Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Hakuna sababu ya kushiriki mechi ambayo refa ni wao na uwanja ni wao, ukinyimwa goli au penati utamlaumu nani?

Mimi siwezi kupiga tena kura kwa tume hii hii.
voters turnover ya 2020 Itashuka sana.Na atapata asilimia 98
 
Wazo zuri lakini umesahau CCM ina vyama vyake vya upinzani vitakavyotumika kufanya justification za kisheria. Lazima udai huku unashiriki; mtasusa 4 wengine 6 kwa maslahi yao wanashiriki; haki unaipataje hapo.
waache hao sita washiriki.Kwani unadhani watu hawaoni.Kwa mfumo huu wa Tume 2020 CHADEMA wakiweka wagombea watakuwa mazwazwa
 
waache hao sita washiriki.Kwani unadhani watu hawaoni.Kwa mfumo huu wa Tume 2020 CHADEMA wakiweka wagombea watakuwa mazwazwa
Na ndio kipimo cha kuwapima kwamba akili zao zipo kwenye ruzuku tu au ni movement 4 change kweli?

Tukishawabaini sasa wananchi tutaunda chama cha ukombozi hatutaki tena chama cha siasa, siasa kwa sasa basi tutatumis njia mbadala.
 
Sina mengi wala nisiwachoshe akili, ni wazi kama kuna upinzani wa kweli nchi hii basi tuache yote lianzishwe vuguvugu la kudai katiba mpya sasa na tume huru ya uchaguzi au kinyume chake wote tutulie tuiache ccm itawale milele na tumechoka na kelele za debe tupo kwa kauli za kijinga eti 'tunalaani'

Na katika hili ni lazima ijulikane wazi sadaka ya damu za watu ni lazima ili kumlazimisha mtu jeuri kama huyu mungu wa Tanzania atake au asitake ni lazima atasalimu amri na kufuata matakwa ya umma.

Tumechoka na siasa za kulalamika wakati wenzenu tayari wameshapanga safu ya 2020 (Wakurugenzi)kama hali ni hii hii mimi sintojisumbuwa kupiga kura na viongozi wa upinzani wakae wakijuwa wataanguka vibaya kwa sababu watu wote tusiopenda upuuzi hatutokuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi wa maigizo.

Mimi siwezi kumpigia kura mgombea ambaye hana hata wakala wa kuhakikisha kura yangu inahesabiwa je kuna umuhimu wa kupiga kura.

Amueni sasa, lianze vuguvugu sasa au mkae kimya daima mle tu ruzuku mnayoipata ili kuwazuga wazungu kwamba Tanzania tuna mfumo wa vyama vingi.
Upinzani wa Tanzania umejaa mamluki kibao wanaoendeshwa na njaa ya madaraka, na hili linazidi kuwa wazi kadri siku zinavyoenda.

Huu upinzani tulionao tayari unaelekea ICU na kinachoupeleka huko ni wapinzani wenyewe wanaonekana wameshindwa kumaliza tofauti zao ndani ya chama sasa nikukomeshana tu kwa usaliti.

Nashawishika kuamini hata katiba mpya nzuri ikiwepo kwa huu upinzani unaoelekea shimoni hakuna jipyaa litakalotekea.
 
Nitawaona wajinga kama watasubir huruma ya rais wakat na yeye anajenga chama chake kwa nguvu ya dola...
Bila tume huru waache tu siasa ccm ni wajinga hakuna mfano na tume hii ndio kiongoz wao
 
Haki hailetwi kwenye sahani, haki inapiganiwa. Viongozi wa upinzani ondoeni woga, nchi hii ilivyo kwa sasa inahitaji uana harakati, tena wanguvu. Nakumbuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 palitokea harakati, maandamano na mikutano mpaka serikali ikaanza kulia na kulalamika. Hilo ndilo linalotakiwa, achaneni na slogan za kulinda amani. Mwambieni Lowasa huko ni upinzani.

