Raha ya kuzaa na pisi kali, uhusiano unakuwa unadumu kutokana na mtoto

Raha ya kuzaa na pisi kali, uhusiano unakuwa unadumu kutokana na mtoto

Katika uzee wangu nitakuwa na mitoto iliyoshiba kama 15 hivi wakiwa wamenizunguka, huku nyie mkiwa na kimoja au viwili tu 😀😀​
 
Hakuna mwanaume mwenye akili anaweza kuwa proud na vitu kama hivi , definitely chai 💯 au just a wish kwa sababu unafikiri ni ujanja na inawezekana wewe bado kijana mdogo
Watoto ni hazina, mapori yanahitaji yajengwe majengo. Bila kuwa na watu, yatajengwaje?
 
Wakuu habari,

Katika ujana wangu niliweza kuzaa na pisi kali watatu, na mwingine wa nne ni wakawaida.

Kutokana na kuzaa nao watoto wazuri, mawasiliano yamekuwa ni ya mara kwa mara, hasa kwenye kujuliana hali pamoja na kuchangia maendeleo ya huo uzao wetu; ingawa wao hawafahamiani.

Kwa sasa wao wana mahusiano mengine, lakini kutokana na watoto niliozaa nao imekuwa njia ya kutuweka karibu, na wakati mwingine wanalazimisha tukutane kwa gia ya mtoto amenikumbuka.

Nami najivunia kuzaa na hawa pisi kali, lasivyo nyakati hizi wangenikimbia kama nisingeliweka alama ya kuzaa nao watoto.

Nashauri kwa wanaume wanaotoka na pisi kali, msiishie kuwahonga tu; hakikisheni mnaweka alama za watoto.

Ata kama ulihonga gari, nyumba, cheo n.k yule mtoto atakuwa anakupunguzia machungu iwapo mama yake atakengeuka, kwa sababu mahusiano hayatabiriki.​
Ubwege huu
 
Back
Top Bottom