Rafiki yangu amezaa na mke wa mtu

Rafiki yangu amezaa na mke wa mtu

Habari zenu waungwana,
Rafiki yangu anaomba ushauri, Kwa kifupi ilitokea akawa na mahusiano na mke wa mtu, kwa maelezo yake anasema Mara ya kwanza Kushiriki tendo mwanamke alinasa ujauzito.

Baada ya mwanamke kujifungua mtoto mzuri wa kike ikawa jamaa anaulizia maendeleo ya mtoto anapewa ushirikiano kama kawaida, Wakati huo Mume wa huyo mwanamke hajui kama mtoto si wake,

Jamaa alimwambia mwanamke kwa kuwa imetokea wamezaa ili kuepusha hatari kwake na kwa mtoto wapunguze kuwasiliana na wavunje mahusiano abaki na jambo moja tu la kumhudumia mtoto japo kwa siri,

mwanamke akamwambia jamaa kama anahitaji kuendelea kupata taarifa za mtoto basi waendelee na mahusiano, mwanamke hataki habari ya kuvunja mahusiano, Jamaa anakiri ni kweli alifanya kosa kubwa na hata nafsi yake inamsuta. Mshaurini huyu jamaa yangu kwani yuko njia panda.
Kuna watu jasiri. Kama ni kweli, maana porojo pia zipo za namna hii
 
Pole!

Sasa mpaka huu mkasa unaletwa hapa, maana wewe na huyo jamaa yako mmeona kuna tatizo, na tatizo lenyewe amezaa na mke wa mtu na wote mnakiri hivyo.

Sasa mnataka ushauri wa kazi gani ikiwa nyote watatu mke, jamaa, na wewe mnahisi siyo sawa?

Hapa mnataka majibu gani?

Anyway, kitanda hakizai haramu, kisheria mtoto siyo wa jamaa bali ni wa mwenye mke.

Huyo mwanamke atumie nafasi yake kama mama kwamba ajuaye baba wa mtoto ni yeye, na hivyo ampe mumewe mtoto na mtoto atambulishwe kwa baba mlezi.

Siku zote ndiyo maana baba huitwa Baba Mlezi na Mama ni mzazi.

Kama jamaa kapanda mbegu shamba si lake basi mazao si yake; kama ana kiherehere lolote limkute; mke wa mtu sumu!
Story za jf si za kuziamini zote, soma kwa macho matatu.
 
Habari zenu waungwana,
Rafiki yangu anaomba ushauri, Kwa kifupi ilitokea akawa na mahusiano na mke wa mtu, kwa maelezo yake anasema Mara ya kwanza Kushiriki tendo mwanamke alinasa ujauzito.

Baada ya mwanamke kujifungua mtoto mzuri wa kike ikawa jamaa anaulizia maendeleo ya mtoto anapewa ushirikiano kama kawaida, Wakati huo Mume wa huyo mwanamke hajui kama mtoto si wake,

Jamaa alimwambia mwanamke kwa kuwa imetokea wamezaa ili kuepusha hatari kwake na kwa mtoto wapunguze kuwasiliana na wavunje mahusiano abaki na jambo moja tu la kumhudumia mtoto japo kwa siri,

mwanamke akamwambia jamaa kama anahitaji kuendelea kupata taarifa za mtoto basi waendelee na mahusiano, mwanamke hataki habari ya kuvunja mahusiano, Jamaa anakiri ni kweli alifanya kosa kubwa na hata nafsi yake inamsuta. Mshaurini huyu jamaa yangu kwani yuko njia panda.
jamaa mwenyewe si ni wewe
 
Back
Top Bottom