Mungu anisamehe sana inawezakana ndo mana ridhiki zangu haziji
Watu walishawahi kosea kwangu =
150,000
95,000
80,000
Hizi 50,000 na zaidi ya mara 4
Sikuwahi kurudisha hata mia nliishia kuwablock
daah kuna mtu nakumbuka nilkosea kutuma hela kwakwe sh 52,000 ilikuwa namtumia mchepuko, nikapiga huduma kwa wateja kwasababu ile no ilikuwa Mtandao tofaut na mm.
niliambiwa nisubili masaa 72, ilikuwa jmos basi nikampigia yule jamaa nikamwambia nikosea kutuma hela kwakwe aniludishie walau 30,000 tuh, jamaa kweli akarudisha 30,000 nikamshukuru.
Nimekaa j3 sina mpango wowote naona messag ya muhamala unaiangia kwenye simu yangu hela imerudishwa, walah sikulemba nikaihamisha ile hela jamaa alipiga mara 3 sikupokea ila hakupiga tena