Rafiki yangu anawaza kuvunja ndoa, lakini nyumba yake alijenga kwenye kiwanja cha wakwe, afanye nini?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu

Nina rafiki yangu ambaye baada ya kuoa, miaka takribani sita baadaye alibahatika kupata watoto wawili, ambapo yeye na mkewe walipewa uhuru wa kuchagua eneo katika kiwanja cha wakwe upande wa Mwanamke na kujenga nyumba yao, baada ya nyumba kukamilika na kuhamia hapo, migogoro ilianza na hali hiyo imemuumiza sana kisaikolojia.

Baada ya kuona maisha ya ndoa yamebadilika na kuwa machungu, sasa hatamani tena ndona na anawaza kuvunja ndoa hiyo, lakini anapokumbuka kuwa nyumba yake ambayo alitumia gharama kubwa sana mpaka ikakamilika, imejengwa kwenye kiwanja cha wakwe, na hajui afanye nini kuhusu mali hiyo.

Mbaya zaidi nyaraka zote zinasoma majina ya wakwe zake, yaani hali hiyo ndiyo imezidi kumchanganya zaidi.
 
Wakuu

Nina rafiki yangu ambaye baada ya kuoa, miaka takribani sita baadaye alibahatika kupata watoto wawili, ambapo yeye na mkewe walipewa uhuru wa kuchagua eneo katika kiwanja cha wakwe upande wa Mwanamke na kujenga nyumba yao, baada ya nyumba kukamilika na kuhamia hapo, migogoro ilianza na hali hiyo imemuumiza sana kisaikolojia.

Baada ya kuona maisha ya ndoa yamebadilika na kuwa machungu, sasa hatamani tena ndona na anawaza kuvunja ndoa hiyo, lakini anapokumbuka kuwa nyumba yake ambayo alitumia gharama kubwa sana mpaka ikakamilika, imejengwa kwenye kiwanja cha wakwe, na hajui afanye nini kuhusu mali hiyo.
Kati ya nyumba na amani yake kipi cha muhimu? Unapoamua kubomoa lazima uingie gharama. Nyumba awaachie watoto ajenge nyingine.
 
Back
Top Bottom