Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Usiende wewe aende huyo rafiki yenu wewe na "homeboy ", Kwa sababu tayari wewe una mgogoro na "homeboy". Lakini pia muwe na ushaidi wa kuthibitisha kwamba kweli uyo mtoto ananyanyaswa. ONGELA KWA KUJALI
 
Minadhani ulikosea mapema kutomweleza ukweli
Mimi niliogopa fitna katika ndoa za watu mkuu. Kuna midume mingine unaweza kuileza matatizo ya mke wake, badala lichunguze lenyewe linakwenda kumweleza mkewe kila kitu ulichomwambia.

End of the day unakuja kusutwa mbele ya watu nyumbani kwako. So niliamua nimsaidie yule mtoto kimya kimya tu.
 
Ni kweli bimadamu hubadirika,ila kununua nguo za mtoto na kumpa ni kosa pia.

Ungemchana live tu oya mbona dogo nguo zake zimechakaa hivi.Afu dogo mbina anakosa raha hebu fuatilia kitu juu ya dogo kama kipo sawa.
Hapo kweli hata mimi najilaumu, sema ndo ishatokea. Kilichobakia ni jamaa kuja kujua kinachoendelea. Wanasema dalili ya mvua ni mawingu.

So hii ni dalili ya jamaa kukaribia kujua ukweli hata kama sio kwangu basi ataujua hata kupitia mtu mungine. Wanasema safari moja huanzisha nyingine. So mimi nimeanza, kuna mungine atamalizia na siri kubumbuluka.
 
Nipe namba yake nikuonyeshepo jinsi ya kudeal na hayo madude
 
Sijui hii Ina ukweli kiasi gani, kama ni kweli, tegemea yafuatayo. Mtoto huyo atapata udumavu wa kukua, ulemavu wa kudumu, tatizo la akili na mwisho kifo. Usipotoa taarifa sehemu husika, utakuwa umeshiriki kumuumiza
Ukitaka kufanya jambo lolote na mke wa rafiki yako, wasiliana na rafiki yako kwanza sio unamgongea shemeji yako na zawadi mumewe akiwa hayupo.
Haya mawazo ya ngono muda wote hata kwa mambo ya msingi tutafika ?
 
Zipo tena huku ndio balaa mkuu. Nafikiri muda wowote kuanzia sasa nitalifikisha swala hili mahali husika, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya muhusika.
Kaka nenda karipoti.

Mostly abusers hua wanaongeza adhabu nikimaanisha anaona adhabu hii huyu kashaiona ndogo so inapanda.

Huu muda unaosema muda wowote kuanzia sasa huyo abuser anaongeza adhabu kisha dogo anapoteza uhai au anakua kilema.

Utaishia kujiuliza nafsi ikiwa ungeripoti asingefikia huko.

Kama dogo anasoma shule ilibidi wawe wa kwanza kuona makovu na majeraha na kuripoti kwa social welfare. Kama hasomi wewe jirani hilo ni jukumu lako.

Muokoe mtoto
 
Nipe namba yake nikuonyeshepo jinsi ya kudeal na hayo madude
😀😀 Nilifuta siku ya pili yake baada ya kuwa tupo lunch tunakula eti ananiuliza mbele ya watu ,
Mshangazi gaidi :kijana umeshiba ? Maana huko ndani sitaki miayo 🙃

Mnyonge Mimi wa mapenzi : Nimeshiba mkuu .

Mshangazi gaidi: Basi sawa tukafanye kazi sasa
 
Shukran mkuu ngoja niufanyie kazi ushauri wako 🙏
 
mijike mingine ina roho mbaya ,sasa chakula kanunua baba yake mpe ale ili akue akupishe hapo ebo!
Mingine kama hili limetoka katika nchi ya vita na njaa, sasa limefika katika amani na chakula kedekede linasahau na kuanza kumtesa mtoto wa mwenzake.

Hili ndio tatizo la jitu jeusi, likishiba tu linasahau shida 🤣🤣🤣
 
Yaani wewe jamaa hufai, mtoto anateswa na kunyanyaswa katika umri huo ushindwa kuchukua hatua? Eti ulikuwa ukiongopa kumwambia homeboy wako? Kama kweli ulikuwa na nia ya kusaidia ulishindwa kureport Police kimya kimya? Ulishindwa kutoa taarifa ustawi wa jamii? Serikali za mitaa hukujui? Acha hizo za kuja kutafuta huruma hapa, wewe kama mzazi ulipaswa kuvaa viatu vya huyo mtoto na ungechukua hatua
 
Asante kwa ushauri mzuri mkuu. Inaonesha una moyo wa upendo sana, na unaweza kulea mtoto ambae sio wa kwako.

Mungu akubariki na kukuongoza kwa kila jambo zuri unalofanya.
 
hongera umefanya kazi nzuri ila ni vema ukiona ngumu kulikamilisha kumsaidia mtoto, tumua asasi za kiraia zinazohusika na masuala ya kijamii,mtoto atasaidiwa na ukweli utajulikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…