akamrudishia elf 50 Kwa ahadi ya kulipa kilichobaki ila aliposhindwa aliacha kutumia hiyo no yake inayoishia na 8650.

Kama unaijua story hii jamaa anakutafuta aombe msamaha na kukulipa ukikubaliana maana anasema jambo hili linamtesa sana.

NB: Jamaa alikua anamtumia pesa wife wake. Ataje kiasi na mkoa aliotoka maana ni vitu anavikumbuka. Asanteni.
Tayari watu washafanya yao, unapigwa udizungwa moja mashetani yanakufukuzia km inzi wameona kinyesi
 
Ni mm ila nlikuwa namtumia ya alikuwa mjamzito wa mapacha .mimba ilitoka na akafariki nikafukuzwa kazi kwa kuwa watoto 3 walipaswa niwalee .ila sikusamehi we jiendee motoni kaenjoy na kina hitler
 
Back
Top Bottom