Rafiki zangu wanapooa ukaribu wetu hupotea ghafla, nini kinawapata huko?

Rafiki zangu wanapooa ukaribu wetu hupotea ghafla, nini kinawapata huko?

Ukiona mwana kaoa alafu kawakataa wahuni jua huyo si mwana alafu ni ndezi maana wana wa ukweli ni pesa , ni madini ni almasi .
Aloo! 🤝Siku hizi upo free!! Niliona uko banned nikajiuliza huyu nae kafanyaje tena??!

Ulichosema ni kweli, kuna watu wakioa wanaona wamemaliza kazi, kumbe ndio imeanza 😀
 
Jamal ni mwanangu sana,
Tulikua tunapanga mipango mingi. Tangu ameowa amekuwa mtu mkimya sana.
One thing I noticed, mkewe huwa hanikubali mimi as a friend to her husband. Namuona fala, kwa sababu mimi nafunika mashimo mengi ya Jamal. Jamal hakuwa eligible kukopa sehemú fulani. Nikasaini makaratasi kwa jina langu nikakopa milion 4 akachukua yeye. Mi shida yangu ilikua laki 5 tu. Mi napigiwa simu na ofisi unadaiwa huleti marejesho........
Lakini Jamal huwa ananikubali mno hasa kwenye deals za pesa.

Jamal baada ya kubadili kampuni ya kazi, amepata marafiki wapya. Mara nyingi nikipanga kukutana naye namkuta nao. Wana mipango yao. Ila akikwama huko hunitafuta. Jamal ni kweli familia inamshughulisha mno. Kuna saa namuonea huruma. Unaweza sema yuko kimya ana enjoy, kumbe ana bills kibao zinataka kulipwa.

Jamal alijenga nyumba ikaishia kati. Nyumba ya kisasa kweli, lakini kwa mpunga aliovuta angeweza kujenga simple house kwanza. Ya milion 30 hivi au 40 ingetosha. Dah sasa bado ana panga na nyumba ile sijui inaisha lini?

Jamal sio jina lake halisi na baadhi ya vitu nimetwist kuficha uhalisia.
Asante.
Take it positively,
One: anakupunguzia majukumu.
Two: wife anamkomaza mumewe, to carry his responsibilities fully, to spread his own wings even further.
 
Ulivyomtetea sasa😓
Kuna kipindi nilipata majanga nikawa sipatikani hewani week nzima. Hapo nimeaga geto naenda Moro mara 1.
Baada ya mwamba kunikosa, hana namba ya mtu mwingine yoyote wa familia wala mchumba wangu.
Alipambana akapata namba ya mama yangu after 10 days.
Mama akampa namba ya mkwewe (mchumba wangu) ndio juhudi ikafanyika akanipata.

Nnavyosema hivyo namaanisha. Jamal sio mtu mbaya. Ila mkewe yule siyo.
 
Kuna kipindi nilipata majanga nikawa sipatikani hewani week nzima. Hapo nimeaga geto naenda Moro mara 1.
Baada ya mwamba kunikosa, hana namba ya mtu mwingine yoyote wa familia wala mchumba wangu.
Alipambana akapata namba ya mama yangu after 10 days.
Mama akampa namba ya mkwewe (mchumba wangu) ndio juhudi ikafanyika akanipata.

Nnavyosema hivyo namaanisha. Jamal sio mtu mbaya. Ila mkewe yule siyo.
Umepata uhakika gani kwamba mkewe sio?
 
Kwenye jando tulifunzwa kufuatana na kuwa na marafiki wa rika letu.

Kama umeenda jando hutakiwi kukaa na wasiotahiriwa.

Kama umeoa hutakiwi kufuatana na wasiyooa.

Na mtu akipewa mafunzo kwamba asiwe na marafiki bachela hawezi kuja na kukuambia kuwa ameambiwa asiwe na marafiki bachela.
 
Mtu akishaoa ni kwamba kashavuka step moja mbele yako maana anakuwa busy na ndoa pia anakuwa amempata rafiki mwingine anaye lala naye kitanda kimoja na shuka moja. Baki na wahuni wenzako mkuu hadi na wewe utakapofanya maamuzi magumu kama yeye.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Ilikuwa nzuri hadi uliposema maamuzi magumu…

Kuoa sio uamuzi mgumu, ni uamuzi sahihi.
 
Hapana. Jamal sio mhuni. Kuna wakati mi sikuwa na kazi, nilikua na deal chache tu za pesa afu nimetoka mkoa kuhustle alinifadhili kuishi ghetto kwake karibia mwaka mzima.
Maana nilikaa July mpaka June mwaka unaofata.
Ni mwana hasa. Akiwa nacho mtakula na hata pocket money anakupa.
Ni mwana sana sana. Na tulikutana tu katika mazingira ya kazi, sikusoma naye na wala hatujakuwa wote utotoni.
Jama ni mwana, sema kule kuowa kumemtoa kwenye reli.
Hapo nimekusoma basi mke wa Jamal anakusnitch kwa mwanao kuwa wewe hufai

Sema nini as long as uwa unamsaidia jamal baadhi ya harakati basi kaa ujue ipo siku mkewe jamal atakukubali na mtakuwa familia .

Ila shida ni jamal naye kuendeshwa na hako kademu alafu anamsahau muhuni wake
 
Back
Top Bottom