Rafiki yangu alivyonishika mkono hadi kufanikiwa

Yeye muanzisha maada ndio mwenye rafiki mchaga kafanikisha jamaa kutoboa, mimi yule mbwa ni mgogo hajielewi kila saa anashauri tukapige tungi hatuna cha duka wala genge mpuuzi sana yule
Nimecheka sana 😂😂😂 si umpunguze tu mkuu? Na wee utakua unapenda mtungi
 
Afadhali wewe nina rafiki Mgogo wa kongwa hana msaada wowote wala hana ushauri wa maisha nataka nitemane naye mbwa yule hajielewi pumbavu zake
Je nawewe una msaada kwake? Au wewe unataka upewe misaada tu kutoka kwake?
 
Sio kila uaridi utanukia ushawahi kuwa na rafiki mwarabu mwenye hela hao jamaa kiboko hawanaga msaada kwa mswahili labda uwe Mwarabu mwenzake.
Siyo kweli! Usihukumu usichokijua kama yalikutokea ni wewe siyo wote.
Acha chuki tafuta pesa tu.
 
Wanajukwaaa wazima nyie.

Kiasili mimi ni mzaliwa kutoka Nyanda za Juu Kusini ndani ya Mkoa flani hivi. Elimu yangu niliipata mkoa wa Kaskazini (Kilimanjaro) kuanzia kidato cha pili hadi Chuo nilisoma kule baada ya maza kupata kazi Kilimanjaro

Nilibahatika kupata Rafiki yangu ambaye amekuwa kama ndugu likizo nilikuwa naenda kwao. Jamaa alikuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani baada ya wazazi wake kuhamia Dar-es- Saalam kwao walikuwa wamejenga sana

Likizo fulani nilimualika kwetu akaja, jamaa alishangaa sana Nyumba yetu ilivyokuwa (Low quality) alinichana palepale tukiwa nae kwamba natakiwa nikifanikiwa nijenge Nyumbani na mji wangu

Baada ya kidato cha sita matokeo kutoka tulipata chuo kimoja pale Moshi. Tulivyomaliza mimi nilienda Arusha yeye akaenda Dar-es-Salaa. Baada ya kupotezana miaka miwili nilifanikiwa kukutana nae Dar-es-Salaam, jamaa alikuwa anapush Toyota Harrier ila alinidanganya la Mzee wake.

Jamaa alinipeleka Kimara mtaani kwao alikuwa na maduka mawili ya kwake nilichoka sana miaka miwili amewezaje. Kesho yake akanipeleka Kariakoo nilichoka maduka wanayo matatu moja la Baba yake moja lake moja la viatu vya kike la Dada yake.

Nilipata kuongea na Baba yake nikamweleza mambo yangu ikiwepo suala la kuoa akanishauri nilifute mara moja kwakuwa sijasimama kiuchumi, akanishauri nisirudi mkoa nibaki Dar kukimbizana na mishemishe kweli Baba yule alinipa chumba ndani ya nyumba yao pale Kimara ikawa asubuhi ni kuamka kwenda Kariakoo kukimbizana

Alikuwa ananishauri sana ndani ya mwaka mmoja nihakikishe nimesimama mwenyewe kwani uwezo ninao kwenye biashara nilikuwa sina uzoefu ila kila siku tukirudi home lazima yule mzee aniite tupige hesabu nimepata sh ngapi, kwa siku tukawa na daftari kama tatu moja la kuanzisha duka langu, moja la kununua Kiwanja, moja la kuanza ujenzi

Niliishi maisha ya kutokula bata na ubahili yule mzee alikuwa anatutoa weekend tu maisha yalikuwa magumu nilikuwa nakula kwa macho pisi kali za Kariakoo

Baada ya Miaka miwili nimesimama na nimeanza Ujenzi huku nina Maduka mawili. Hakika ndugu yangu Kimaro umenitoa mbali🙏🏿🙏🏿
Hongera sana. Watu waliofanikiwa ni kama kitabu chenye kurasa nyingi na tamu kuwasoma huna budi. Kipindi fulani nilikuwa napitia changamoto nyingi za kifedha, nikawa naongea na tajiri mmoja akasema "JIFUNZE KUIHESHIMU PESA, KWANGU MIMI HAKUNA PESA KUBWA WALA NDOGO". Kuanzia hapo, financially nikaanza kubadilika. Kwenye kitu pesa, DISCIPLINE ni muhimu Sana.
 
