Rafiki yangu wa ukubwani kafariki kisa ndoa

Kuna kitu Kinaitwa NGUVU YA KUJUA UKWELI.

Ngoja siku ujue Her other side.

#YNWA
 
Kuna kitu Kinaitwa NGUVU YA KUJUA UKWELI.

Ngoja siku ujue Her other side.

#YNWA
Wala usintishe Jomba we unakutana na madanga unadhani dunia nzima iko hivyo, kama unataka wife material lazma na we uwe husband material so we pambana na majanga yako huko udangako, ndoa ni raha ukiingia mahala sahihi, we met at our younger age and now we are parents to a very beautiful family Alhamdulillah
 
Daaah ishi kimya tu
 
Asante
Asante kwa huu uzi mkuu, kuna kitu nimejifunza hapa kutokana na mahusiano yangu ya sasa hayana afya kabisa, siku chache zijazo nitaweka uzi nipate elimu zaidi hapa jamvini.
 
Kwahiyo wotee wanaokuzunguka wenye ndoa NGUMU ni kwasababu wake zao ni madanga?

#YNWA
 
1. Bill gate kaachana na ndoa, Hivi MELINDA GATE ni MDANGAJI?

2. Dangote kaachana na ndoa, hivi mke wa billionea wa Africa ni MDANGAJI?

3. Kwenye ile top Ten ya RICHEST PEOPLE IN THE WORD, asilimia 70 wameachana na wake zao, HIVI WAKE ZAO NI WADANGAJI?

#YNWA
 
Kama sio Malaya shoga yangu mvumilie tu
 
Ngoja bas ni mi niwe Billionaire niachane na wangu ili ujione mtabiri, acheni kushambulia kila mwanamke kwa reference ya majitu ya hovyo mnayokutana nayo, wazazi wangu wapo ktk ndoa kwa zaidi ya miaka 45 leo na ni wazee na sikuwahi kuona wakizinguana pamoja na ukweli kua kama familia tumewahi kupita nyakati ngumu mnoo, so wapo watu wako ktk ndoa na wanakula raha hivyo huwez kuja na general statement kua ndoa hazina maana
 
Nyie oeni tu.

Jana nikiwa ofisini, alikuja jamaa ni fundi ofisi ya jirani hapa kwetu. Karudi kutoka shamba alikohamia baada ya kuona maisha ya mjini hayakai sawa, akaamua yeye na mkewe warudi zao shamba kama miaka miwili sasa na kule shamba wana mashamba ya familia hivyo ni uwezo wako tu wa kuyahudumia.

Jamaa akaanza kulima Ufuta, huku kwingine akiwa na minazi, yeye Ufuta aliacha ukiwa umeshavunwa mwezi wa pili alivokuja tena town. Mwezi wa tano akampigia simu mkewe aliyebaki shamba kumuuliza kama alienda kupima ghalani, mkewe akamwambia asubiri kwanza atamjuza. Siku zimekwenda hapewi jibu, sasa siku moja akapigiwa simu na jamaa yake tu jirani kumuuliza kilo walizopata, jamaa akabaki na butwaa sababu hajui chochote wala hajashirikishwa lolote na mkewe.

Basi yule jamaa yake akamsihi kuwa asimwambie mkewe kama yeye ndiye alotoa taarifa hiyo ya ufuta kupelekwa ghalani na pesa akalipwa. Kumbuka huyu mke na mume wana akaunti benki ya pamoja, kiasi kwamba pesa ikiingia benki mume anapata ujumbe kwenye simu yake. Mume akaanza kumkomalia mkewe amwambie amepima kapata bei gani! Mke akawa Mbogo, akamjibu ametumia akaunti ya kaka yake kufanya malipo. Jamaa akaona hili limeshakuwa tatizo, akaondoka zake kurudi Pande hapo mjini Kilwa, kufika akaenda mpaka kwa kaka mtu kumuuliza kama malipo yalifanyikia kwenye akaunti yake, kaka mtu akamwambia amuulize vizuri mkewe malipo alikofanyia. Mke akalipuka akamwambia mumewe, pesa hana na anataka talaka yake
Lahaulaaaaaaaaaa!!!!!!!!

Bwana yule ikabidi akatoe taarifa kwa wazazi, kikaitishwa kikao upande wa mke na upande wa mume. Mume akaeleza ya kwake na kubwa alilokuwa analidai ni fedha za jasho lake ila mke alilolizungumza kwa kumaanisha ni kuwa ANATAKA TALAKA YAKE LA SIVYO KATI YAKE MKE AU MUME KUNA MTU ATAKUFA HAPO, watu wakahamaki! Yule bwana akamwambia mkewe ampe pesa zake Talaka itafuata, mke akakataa ikabidi baba mkubwa wa mume atoe talaka kwa niaba ya mwanae ili kunusuru mengine.

Mshikaji alipoona jambo limefikia hivyo ikabidi arudi tu Dar aje kuanza maisha mapya, ila alichokisema yule bwana ni anataka Amuue alokuwa mkewe ndio awe na amani.

Nb hii ndoa haina hata miaka minne.
 
Kipanya alisema malcolm alitufundisha kushukuru. Shukuruni kwa kila jambo
 
Wajifunze k*m*m*k, watu wanaoa kwa mihemko na uzuri wa umbo na sura, let them die f*ck! Na iwe fundisho. Wanawake wenye mapenz ya kweli wapo ila hawana sura wala shape za kuvutia, ila watu wanahangaika na ma-slay queen.
 
Wajifunze k*m*m*k, watu wanaoa kwa mihemko na uzuri wa umbo na sura, let them die f*ck! Na iwe fundisho. Wanawake wenye mapenz ya kweli wapo ila hawana sura wala shape za kuvutia, ila watu wanahangaika na ma-slay queen.
Hata hao wasio na shape nzuri, kiumbe kikishakuwa cha kike tu! Ni tabu mnooo
 
POLE NYINGI KWAKE NA MUNGU AMREHEMU! Wanawake hawa na hongo za ngono wanazotoa mahakamani yaani balaa tupu!
Mimi nilinusurika kujinyonga hivihivi! Nyumba zangu 3 na viwanja 2 vilienda na maji! Nilala nakesha muda wa miezi 4, nikanunua kamba kabisa ili nijimalize.

Nilikuwa naamka usiku wa manane zaidi ya mara tatu ili nijining'inize lakini nikiwafikiria wanangu narudi tena kitandani! NAMSHKURU SANA MUNGU alivyoweza kunituliza nikakivuka kipindi kile kigumu! Nilipungua uzito zaidi ya kilo 6!
Hayo mambo ya TALAKA omba yasikutokee, kuna wanawake mashetani wakubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…