Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.

Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.

Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.

Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.

Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.

Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.

Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.

Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.

Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.

Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.

Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.

Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.

Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.

Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.

*Angalizo*

[Kuwa na tume huru ya uchaguzi haimaanishi moja kwa moja kuwa CCM itashindwa na wapinzani watashinda kwenye chaguzi kuu. Tunachotaka baadhi yetu ni kuwa na tume huru inayoaminika.]

Nonsense. What is tume huyu? Yesu Marua ba Joseph? Itachaguliwa na Mungu? Au Obama? Au Tundukissu? Huyi anayeichagua anachagua kwa niaba ya watu waliomkubali. Lazima awe Rais. Kama Rais ni biased ni kwa sababu waliomchagua ni biased. Ni lazima tu watu wanataka awe biaesd kwa sababu walimchakua kwa bias yao. Rais kama hafai basi tusubiri CUF washinde wawe na Rais hapo ndipo tume itajaa watu wa Sultani na mashoga kama walivyo CUF walioshibda uraus. Ukitaka mtu neutral labda awe Mufti wa Makka au Papa Fransisko. Wacheni huu ujinga wa Kenya wa kutokubali kushindwa, sasa Katiba ovyo ya Kenya inawatafuna. Sasa wanataka pawe na Waziru Mkuu na Makamu WM ili wagawane mkate.
 
Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.

Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.

Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.

Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.

Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.

Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.

Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.

Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.

Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.

Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.

Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.

Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.

Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.

Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.

*Angalizo*

[Kuwa na tume huru ya uchaguzi haimaanishi moja kwa moja kuwa CCM itashindwa na wapinzani watashinda kwenye chaguzi kuu. Tunachotaka baadhi yetu ni kuwa na tume huru inayoaminika.]
Nani atakayekubali tume huru? Magu au CCM. "Kinachohitajika ni ukombozi wa pili kutoka kwa mkoloni mweusi"
 
vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote

mkuu hapa umenena na ndiyo njia ya kukomesha uupuzi wote, lakini vyama vya siasa kwa kupenda ruzuku na unafiki watataka wakashindane na ccm ambayo ina mtaji nzuri wa mfumo hadi kwenye tume ya uchaguzi.

mkuu kwa kusaidia nikuombe tuanzishe vuguvugu la kususia uchaguzi hadi pale katiba na tume huru ya uchaguzi ipatikane
 
wananchi wanapewa motisha na vyama vyao vya siasa!! vyama kazi yao just kuwaongoza wapiga kura wao km vyama vimelala what do u expect from wananchi wanaowapigia kura? vyama havina namna ya kulikwepa hili km wameshindwa waseme tuingie wenyewe mzigoni simple...

Kwamba kama vyama vimelala, basi na wananchi nao wanalala. Eti? Kwamba unasubiri vyama vya siasa vikuambie kuwa vimeshindwa? La sivyo, wewe unakula shushu tu. Na kumbuka, vyama vya siasa havijashuka kutoka mbinguni. Vinaakisi aina ya jamii tuliyonayo. Kama tuna jamii ya watu mbumbumbu na wabinafsi, basi ujue na vyama vya siasa na viongozi nao watakuwa hivyo hivyo. It's insanity to expect a different outcome. Nobody is going to do it for you; you have got to do it yourself.
 
Yes, ila ujue kuna walioshika dhamana, mfano, wananchi tujikwamue kiuchumi km serikali itakuwa na vikwazo kwenye kujikwamua kwetu unafikiri kuna kitu kitatokea?

Vyama vya kisiasa vikilala pia wananchi watalala kwa kiasi fulani,kwa kifupi vyama vya sasa vipo kiruzuku zaidi?
 
Mletaa mada ulipaswa kusema (kichwakisomeke,),
Watanzania wadai

Katiba mpya sio wapinzani.wao wabakie waratibu
 
Ni Mara kadhaa sasa serikali kupitia NEC imekuwa ikipindua matokeo yenu hadharani huku wakisaidiwa Na jeahi la police.

Mfano Upo hai Kwa chaguzi Za jana buyungu, Arusha Na zile Za nyuma Kwa Kinondoni Na Siha.

Mkilala hata Monduli Na Ukonga itakuwa hivi hivi.

Naomba viongoZi wa CDM mtoe neno kuhusu hiki maana sisi wapiga Kura wenu tunahasira sana.

Kwa kuwa hakuna atakayeishi hapa milele, I assure you Kwa hali ilivo sasa tupo tayari Kufa kutetea haki zetu. Jitokezeni hadharani MSEME.

I am crying inside out for my country Tanzania
 
Njoo huku mtoe neno wajamoni
 
Neno linasaidia nini
Dawa niwewe namimi kukataa huu upumbav
 
Tusisahau jinsi tulivyompa kichwa dada wa taifa siku ya mwisho akawa kituko huko mambele
 
Ni Mara kadhaa sasa serikali kupitia NEC imekuwa ikipindua matokeo yenu hadharani huku wakisaidiwa Na jeahi la police.

Mfano Upo hai Kwa chaguzi Za jana buyungu, Arusha Na zile Za nyuma Kwa Kinondoni Na Siha.

Mkilala hata Monduli Na Ukonga itakuwa hivi hivi.

Naomba viongoZi wa CDM mtoe neno kuhusu hiki maana sisi wapiga Kura wenu tunahasira sana.

Kwa kuwa hakuna atakayeishi hapa milele, I assure you Kwa hali ilivo sasa tupo tayari Kufa kutetea haki zetu. Jitokezeni hadharani MSEME.

I am crying inside out for my country Tanzania
Maandishi nyuma ya keyboard huwa hayaakisi ukweli: kumbuka maandamano ya Mage yalivyobuma ingawa katika mitandao ungalidhani hakuna atakayebaki
 
Una hasira? Wewe ndiye ulikuwa unagombea? Wajinga ndo mtaji WA wanasiasa!!
 
Endeleeni Kushangilia hii ni style ya Uganda na Rwanda ...Jiwe ameamua sio mtu wa kutoka.
 
Write your reply...CDM inapaswa kujitafakari kwa kina je watamudu huu mchezo?Ikishindikana turudi tulipotoka,inauma watu kuumizwa wakati ni watanzania walewale,mbona tunagombea fito?
 
Back
Top Bottom