Rafiki yangu anatafuta Mwanamke mwenye sifa zifuatazo

Sawa kma ni hivo but Kuna familia ni ngumu kukubaliana na Hilo suala
Naongea kwa experience ni rahis wapenz mnapokubaliana mkiwa wawili mmekumbatiana Sasa nendeni huko mbele ndo tatizo maswali Huwa mengi sana

Unamaanisha wazazi wa pande zote mbili kuingilia na kukataa.?

Ni Kijana mjinga ambae anaweza kuamini ukioa musilam au mkiristu utafanikiwa katika ndoa .


Swala la dini halina umuhimu na nafasi Kwa watu wanaojitambua.

Maana binadamu anabidi kuwa karibu na Mungu na sio dini.
 
How unakuwa karibu Mungu bila dini?
 
Hiv mnaotafuta dini yoyote Huwa mnaujasiri wa namna ipi,mbona ni suala gumu sana mkifika hatua ya kufunga ndoa Yani Huwa ni kasheshe sana au mm tu uwezo wangu wa kufikiri
Mmoja anamfuata mwenzake

Kwa sisi tusio na dini hali ndo mbaya zaidi
 
How unakuwa karibu Mungu bila dini?
Dini ni njia ya kukupeleka Kwa Mungu Ila unaweza kwenda Kwa Mungu bila dini yoyote .


Watu wengi hasa waafrica wapo karibu na Dini Ila hawapo karibu na Mungu

Mtu aliyekaribu na Mungu ni wachache sana.

So mtu akitumia kigezo cha dini kuoa au kuolewa anakuwa bado hajitambui na hana ufahamu kuhusu maswala ya kiroho .
 
Kufunga ndoa tunatafuta kibali Kwa Mungu kujiepusha na dhambi ya uzinifu
Dini tofaut ndoa mnafungaje mnaweza kuwa karibu na Mungu kiroho na mnazini?
 
Shida unagoma kuelewa kwamba afrika kuna miungu miwili; Yahweh na Allah.

Watu wanasemaga kiunafki mungu ni mmoja ila ikifika kwenye masuala kama ndoa ndo tunajua ukweli
 
Shida unagoma kuelewa kwamba afrika kuna miungu miwili; Yahweh na Allah.

Watu wanasemaga kiunafki mungu ni mmoja ila ikifika kwenye masuala kama ndoa ndo tunajua ukweli
Bora wew umesema ukweli ni rahis kuongea ikiwa unauhitaji ila ukija uhalisia wengi tunaangukia pua
Africa udini ni mwingi hasa ngazi ya familia tunamezeshwa mambo had unamuona asie wa dini Yako km adui
 
Kufunga ndoa tunatafuta kibali Kwa Mungu kujiepusha na dhambi ya uzinifu
Dini tofaut ndoa mnafungaje mnaweza kuwa karibu na Mungu kiroho na mnazini?

Kuzini ni kuwa unalala na wanawake au wanaume tofauti tofauti ambao haupo katika muunganiko nao (bond)

Ukipata mwanamke /mwanaume unachofanya unatulia nae na kufanya nae muunganiko wa kiroho kupitia maneno , hapo ndo kibali hutokea.

Ikiwa mme wako au mke wako anatoka dini tofauti , ndoa inaweza kufungwa either kanisani au msikitini au serikalini au Kwa wazee wa mila .

Baada ya hapo kila mtu ataendelea na kusali sehemu anayoamini inamfungamanisha na nguvu yake ya juu (higher power )
 
Muunganiko kimaneno Tena ndo nn?
 
Muunganiko kimaneno Tena ndo nn?

Mambo ya kiroho mkuu bado haujayaelewa vizuri .

Ukiwa enlightenment you will understand ulimwemgu wa roho .

Kwa sasa Bado hautaweza kuelewa Ila kinachoendesha ulimwengu wa roho ulimwengu wa roho ni maneno /neno na sio dini
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…