Hivi ni mara ngapi Tundu Lissu amedai na kukumbushia mchakato wa Katiba Mpya uliouliwa na JPM? Wananchi walimsapoti? Si walimwacha aonekane kana kwamba ni yeye tu anadai Katiba Mpya ila wananchi hawana shida na hiyo iliyopo? Na kwa sababu hiyo, walitoa urahisi kwa wenye mamlaka "kumshughulikia" Lissu as an individual. Wa kulaumiwa kwa hali ya siasa hapa nchini ni wananchi wenyewe. Kulaumu viongozi wa upinzani ni kukwepa majukumu kama wananchi wa nchi hii. Kazi ya viongozi wa upinzani ni ngumu mno kwa kuwa wananchi hukaa kimya pale ambapo mambo ya msingi yanaibuliwa na viongozi hao. Nakumbuka miaka ya nyuma John Mnyika alikuwa akihamasisha watu kudai huduma bora ya maji Ubungo. Hakupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wakazi wa Ubungo kana kwamba shida ya maji aliipata Mnyika peke yake.

Na nikukumbushe tu kuwa kwa sasa mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na Rais. Na wanaodai haki hiyo ni viongozi wa upinzani peke yake. Wananchi wako kimya kana kwamba katazo hilo ni halali.
 
Wamdai nani? Yaani tuwasaidienu kupata nguvu za kututoa? Hamuwezi kuwa serious, halafu kudai kwenyewe mnadai kiulauni kama mlenda au ndizi iliyoiva.
Mbaya zaidi viongozi weny wa upinzani mmeweka watu wenye hofu ya kupoteza vingi, umewahi kuona wapi uongozi wa aina ukafanikisha jambo? Unadhani Mugabe alikuwa ni Tajiri mpaka kufikia pale? Mandela? Nyerere? Hao wote hawakuwahi kuuza hata sindano lakini nyuma yao kulikua na matajiri na wafanya biashara wasioonekana.
Hiyo tabia ya siasa za kuhongwa na wanaotaka madaraka ndiyo zimepelekea watu wenye uwezo kifedha na wafanyabiashara ndiyo wajae kwenye uongozi wa kisiasa matokeo yake wanapohitaji kuongoza mabadiriko ya kweli wanajawa na hofu ya kupoteza vingi.
Mfano CHADEMA leo hii ingekuwa na vijana zero brain fulani na waliochoka kabisa kimaisha na wasio na cha kupoteza halafu mkawaweka hao kwenye uongozi, mngeona mtiti wake, kwa mseto huo nchi ingenyooka tu hii.
Hao vijana ndiyo wangekua wanaongoza vyama halafu serikalini ndiyo mnapeleka hao wasomi wenu. Nawaapieni mngeuona mziki wake.
Lakini kwa mtindo huu wa kuwakabidhi chama hao wafunga tai wenu wenye madili kibao mjini na biashara kadhaa, mtasubiri sana. Huu ni ushauri nimewapeni msingeupata popote pale. Tambueni kuwa nchi yetu bado ina jungle leaders, nchi yenye rais kama tuliye naye sasa anatakiwa kukabiliana na watu wehu siyo watu smart. Na yeyw kwa kuwaogopa wehu wenzake au waliomzidi na wasiohofia chochote ndiyo maana akaanza kwa kum neutraluze Prof. Lipumba kwanza

Hichi ndio sahihi kwa Upinzani. Wewe unampa Sumaye awe kiongozi wa Kanda ya Pwani wakati amepora Mashamba Kibao au unampa Dr Feki Makongoro Mahanga eti mwenyekiti wa CHADEMA Ilala halafu unategeme Mabadiliko? CHADEMA Msipofukuza Lowassa, Sumaye, Makongoro Mahanga na Vibaka wengine hamtakaa mrudishe imani ya Chama kwa Watanzania Tena
 
