Jamal ni mwanangu sana,
Tulikua tunapanga mipango mingi. Tangu ameowa amekuwa mtu mkimya sana.
One thing I noticed, mkewe huwa hanikubali mimi as a friend to her husband. Namuona fala, kwa sababu mimi nafunika mashimo mengi ya Jamal. Jamal hakuwa eligible kukopa sehemú fulani. Nikasaini makaratasi kwa jina langu nikakopa milion 4 akachukua yeye. Mi shida yangu ilikua laki 5 tu. Mi napigiwa simu na ofisi unadaiwa huleti marejesho........
Lakini Jamal huwa ananikubali mno hasa kwenye deals za pesa.
Jamal baada ya kubadili kampuni ya kazi, amepata marafiki wapya. Mara nyingi nikipanga kukutana naye namkuta nao. Wana mipango yao. Ila akikwama huko hunitafuta. Jamal ni kweli familia inamshughulisha mno. Kuna saa namuonea huruma. Unaweza sema yuko kimya ana enjoy, kumbe ana bills kibao zinataka kulipwa.
Jamal alijenga nyumba ikaishia kati. Nyumba ya kisasa kweli, lakini kwa mpunga aliovuta angeweza kujenga simple house kwanza. Ya milion 30 hivi au 40 ingetosha. Dah sasa bado ana panga na nyumba ile sijui inaisha lini?
Jamal sio jina lake halisi na baadhi ya vitu nimetwist kuficha uhalisia.
Asante.