Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Ukitaka kufanya jambo lolote na mke wa rafiki yako, wasiliana na rafiki yako kwanza sio unamgongea shemeji yako na zawadi mumewe akiwa hayupo.
 
Chakufanya mrekodi mtoto akiwa anateswa msalabani alafu mtumie jamaa ajipimie mwenyewe
Kitu cha kwanza alitakuwa kufanya ilikuwa ni kumweleza rafiki yake ukweli kuhusu mateso ya mwanawe.zipo njia mbalimbali za kumueleza,kwa mfano..bro hebu jaribu kufuatilia malezi ya mtoto wako kuna mambo hayako sawa kabisa...
 
Achana naye ila report ustawi wa jamii mateso ya mtoto, mama Gwajima yupo hapa mtext tu, usiache mtoto aendelee kuteseka kwa sbb ya mjinga mtu mzima
Ku report ni swala zuri lakini rafiki yetu ameshauri nisubiri kwanza tuongee na jamaa. Akishindwa kumnyoosha mkewe ndio hatua zingine zitafuata.
 
Ulikosea ulipomkabidhi hizo nguo mkewe,ilibidi hizo nguo umkabidhi MUME na si mke.........MAWASILIANO YA NAMNA YEYOTE NDANI YA FAMILIA LAZIMA YAANZIE KWA MUME,UNLESS MUME HATAKI KUKUSIKILIZA
Asante mkuu kwa ushauri, lkn mimi sikufikiria wala kujua kama yangefikia huku.
 
Chakufanya mrekodi mtoto akiwa anateswa msalabani alafu mtumie jamaa ajipimie mwenyewe
Naamini nikipata namna ya ku record na kumuonesha jamaa, akili itamkaa sawa na atanipigia magoti kuniomba msamaha. We subiri nikipata namna ya ku record nifanye hivyo.
 
Duniani hapa bado **** watu Wana mioyo safi.

Mioyo ya kuhangaikia na kuumia hata Kwa wale wasokua Ndugu zetu.

Ubarikiwe sana Mkuu, usiogope kumpambania huyo mtoto.
Ndo najaribu kufanya ninachoweza kumuokoa mtoto na ikiwezekana kumuamsha mshikaji alielala fofofo kwenye dimbwi la mapenzi ya hovyo.
 
Haya uliyoyaandika kama ni ya kweli,Jamaa Yako ataiona Aibu sana,siku kikao chenu kikifanyika, maana wema unafanya kwa Mwanae tunaoamini mambo ya dini huyu mwanamke hafai na hana fikra chanya!
Kwa namna anavyoteseka huyu mtoto hata wewe ukiona hauwezi kuvumilia, utamsaidia tu kwa kweli.
 
Child protection ni emergency to me potelea mbali hata km ujirani utakufa, unaweza kufanya anonymously, hivi suppose huyo mtoto akaadhibiwa na kuuwawa leo usiku, Huoni hata kwako nafsi hiyo itakutesa maisha yako yote kwa kutochukua hatua? Au kuchelewa? Just common sense bro
 
Nimesikitishwa sana na jambo hili.
Zingatia ushauri uliotolewa na baadhi ya wadau hapo juu, hasa kuona uwezekano wa kulifikisha suala hili kwa Dkt. Gwajima D . Japo ni ngazi ya mbali, lakini naamini ni namna rahisi na ya haraka kupata msaada.
I wish hata ndugu upande wa Mama Mzazi wa Mtoto wangefahamu madhila anayopitia Mtoto wa Marehemu ndugu yao, na kuchukua hatua muafaka za kumsaidia.
Hata baba wa mtoto kama anapata muda wa kuufahamu ukweli nadhani mapenzi yake kwa mkewe yatapungua kwa kiasi kikubwa sana. Japo sishauri waachane, maana na huyu ashazaa nae, so akiondoka na kumuachia mtoto ina maana jamaa atajikuta ana watoto wawili. Mwanamke mungine atakaeowa na yeye akija na moyo wa kinyama hivi, hali itakuwa mbaya zaidi. Maana watateseka wawili badala ya sasa mmoja.

So itakuwa vizuri jamaa amuonye tu mkewe, na ikishindikana sana ndo achukue hatua anayoona inafaa bila kusababisha madhara ya baadae kwa huyu mdogo aliezaa nae. Lakini changamoto nyingine, haya yanafanyika nje ya Tz. Hivyo kuna hatua za kufuata ku report tukio ambalo pengine baadae linaweza kuniletea matatizo mimi binafsi.
 
Mtoa mada anaishi SA south Africa na amekaa huko muda Ila mnamwambia aende kwa Gwajima!

Popote alipo, Gwajima ni mfano tu wa authority areport tu kwa child protection services huyo mtoto ana haki ya kuwa mtoto na kukua kwa wazazi wake km watoto wengine na kama Hawako responsible wapo wanaoweza
 
Sijui huwa wanarogwa?yaani ni kama wanapumbazwa maana hata kusema nifanye uchunguzi mtoto anaishije wapi
Yani mtoto anapururuka yeye haoni. Halafu haya mambo ya watoto kuteswa na mama zao wa kambo sio mageni. Hivyo inatakiwa jamaa awe na muda wa kufuatilia namna mwanae anavyoishi.

Lakini jamaa wapi, akirudi ni kula kuangalia tv na kupanda kitandani kulala huku mtoto anateseka kila anapokuwa hayupo.
 
Child protection ni emergency to me potelea mbali hata km ujirani utakufa, unaweza kufanya anonymously, hivi suppose huyo mtoto akaadhibiwa na kuuwawa leo usiku, Huoni hata kwako nafsi hiyo itakutesa maisha yako yote kwa kutochukua hatua? Au kuchelewa? Just common sense bro
Thanks kwa ushauri mzuri bro
 
Back
Top Bottom