Kwa kauli hii, mkuu unakubali katiba tuliyonayo haifai??? Na aliyepo kutuambia katiba si kipaumbele chake ina maanisha anataka kufaidika na mapungufu ya katiba iliyopo??? Kupitia katiba mpya, tume huru ya uchaguzi itapatikana na kama taifa tutakua tumepata faida. Bila kujali vyama, wote tuwe na nia njema ya kupata katiba mpya na hatimaye tume huru ya uchaguzi. Bila hivi vitu, wapiga kura watazidi kupungua na kama ndivyo, tuiache CCM iendelee na wananchi tuendelee na mambo yetu. Kwa mwendo huu, 2020 uchaguzi utaweka historia ya aina yake.
Ni kuwakumbusha tu kua akili zenu ni za kuku mtu yule mnayajua mabaya yake mengi aliyoyatenda amejigeuza ngozi nanyi mmesahau mnamuona mwenzenu swali je ana nia ya dhati!
 
Sina mengi wala nisiwachoshe akili, ni wazi kama kuna upinzani wa kweli nchi hii basi tuache yote lianzishwe vuguvugu la kudai katiba mpya sasa na tume huru ya uchaguzi au kinyume chake wote tutulie tuiache ccm itawale milele na tumechoka na kelele za debe tupo kwa kauli za kijinga eti 'tunalaani'

Na katika hili ni lazima ijulikane wazi sadaka ya damu za watu ni lazima ili kumlazimisha mtu jeuri kama huyu mungu wa Tanzania atake au asitake ni lazima atasalimu amri na kufuata matakwa ya umma.

Tumechoka na siasa za kulalamika wakati wenzenu tayari wameshapanga safu ya 2020 (Wakurugenzi)kama hali ni hii hii mimi sintojisumbuwa kupiga kura na viongozi wa upinzani wakae wakijuwa wataanguka vibaya kwa sababu watu wote tusiopenda upuuzi hatutokuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi wa maigizo.

Mimi siwezi kumpigia kura mgombea ambaye hana hata wakala wa kuhakikisha kura yangu inahesabiwa je kuna umuhimu wa kupiga kura.

Amueni sasa, lianze vuguvugu sasa au mkae kimya daima mle tu ruzuku mnayoipata ili kuwazuga wazungu kwamba Tanzania tuna mfumo wa vyama vingi.
Mkuu unaamini Tanzania kuna upinzani?........ Kilichopo hapa ni kanyaboya tu ndio maana Prof Lipumba ameona huu ni ujinga bora " ajitafunie" ruzuku tu!
 
Upinzani wa Tanzania umejaa mamluki kibao wanaoendeshwa na njaa ya madaraka, na hili linazidi kuwa wazi kadri siku zinavyoenda.

Huu upinzani tulionao tayari unaelekea ICU na kinachoupeleka huko ni wapinzani wenyewe wanaonekana wameshindwa kumaliza tofauti zao ndani ya chama sasa nikukomeshana tu kwa usaliti.

Nashawishika kuamini hata katiba mpya nzuri ikiwepo kwa huu upinzani unaoelekea shimoni hakuna jipyaa litakalotekea.
Sasa mtu kama Mbowe eti ndiye kiongozi wa upinzani tena hadi bungeni.......yaani full vichekesho!
 
CHADEMA ilijengwa na Dr. Slaa............Mbowe hajawahi kujenga chama hata siku moja.....Slaa alivyoondoka na chama kimekufa.........uchaguzi ujao 2020 ndio tunaizika CHADEMA rasmi
Na ukiizika cdm ndio itakuwa furaha yako?elewa maisha bila kujishindanisha sio maisha,inaonekana system iliyopo imekunufaisha maadamu wewe na watoto wako mpo poa u don't take a dam yanayotokea pale lingusenguse,yes ccm itatawala ila nakuhakikishia sio milele,generations zenye kujaribu zinakuja sio hii ya mimi na wewe iliyojaa unafiki,woga ,na njaa,mfano wa kubomoa jengo la Tanesco lilitakiwa lifuate sheria sio shinikizo kutoka kwa no 1,wanasheria wa tanesco wapo nini kimewafanya wasipeleke kesi mahakamani ni woga na njaa;na ninakuhakikishia kuwa kubomelewa kwa jengo lile hakutatatua msongamano wa magari jijini,kuwa na public transport na kuwaelimisha watu kutumia usafiri huu,lift clubs,underground trains(tubes) etc etc ,sio mihemko hii;ila time itakuja kutupa ukweli.
 
