Pasingekuwa na mikingamo, wema wako ungelithaminiwa.
Sasa pata kujifunza kuwa desturi za kiAfrika, mawasiliano yote huwa ni kwa baba.
Mzigo ulopeleka kwa wema, baada ya kumkosa baba mwenye nyumba usingeliukabidhi kwa mkewe.
Wazo la jamaa wa kati kuwaweka kikao cha upatanisho ni wazo zuri na litaleta mafanikio.
Tatizo litabakia kwa jamaa yako muda pamoja na namna atakavyopona majeraha ya wivu.
Ukiisha maliza kuyaweka sawa maridhiano, jitahidi kuwa muwazi kwa rafiki yako kila hatua ili kuzuia ujinga wa namna hii usijirudie.