Rafiki yangu anawaza kuvunja ndoa, lakini nyumba yake alijenga kwenye kiwanja cha wakwe, afanye nini?

Rafiki yangu anawaza kuvunja ndoa, lakini nyumba yake alijenga kwenye kiwanja cha wakwe, afanye nini?

Kisheria hili haliwezekani kwasababu kuna watoto ambao wao hawahusiki na ugomvi wao. Na sheria inalinda sana haki za watoto. Yaani hapo jamaa akubali tu ugenini kufungwa 2-0.
Kiwanja ni cha wakwe, na wakwe siyo wazazi wa hao watoto kisheria. Mahakama haiwezi kuwazalishia wakwe jukumu la kulea watoto wa mtu mwingine, ndio maana suluhisho la kisheria ni mume kufidiwa fedha zake ili kila mtu aendelee na maisha yake.
 
Ni kheri achukue mkopo asepe mana akiacha NYUMBA kesho ataletwamo mwanaume mwingine
Mkopo bank watakupatia bila kuwakabidhi dhamana ya hati (tittle deed)?

Na kama atakuwa na hati, basi hilo jambo ni jepesi na si la kuumiza kichwa.

Lakini nionavyo mimi, hana hati huyo na pale alipo ashafanywa kama dume la mbegu lililoazimwa kwenda kuzalisha kwa jirani na likimaliza jukumu lililolipeleka halitahitajika tena hapo na watoto atakaozalisha wanakuwa si mali yake.
 
Mimi nime comment vile makusudi kwa sababu huyo mwanaume anaonekana hana pesa, mtu kama huyo anapaswa kupewa ushauri gani Seran?
Nashangaa hapa wanajiongelesha ujinga, wakati so far hiyo nyumba iko kwenye mgogoro huwezi kukurupuka tu ukachukua mkopo, anahisi benki kuna mtahira yanagawa tu pesa! Mikopo inapitishwa kisheria na mawakili.. kiwanja sio chako unauzaje au kukopaje kwa nyaraka/hati zisizo na jina lako? Akili hazipo kabisa hapa!
 
Kwa busara ya kawaida anatakiwa afanye yafuatayo.
Kwanza ate atemane na wazo la kuvunja nyumba, kwasababu kama ni kukosea alisha kosea mwanzoni.
Pili asielekeze hasira za maumivu yake ya ndoa kwenye mali na vitu.
Kwakua tayari wamezaa, basi nivyede akajikataa kisha akaanze maisha mapya maana hajachelewa.
 
Nashangaa hapa wanajiongelesha ujinga, wakati so far hiyo nyumba iko kwenye mgogoro huwezi kukurupuka tu ukachukua mkopo, anahisi benki kuna mtahira yanagawa tu pesa! Mikopo inapitishwa kisheria na mawakili.. kiwanja sio chako unauzaje au kukopaje kwa nyaraka/hati zisizo na jina lako? Akili hazipo kabisa hapa!
Haya mambo yanafurahisha sana muda mwingine.
 
Haya mambo yanafurahisha sana muda mwingine.
Watu wengi huwa wanasolve mambo yao kwa kukomoa/kukurupuka na kutumia hasira badala ya kutumia akili!

Unamkomesha mtu kwasababu mmeshindwana, hujui kuwa sio lazima uelewane na kila mtu kwenye hii dunia, yaani mtu asiyetaka kukubali ukweli na anatumia hasira kwenye kufanya maamuzi, hawezi kufanikiwa mambo mengi ataishia kujiona anaonewa tu kila anakokwenda!
 
Nakuuliza juu ya watoto wasiohusika na ujinga wa wanandoa wanawekwa upande wa nani? Au wanagawiwa chao mapema?
Kisheria, watoto hawana haki ya kumiliki mali ya wazazi wao mpaka wazazi watakapofariki.

Sana mahakama huwa inaangalia tu ustawi wa mtoto, chini ya miaka 7, sheria inapendekeza mama ndiye abaki na watoto.
 
Sawa, kwahiyo mama atawapeleka wapi kama baba anavunja au kukopea nyumba?
 
Back
Top Bottom