Kwa nyakati hizi, wananchi hawaangushi upinzani, viongozi wa upinzani wanawaangusha wa Tanzania. Watanzania wameshawaelewa Upinzani, na wako tayari kuchagua upinzani na kuiangusha CCM, ila shida ipo kwenye mfumo, tume ya uchaguzi, MABADILIKO YA KATIBA NI YA LAZIMA.

Viongozi wako kwenye mazingira mazuri zaidi yetu sisi kuililia katiba iliyopendekezwa, sio kuja kulialia huku mtaani na kutaja taja Mungu. Mungu kawapa akili, nguvu, uongozi na afya Njema, pambaneni huko bungeni kuhusu katiba.

Viongozi wa chama waoga hatari chadema inakufa muda sio mrefu kiukweli sitapiga kura tena kuondoa mfumo uliopo sasa pengini kifanyike kitu kama kilichofanyika Zimbabwe kinyume na hapo tutajichosha kutegemea vyama uchwara
 
Kuwa na katiba ninjambo moja lakini kuifuata ni jambo jingine. Nilichotambua hapa ni kuwa hata hii iliyopo wenye mamlaka hawataki kuifuata je ikitengezwa mpya mambo yatakuwaje naweza kusema inaweza isifuatwe lakini mchakato nao unaweza kuzalisha katiba mbaya zaidi ya hii ili kuwabeba watawala na interest zao.
 
Sina mengi wala nisiwachoshe akili, ni wazi kama kuna upinzani wa kweli nchi hii basi tuache yote lianzishwe vuguvugu la kudai katiba mpya sasa na tume huru ya uchaguzi au kinyume chake wote tutulie tuiache ccm itawale milele na tumechoka na kelele za debe tupo kwa kauli za kijinga eti 'tunalaani'

Na katika hili ni lazima ijulikane wazi sadaka ya damu za watu ni lazima ili kumlazimisha mtu jeuri kama huyu mungu wa Tanzania atake au asitake ni lazima atasalimu amri na kufuata matakwa ya umma.

Tumechoka na siasa za kulalamika wakati wenzenu tayari wameshapanga safu ya 2020 (Wakurugenzi)kama hali ni hii hii mimi sintojisumbuwa kupiga kura na viongozi wa upinzani wakae wakijuwa wataanguka vibaya kwa sababu watu wote tusiopenda upuuzi hatutokuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi wa maigizo.

Mimi siwezi kumpigia kura mgombea ambaye hana hata wakala wa kuhakikisha kura yangu inahesabiwa je kuna umuhimu wa kupiga kura.

Amueni sasa, lianze vuguvugu sasa au mkae kimya daima mle tu ruzuku mnayoipata ili kuwazuga wazungu kwamba Tanzania tuna mfumo wa vyama vingi.
Wakati ni Sasa kwani uwezo wanao mkubwa kupitia wafuasi na tasisi mbalimbali za kijamii. Hiki ndicho kipindi muhimu kuliko vyote. Ee Mwenyezi Mungu naomba uwaondolee roho ngumu ktk hili
 
Na ndio kipimo cha kuwapima kwamba akili zao zipo kwenye ruzuku tu au ni movement 4 change kweli?
Mkuu Ruzuku inapigwa pini soon.Sheria ishaandaliwa inapelekwa bungeni kwenye seating ijayo
Ruzuku itatolewa kutokana na maamuzi ya waziri wa wizara husika kutokana na hali ya kipesa ya serikali

Kibano kingine vyama vya siasa

upload_2017-11-28_9-33-8.png
 
Sabalkheri na masalkheri mabibi na mabwana popote pale mlipo kwenye pembe ya dunia hii.

