Rafiki yangu wa ukubwani kafariki kisa ndoa

Rafiki yangu wa ukubwani kafariki kisa ndoa

Ukipatikana utaratibu mpya wa kuweza kupata watoto na kuwalea vyema bila kuishi kwenye committed marriage itakuwa poa sana..na life expectancy ya wanaume itaongezeka mara dufu.

For the meantime tukubali tu kuwa bila ndoa bora taifa hili sijui litakuwa na kizazi cha namna gani.
Ni mtihani na kitendawili kikubwa kwakweli

Kuna time unakata tamaa na kuchukia kabisa haya mahusiano

Ila kuna time unatamani umpate wa kutulia nae na kumpa mapenzi yako

Tatizo ni pale yule unaewekeza upendo wako kwake anakukorogea mambo meusi mpaka unakoma
 
Nyie oeni tu.

Jana nikiwa ofisini, alikuja jamaa ni fundi ofisi ya jirani hapa kwetu. Karudi kutoka shamba alikohamia baada ya kuona maisha ya mjini hayakai sawa, akaamua yeye na mkewe warudi zao shamba kama miaka miwili sasa na kule shamba wana mashamba ya familia hivyo ni uwezo wako tu wa kuyahudumia.

Jamaa akaanza kulima Ufuta, huku kwingine akiwa na minazi, yeye Ufuta aliacha ukiwa umeshavunwa mwezi wa pili alivokuja tena town. Mwezi wa
Laaulaah! Yan kila siku vituko haviishi hapa duniani aisee hawa wanawake wa kizazi cha nyoka wana shida gani
 
Hatujapata kujua ukweli toka upande wa pili .

Kuna uwezekano mkubwa huyo Mwanaume akawa ndiye mkosaji zaidi kwa kuzaa nje ya ndoa na mwanamke mwingine.

Pengine makosa yake ndio yamefanya dhamiri yake imhukumu ndani kwa ndani hadi kuangamia.

Kuna Habari sahihi ukizisikia Mwanaume wa ndoa amemfanyia mkewe utachoka sana!

Kuna Mwanaume anafika mahala hatunzi familia hela yote inaishia kwa mahawara!

Kuna Mwanaume mwingine anatumika nje ya ndoa sana wakati kwa mkewe nguvu anakuwa hana.

Kuna matukio ya ajabu kwenye ndoa Yani ukiwasikiliza wanandoa tofauti tofauti utachoka.
 
Unaijua maana ya kuvumiliana kwenye ndoa?

Yatakupata mabaya kuliko hata yaliyompata mwenzi wako Ni swala la muda tu.


Hivi kipimo cha uvumilivu ni kipi kwa mfano?

Je avumiliwe mtu anayeendelea kufanya makosa ya makusudi hata baada ya kuonywa mara kadhaa?
 
Ni mtihani na kitendawili kikubwa kwakweli

Kuna time unakata tamaa na kuchukia kabisa haya mahusiano

Ila kuna time unatamani umpate wa kutulia nae na kumpa mapenzi yako

Tatizo ni pale yule unaewekeza upendo wako kwake anakukorogea mambo meusi mpaka unakoma
Yeah..

Ulichosema ni kweli kabisa.
 
Yupo mwingine namjua
Mgogoro wa ndoa na kesi za mahakamani, alikua na maisha mazuri nasikia now kapoteza kila kitu hadi nyumba yake anatembea anaongea mwenyewe barabarani.
Wanawake tuwe na huruma
Sorry for HIM.

#YNWA
 
No noo,unakosea mkuu.kumwita wizard mtu ingali hujui anapitia nn.unakosea.But it is okay huenda ulivyoandika ivo moyo wako umepata ahueni
Don't judge a book by it's cover inaonekana ulivutiwa nae sana b4 hujagundua madhaifu yake Sasa unaumia sana na kujuta
 
Wajumbe sikieni hii.

Mwaka 2012 nilikutana na Dav (sio jina lake halisi) akiwa mkuu wa kitengo fulani ofisi kubwaa Morogoro.
Kipindi hicho mimi nilienda ofisini kwao kufanya field, kwa sababu yeye alikua mkuu wa kitengo nilichopangiwa field then nilimkubali sanaa mwana.

