Rafiki yangu anawaza kuvunja ndoa, lakini nyumba yake alijenga kwenye kiwanja cha wakwe, afanye nini?

Watu wengi huwa wanasolve mambo yao kwa kukomoa/kukurupuka na kutumia hasira badala ya kutumia akili!

Unamkomesha mtu kwasababu mmeshindwana, hujui kuwa sio lazima uelewane na kila mtu kwenye hii dunia, yaani mtu asiyetaka kukubali ukweli na anatumia hasira kwenye kufanya maamuzi, hawezi kufanikiwa mambo mengi ataishia kujiona anaonewa tu kila anakokwenda!
You nailed it, huko ni kushindwa kutofautisha kati ya kutafuta haki na kutafuta kulipa kisasi.
 
Atafute hati kama hana au ahamishe umiliki kutoka kwa baba mkwe, wakiachana wanagawana
 
Sawa, kwahiyo mama atawapeleka wapi kama baba anavunja au kukopea nyumba?
Kiwanja ni cha wakwe, Benki inapoamua kutoa mkopo huwa inaangalia hati ya kiwanja kwa sababu kiwanja kipo kisheria chini ya jina la wakwe, mume hawezi kisheria kuchukua hati ya mtu mwingine na kwenda kukopea benki bila wamiliki wa ardhi kuhusika na kusaini kama wadhamini.

Kwenye hii situation nilicho kielewa mimi ni kwamba, Mume anachodai ni financial compensation. Nyumba inaweza kubaki hapo hapo, mama na watoto wakaendelea kuishi, lakini mke na wazazi wake watalazimika kumpa mume kiasi fulani cha fedha ili kufidia jasho lake.
 
Amwachie mume watoto, yeye akajenge yake au aende kuishi kwa wazazi wake. Tupo kwenye ulimwengu wa haki sawa. Anachokifanya mwanaume mwanamke anaweza kukifanya kwa ubora zaidi
Anayetaka kuondoka ni yeye kwanini mwanamke aondoke? Aondoke yeye akajenge upya kama anashindwa kusolve matatizo yake ya ndoa!
 
Kiwanja ni cha wakwe, Benki inapoamua kutoa mkopo huwa inaangalia hati ya kiwanja kwa sababu kiwanja kipo kisheria chini ya jina la wakwe, mume hawezi kisheria kuchukua hati ya mtu mwingine na kwenda kukopea benki bila wamiliki wa ardhi kuhusika na kusaini kama wadhamini.

Kwenye hii situation nilicho kielewa mimi ni kwamba, Mume anachodai ni financial compensation. Nyumba inaweza kubaki hapo hapo, mama na watoto wakaendelea kuishi, lakini mke na wazazi wake watalazimika kumpa mume kiasi fulani cha fedha ili kufidia jasho lake.
Alijenga kwaajili ya familia yake, amechoka mwenyewe anataka kuondoka, wakwe hawawezi kumlipa pesa yoyote ile akajitafute upya mjinga kabisa!
 
Wakuu

Nina rafiki yangu ambaye baada ya kuoa, miaka takribani sita baadaye alibahatika kupata watoto wawili, ambapo yeye na mkewe walipewa uhuru wa kuchagua eneo katika kiwanja cha wakwe upande wa Mwanamke na kujenga nyumba yao, baada ya nyumba kukamilika na kuhamia hapo, migogoro ilianza na hali hiyo imemuumiza sana kisaikolojia.

Baada ya kuona maisha ya ndoa yamebadilika na kuwa machungu, sasa hatamani tena ndona na anawaza kuvunja ndoa hiyo, lakini anapokumbuka kuwa nyumba yake ambayo alitumia gharama kubwa sana mpaka ikakamilika, imejengwa kwenye kiwanja cha wakwe, na hajui afanye nini kuhusu mali hiyo.

Mbaya zaidi nyaraka zote zinasoma majina ya wakwe zake, yaani hali hiyo ndiyo imezidi kumchanganya zaidi.
Avunje kwanza hiyo nyumba aliyoijenga kwenye kiwanja cha wakwe zake
 
Alichokiungasha Bwana Mwanadamu hapaswi kukitenganisha.
Anachopaswa kufanya ni kuangalia namna gani anaweza kuinusuru ndoa yake.

Nyumba ajenge kwa gharama zake halafu akubali nyaraka zisome majina ya wakwe?

Hakuna kubomoa nyumba awaachie wakwe zake, akaanze maisha kwingine, hakuui kuanzia chini kwa mara nyingine.
 
Avunje na nyumba.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Alijenga kwaajili ya familia yake, amechoka mwenyewe anataka kuondoka, wakwe hawawezi kumlipa pesa yoyote ile akajitafute upya mjinga kabisa!
Angekuwa na akili inayoona mbali, asingethubutu kabisa kufanya ujinga wa aina hiyo.

Huwezi kuwa na pesa zako ukakubali kwenda kujenga kwa wakwe aisee, hili suala hata ukilifikiria kwa akili ya kawaida tu unaona kabisa haijakaa vizuri.

Kwa sasa atalazimika tu kukubali matokeo kama wakwe wakiamua kumkazia, hamna namna.
 
Anayetaka kuondoka ni yeye kwanini mwanamke aondoke? Aondoke yeye akajenge upya kama anashindwa kusolve matatizo yake ya ndoa!
Yeye ndie alijenga nyumba, ana haki ya kuivunja. Huyo mwanamke anaetaka kubaki ndio anatakiwa kujenga yake. Maana kiwanja kitakuwepo
 
Kiwanja ni cha wakwe, na wakwe siyo wazazi wa hao watoto kisheria. Mahakama haiwezi kuwazalishia wakwe jukumu la kulea watoto wa mtu mwingine, ndio maana suluhisho la kisheria ni mume kufidiwa fedha zake ili kila mtu aendelee na maisha yake.
Wakwe hawawezi kukataa wajukuu zao, sana sana hapo sheria itaangalia kipato cha baba mtu; watafanya tathmini kiasi cha pesa atakacholipa kama child support. Mwanaume hapo unaanza safari upya. Yaani hapo jamaa hatoki. Sheria imeegemea upande wa wakwe.
 
Wakuu

Nina rafiki yangu ambaye baada ya kuoa, miaka takribani sita baadaye alibahatika kupata watoto wawili, ambapo yeye na mkewe walipewa uhuru wa kuchagua eneo katika kiwanja cha wakwe upande wa Mwanamke na kujenga nyumba yao, baada ya nyumba kukamilika na kuhamia hapo, migogoro ilianza na hali hiyo imemuumiza sana kisaikolojia.

Baada ya kuona maisha ya ndoa yamebadilika na kuwa machungu, sasa hatamani tena ndona na anawaza kuvunja ndoa hiyo, lakini anapokumbuka kuwa nyumba yake ambayo alitumia gharama kubwa sana mpaka ikakamilika, imejengwa kwenye kiwanja cha wakwe, na hajui afanye nini kuhusu mali hiyo.

Mbaya zaidi nyaraka zote zinasoma majina ya wakwe zake, yaani hali hiyo ndiyo imezidi kumchanganya zaidi.
Alizingua mwenyewe kutotafakari. unajengaje ukweni?
 
Wakwe hawawezi kukataa wajukuu zao, sana sana hapo sheria itaangalia kipato cha baba mtu; watafanya tathmini kiasi cha pesa atakacholipa kama child support. Mwanaume hapo unaanza safari upya. Yaani hapo jamaa hatoki. Sheria imeegemea upande wa wakwe.
Of course amejichanganya sana.
 
Back
Top Bottom