Natumai nyote mna na mmekuwa na Jumapili njema kabisa kama ilivyo kwangu.

Baada ya salamu ngoja nizame sasa kwenye hoja ya mada husika.

Tayari kuna minong'ono ya hapa na pale iliyoanza kusikika kuhusu nani labda atagombea urais kupitia kile chama kikubwa cha upinzani au kupitia mwamvuli wa UKAWA.

Jambo ambalo linanishangaza ni ukimya wa vyama vya upinzani kuhusu chombo kinachoendesha na kusimamia chaguzi zetu, tume ya taifa ya uchaguzi.

Wengi tunajua jinsi ambavyo uongozi wa hicho chombo unavyoundwa. Na naamini tupo kadhaa ambao hatuna imani kivile na hicho chombo kutokana na ukweli kuwa huwa kinaundwa na rais aliyeko madarakani na ambaye mpaka sasa amekuwa ndiyo mwenyekiti wa chama tawala cha CCM.

Kwa mtaji huo, baadhi yetu huona dosari iliyopo katika muundo mzima wa hicho chombo. Binafsi naamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/ mwenyekiti wa CCM huwa anaweka makada wa chama chake pale ili kulinda na kuhifadhi maslahi ya chama chake endapo ikibidi kufanya hivyo.

Tayari tumeshaona aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume hiyo hapo zamani, Jaji Agustino Ramadhani, alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM. Huyu mtu mimi naamini hata alipokuwa makamu mwenyekiti wa hiyo tume ya uchaguzi, pia alikuwa kada wa chama chake kwa wakati huo huo.

Sasa sijui hivi vyama vyetu vya upinzani vimejipangaje kuhusu hilo suala la tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inayoundwa na mtu mmoja, tena mtu mwenyewe ndiye mwenyekiti wa chama tawala na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama chake, haiwezi kuwa huru hata kidogo.

Haiwezi kuwa huru kwa sababu ina wiwa [beholden] na shukurani kwake yeye huyo aliyeiunda.

Mimi ningependa kuona vyama vya upinzani vikisusia kabisa chaguzi kuu zote zijazo hadi hapo tutapokuja na njia ya kuunda chombo kilicho huru cha kuendesha na kusimamia chaguzi zetu.

Kinyume na hapo, wapinzani daima watakuwa wanainsindikiza CCM ikulu halafu baadaye watajifanya kuyasusia matokeo, kutokumtambua rais, na mwisho wao wenyewe kuachia msimamo wao na kumkubali rais aliyepo ikulu.

Sioni kabisa sababu ya kushiriki chaguzi ambazo zinasimamiwa na chombo kisicho huru. Kwa jinsi ilivyo sasa hivi, wapinzani kamwe hawatoiona ikulu. Hata uwingi wa wabunge watauona kwa CCM tu.

Tume ya taifa ya uchaguzi iliyopo sasa hivi haipo kwa ajili manufaa ya Watanzania wote. Ipo kwa ajili ya manufaa ya CCM. Hivyo ndivyo niaminivyo.

*Angalizo*

[Kuwa na tume huru ya uchaguzi haimaanishi moja kwa moja kuwa CCM itashindwa na wapinzani watashinda kwenye chaguzi kuu. Tunachotaka baadhi yetu ni kuwa na tume huru inayoaminika.]
HOJA SIYO TU KUSUSIA UCHAGUZI BALI TUWE NA CHAMA KIMOJA IJULIKANE WAZI. TUACHE HAYA MAZINGAOMBWE YA VYAMA VINGI AMBAVYO KIMSINGI HAVIPO.
 
Back
Top Bottom