Alikua mchapa kazi balaa hivyo kitengo kiling'ara kwasababu yake.
Maisha yake binafsi yalikua mazuri huku akimiliki nyumba na gari (simply kijana mwenye chenji zake).

Field ikaisha na mimi nikaondoka ila urafiki uliendeleaa halafu ukapotea ghafla.

Baada ya muda bila kuwasiliana siku moja (mwaka jana) ghafla nikamkuta njiani.

Alikua kachoka balaaa, halafu anatafuta kazi. Ikabidi nisimamishe tukituki yangu ya miguu 4 apande kwenda sehemu kuongea.
Alikua kama kachanganyikiwa. Nikampa lunch then nikampeleka gheto, alikaa gheto kama wiki hivi, then akasepa Dar.

Tukiwa nyumbani kwangu akanipa hadithi kwamba mwaka ule wa field yangu (2012) alioa. Mkewe alimkuta Dav ana nyumba, gari, mashamba na mali nyingi tuu.

Baada ya ndoa, miaka iliyofata maisha nyumbani yalianza kuwa magumu, kampuni ilikua ya wazungu. Mkataba uliisha, wazungu wakarudi kwao, Dav akakosa kipato cha kudumu. Mkewe akachepuka na kuhamia kwa jamaa mpya moja kwa moja.

Mkewe alipeleka kesi mahakamani kuomba talaka. Huko nako Dav alichosikia, mkewe alitembeza hongo mpaka talaka ikatolewa. Ilibidi gari na mashamba yauzwe iliwagawane na ndoa ivunjwe.

Nikashangaa sana, nikamuuliza ""Mbona hizi Mali ulizipata kabla ya ndoa?"" Alinijibu "hata sijui nini kilifanyika, na vile kuokoa watoto wangu (wawili) ilibidi nikubali liuzwe gari na mashamba ndio tugawane halafu nyumba abaki nayo akae na watoto""

Mwana alikua kama kachanganyikiwa. Tuliongee akasema anaenda Dar kutafuta ajira na anashukia kwa Steve (sio jina lake halisi).
Kwa bahati nzuri Steve namjua sanaa (classmate). Then siku ilivyofika nikampeleka stend akapanda ndinga huyoo Dar.

Yote haya yalitokea February/2021. Leo yaani alifajiri hii napata taarifa kuwa ""Davi kafariki kwasababu ya ugonjwa wa akili"" Steve anasema, Dav alikuwa mwana Sana, tulicheza na kukua wote kitaa.
Kwasababu tupo field moja ya kazi, tuliunda kama team ya kusaidiana kimawazo ya fani yetu kila jambo, liwe jipya au gumu tunashirikishana.

Ila tokea aoe na kuanza matatizo ya ndoa performance ilishuka. Kazi zikaisha na mali zake zikauzwa, alivyofika Dar alikua kama chizi, kutwa kuwataja wanae, mara aropoke majina ya mkewe kwa hasira na vitu kama hivyo.

Tarehe 01/08 hali ilikua mbaya hasa, akakimbizwa hospital. Na leo 07/08/2021 Dav kafariki kwasababu ya matatizo ya akili.

Watoto wawili hawana baba tena. Kuna wazazi wamepoteza mpendwa wao mtoto wa kiume pekee. Kuna sisi tumepoteza role model wa kazi na rafiki. Tasinia yetu ya science imepoteza mtaalamu. Tanzania imepungukiwa GDP

Alidhani kuoa ni kuzuri kumbe kumemtafutia kifo mapema akiwa na miaka 39 tuu.

Tafuta hela kijana kuoa ni upuuzi kwa dunia ya sasa.
Hawataki penzi lako ila wanataka hizo mali zako tuu. They are gold diggers, they need kuchimba dhahabu yotee kutoka kwenye huo mgodi wako then wauache empty.

Leo nipo gheto kusikiliza nyimbo alizozipenda Dav tuu.

RIP Brother

"If you think money can't buy happiness, nenda kaulizewanufaika wa ajira mpya za walimu wiki hii walivyolipwa hela zao za kujikimu walijisikiaje.

View attachment 1883485

View attachment 1883489

Tafuta hela kijana.

#YNWA
Hahaha
 
Back
Top Bottom