Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Ferouz: 🎶Wema wangu umeniponza sasa machungu ya dunia nayaona🎶

Kausikilize wimbo huu mkuu, kuna jambo utajifunza kuhusu wema. Sio kila wema hulipwa kwa wema, mungine hulipwa kwa mabaya kama hivyo.

Pole.
Naufahamu mkuu.
 
Pole, jamaa atakuwa anajua mtoto anateseka sema ndio ukute kajazwa sumu na mkewe.

Kila siku akirudu jioni anapewa orodha ya maovu ya dogo, kwahiyo akilini mwake anajenga picha ya mtoto jeuri, mtundu na asiye na thamani kwa familia.

Wengi walioishi na mama wa kambo wanayajua vema haya.

Hiyo siku ya kikao mchane ukweli wote waziwazi bila kuyumbisha maneno. Mwambie yeye ni MPUMBAVU MKUBWA!
 
Learn to mind yout own business
We mtoto wa mjini lakini inakuwaje kufatilia mambo ya watu,utakuja kufungwa siku kwa uzembe wako,dunia ya kibepari hii,bora ungeripoti kwenye mamlaka husika sio kumnunulia mtoto nguo,big mistake
 
Ooh inasikitisha sana Mungu atuepushe na hii mitihani aisee Ila fanya tu kumsaidia huyo mtoto kama nirafiki yako toka nitoke nina imani utakuwa unajuana na ndugu zake mtafute yule anaemuheshimu mwaambie waamfikishie huo ujumbe km utakuwa una ushahidi itakuwa poa sana than achana nae.
 
Mungu atakusimamia kwa sababu umesimama kwenye haki na mungu ana daraja maalum kwa wale wanaowatendea wema yatima, usichoke kumpigania huyo dogo, wazazi kama huyo home boy wako ndio wanaoongeza watoto wa mitaani inakera sana
 
Mpeleke kwenye mamlaka husika. Huyo jamaa anajua kila kinachoendelea na anakiunga mkono. Wiki mbili ni nyingi mno na lolote linaweza kumpata mtoto. Jitahidi kuokoa maisha ya hako ka malaika. Achana na huyo mshamba.

Amandla...
 
Pasingekuwa na mikingamo, wema wako ungelithaminiwa.

Sasa pata kujifunza kuwa desturi za kiAfrika, mawasiliano yote huwa ni kwa baba.

Mzigo ulopeleka kwa wema, baada ya kumkosa baba mwenye nyumba usingeliukabidhi kwa mkewe.

Wazo la jamaa wa kati kuwaweka kikao cha upatanisho ni wazo zuri na litaleta mafanikio.

Tatizo litabakia kwa jamaa yako muda pamoja na namna atakavyopona majeraha ya wivu.

Ukiisha maliza kuyaweka sawa maridhiano, jitahidi kuwa muwazi kwa rafiki yako kila hatua ili kuzuia ujinga wa namna hii usijirudie.
 
Jamaa uko na moyo wa kipekee, Mungu akulipe thawabu za kutosha. Wote tungekuwa kama wewe watoto wasingekuwa wanapata mateso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…