Afadhali wewe nina rafiki Mgogo wa kongwa hana msaada wowote wala hana ushauri wa maisha nataka nitemane naye mbwa yule hajielewi pumbavu zake
Wagogo akili zao acha kabisa.
 
2020 miaka miwili nyuma alikuwa na dili za asali ,mara alikuwa jela .huo mda kapata wapi? Naona vijana mnajitekenya kwamba mna roho nzuri ila behind sio kweli.
Kumbuka ile safari yako ya Arusha kwenda Moshi sijui ,wewe ni mtu wa Arusha sijui jambazi ambaye ulishwai kufungwa ,sasa unaleta porojo.

Ooohoooo mafaili yameanza kufukuliwa.
 
Kitu kibwa sana tunachokikosa sisi vijana wa kiume ni kuwa na wazee wa kiume wenye mafanikio wanaotusimamia mwanzo mwisho wengi wa wazee hawa wamefariki vijana tumebaki tunajitafutia tu maisha bila miongozo.

Pia Kuna umuhimu mkubwa sana haya maisha kuwa na mentors wenye mafanikio.

Pia hongera kwa kupata famili friend wanaokupenda.
Mentors wenyewe sasa anataka akugeuze punda akiona unaanza kuimarika anaingiwa na husuda hataki uondoke anataka uendelee kuwa chini yake akutumie kwa faida yake maana ukiondoka atakosa jembe wa kumtuma.

Mzazi wako hawezi kuwa hivyo atataka utoboe akijua utakuja kuwa msaada wake. Sasa shida ndipo ipo hapo.
 
Wanajukwaaa wazima nyie.

Kiasili mimi ni mzaliwa kutoka Nyanda za Juu Kusini ndani ya Mkoa flani hivi. Elimu yangu niliipata mkoa wa Kaskazini (Kilimanjaro) kuanzia kidato cha pili hadi Chuo nilisoma kule baada ya maza kupata kazi Kilimanjaro

Nilibahatika kupata Rafiki yangu ambaye amekuwa kama ndugu likizo nilikuwa naenda kwao. Jamaa alikuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani baada ya wazazi wake kuhamia Dar-es- Saalam kwao walikuwa wamejenga sana

Likizo fulani nilimualika kwetu akaja, jamaa alishangaa sana Nyumba yetu ilivyokuwa (Low quality) alinichana palepale tukiwa nae kwamba natakiwa nikifanikiwa nijenge Nyumbani na mji wangu

Baada ya kidato cha sita matokeo kutoka tulipata chuo kimoja pale Moshi. Tulivyomaliza mimi nilienda Arusha yeye akaenda Dar-es-Salaa. Baada ya kupotezana miaka miwili nilifanikiwa kukutana nae Dar-es-Salaam, jamaa alikuwa anapush Toyota Harrier ila alinidanganya la Mzee wake.

Jamaa alinipeleka Kimara mtaani kwao alikuwa na maduka mawili ya kwake nilichoka sana miaka miwili amewezaje. Kesho yake akanipeleka Kariakoo nilichoka maduka wanayo matatu moja la Baba yake moja lake moja la viatu vya kike la Dada yake.

Nilipata kuongea na Baba yake nikamweleza mambo yangu ikiwepo suala la kuoa akanishauri nilifute mara moja kwakuwa sijasimama kiuchumi, akanishauri nisirudi mkoa nibaki Dar kukimbizana na mishemishe kweli Baba yule alinipa chumba ndani ya nyumba yao pale Kimara ikawa asubuhi ni kuamka kwenda Kariakoo kukimbizana

Alikuwa ananishauri sana ndani ya mwaka mmoja nihakikishe nimesimama mwenyewe kwani uwezo ninao kwenye biashara nilikuwa sina uzoefu ila kila siku tukirudi home lazima yule mzee aniite tupige hesabu nimepata sh ngapi, kwa siku tukawa na daftari kama tatu moja la kuanzisha duka langu, moja la kununua Kiwanja, moja la kuanza ujenzi

Niliishi maisha ya kutokula bata na ubahili yule mzee alikuwa anatutoa weekend tu maisha yalikuwa magumu nilikuwa nakula kwa macho pisi kali za Kariakoo

Baada ya Miaka miwili nimesimama na nimeanza Ujenzi huku nina Maduka mawili. Hakika ndugu yangu Kimaro umenitoa mbali🙏🏿🙏🏿
Inabidi ukaoe kwenye ukoo huo huo upate mbegu za biashara.
 
Back
Top Bottom