Rafiki zangu wanapooa ukaribu wetu hupotea ghafla, nini kinawapata huko?

Halafu mambo ya simu yangu yanahusiana vipi na pointi zangu embu badili fikra za kishamba

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Na kuna muda anakuwa Malaika wa Kifo 🤭😆
 
Jamal ni mwanangu sana,
Tulikua tunapanga mipango mingi. Tangu ameowa amekuwa mtu mkimya sana.
One thing I noticed, mkewe huwa hanikubali mimi as a friend to her husband. Namuona fala, kwa sababu mimi nafunika mashimo mengi ya Jamal. Jamal hakuwa eligible kukopa sehemú fulani. Nikasaini makaratasi kwa jina langu nikakopa milion 4 akachukua yeye. Mi shida yangu ilikua laki 5 tu. Mi napigiwa simu na ofisi unadaiwa huleti marejesho........
Lakini Jamal huwa ananikubali mno hasa kwenye deals za pesa.

Jamal baada ya kubadili kampuni ya kazi, amepata marafiki wapya. Mara nyingi nikipanga kukutana naye namkuta nao. Wana mipango yao. Ila akikwama huko hunitafuta. Jamal ni kweli familia inamshughulisha mno. Kuna saa namuonea huruma. Unaweza sema yuko kimya ana enjoy, kumbe ana bills kibao zinataka kulipwa.

Jamal alijenga nyumba ikaishia kati. Nyumba ya kisasa kweli, lakini kwa mpunga aliovuta angeweza kujenga simple house kwanza. Ya milion 30 hivi au 40 ingetosha. Dah sasa bado ana panga na nyumba ile sijui inaisha lini?

Jamal sio jina lake halisi na baadhi ya vitu nimetwist kuficha uhalisia.
Asante.
 
Atakutafuta tu ngoja ndoa iote mapembe kwanza hayo ni mambo ya kawaida kwa baadhi ya watu waliyo oa,nimeshaishi na watu wa namna hiyo. Yakiwafika huwa wanarudi resi kama gari lililofeli breki.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Hahah wanasahau walikotoka! Ila watakumbuka tu
 
Ni mfano tosha wa usaliti!
 
Atakutafuta tu ngoja ndoa iote mapembe kwanza hayo ni mambo ya kawaida kwa baadhi ya watu waliyo oa,nimeshaishi na watu wa namna hiyo. Yakiwafika huwa wanarudi resi kama gari lililofeli breki.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Hivi hapa tuna miezi kama 2 hatujazungumza wala kutumiana msg. Nakumbuka mara ya mwisho nilimtumia ishu fulani acheki anipe feedback. Ameniblue tick na amekausha......😅😅
Mimi nikiowa atajuta huyu. Maana mama mtoto wangu anajua visanga vyake vingi. Tushakutana na Jamal mara 2 mimi nikiwa na mama mtoto wangu yeye ana madem tofauti.
Nadhani siku nikiowa ntapigwa marufuku hata kuongea naye.😅😅
 
Jamal si mwana ni muhuni fulani anapenda kamserereko kwako hamna lolote.
 
Jamal si mwana ni muhuni fulani anapenda kamserereko kwako hamna lolote.
Hapana. Jamal sio mhuni. Kuna wakati mi sikuwa na kazi, nilikua na deal chache tu za pesa afu nimetoka mkoa kuhustle alinifadhili kuishi ghetto kwake karibia mwaka mzima.
Maana nilikaa July mpaka June mwaka unaofata.
Ni mwana hasa. Akiwa nacho mtakula na hata pocket money anakupa.
Ni mwana sana sana. Na tulikutana tu katika mazingira ya kazi, sikusoma naye na wala hatujakuwa wote utotoni.
Jama ni mwana, sema kule kuowa kumemtoa kwenye reli.
 
🤣🤣🤣
 
Ulivyomtetea sasa😓
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…