Unachopswa kuandika hapa, sema umeanza kuifuatilia Chadema kipindi Dr Slaa akiwa katibu.hao wakina Mtei ni waanzilishi wa chama mkuu lakini alieipa CHADEMA nguvu ni dr. slaa baada ya kuibua hoja nyingi za madudu ya serikali...........hata TLP, NCCR zina waanzilishi wao lakini sio maarufu kama CHADEMA..........toka slaa aondoke na umaarufu wa chadema umeisha
h
umenena kweli mtu kama Lowasa ana madudu mengi hawezi fanya chochote anaogopa kufilisiwa mali zake alizozipata kwa kupiga madiliWamdai nani? Yaani tuwasaidienu kupata nguvu za kututoa? Hamuwezi kuwa serious, halafu kudai kwenyewe mnadai kiulauni kama mlenda au ndizi iliyoiva.
Mbaya zaidi viongozi weny wa upinzani mmeweka watu wenye hifu ya kupoteza vingi, umewahi kuona wapi uongozi wa aina ukafanikisha jambo? Unadhani Mugabe alikuwa ni Tajiri mpaka kufikia pale? Mandela? Nyerere? Hao wote hawakuwahi kuuza hata sundano lakini nyuma yao kulikua na matajiri na wafanya biashara wasioonekana.
Hiyo tabia ya siasa za kuhingwa na wanaotaka madaraka ndiyo zimepelekea watu wenye uwezo kifedha na wafanyabiashara ndiyo wajae kwenye uongozi wa kisiasa matokeo yake wanapohitaji kuongoza mabadiriko ya kweli wanajawa na hofu ya kupoteza vingi.
Mfano CHADEMA leo hii ingekuwa na vijana zero fulani fulani na waliochoka kabisa kimaisha na wasio na cha kupoteza halafu mkawaweka hao kwenye uongozi, mngeona mtiti wake, nchi ingenyooka tu hii.
Hao vijana ndiyo wangekua wanaingoza vyama halafu serikaluni ndiyo mnapeleka hao wasomi wenu. Nawaapienu mngeuona mziki wake.
Lakuni kwa mtindo huu wa kuwakabidhi chama hao wafunga tai wenu wenye madili kibao mjuni na biashara kadhaa, mtasubiri sana. Huu ni ushauri nimewapeni msingeupata popote pale.
Ni kweli upinzani unajengwa na sisi wananchi lakini ni baada ya kuwa na kiungo mzuri wa kuwaunganisha ili umoja huo wa wananchi upatikane. Wananchi hawawezi kujiunganisha wenyewe na kuanzisha vuguvugu kama hakuna kiuongo. Chadema kwa sasa sidhani kama ni chama tena chenye uwezo wa kuwaunganisha wananchi kama ilivyokuwa hapo awali kwani dalili zote zinajionesha kuwa kadri siku zinavyokwenda wananchi wanakata tamaa na Chadema na hata ile nguvu ya umma iliyokuwepo haipo tena leo. Leo hii mfano pale Arusha ile nguvu ya LEMA ya kuhamasisha watu kujitoa kwa lolote haipo tena, vivyo hivyo kwa Mwanza na hata DSM pia. Kidogo nguvu imebaki Mbeya ambayo nayo soon itapotea kabisa. Ni muhimu sana Chadema kama wanataka kukinusuru chama basi wachague agenda moja ya kwenda nayo sio ingine ni kupambana kulqzimisha mifumo huru ya uchaguzi kwani bila hivyo hakuna mwananchi mjanja atawapa kura yake na wakati anajua kura hiyo itaporwa kwa mabavu ya nguvu za dolaKwani mnapozungumzia "upinzani" huwa mna maanisha nini !? Siwaelewi.
Upinzani unajengwa na sisi wananchi wala sio bendera ama rangi za sare za vyama.Ka ma sisi wananchi hatuoni umuhimu wa kujiunga nao ama kusimama upande huo,hatutaki kuwa sehemu yake kamwe hakuna upinzani.
Tuache hii tabia ya kuamini kuna aliyepewa jukumu la kuupa nguvu upinzani na sisi kujiweka kando...
Kama kweli tunachukizwa na tunayotendewa na watawala,tuondoe woga,ubinafsi na unafiki...TUJIUNGE UPINZANI.
Vinginevyo kaa kimya,ufyate.
watanzania wengi hawakuwapenda wakina zitto kwa sura zao bali kwa hoja zao.........Zitto alipata umaarufu baada ya kuibua hoja ya buzwagi hii ndio imemtoa........Sugu na Mnyika siwezi kuwazungumzia hawa walipata ubunge baada ya CHADEMA kupata umaarufu Dr. Slaa ndio alieipa umaarufu CHADEMAUnachopswa kuandika hapa, sema umeanza kuifuatilia Chadema kipindi Dr Slaa akiwa katibu.
Waulize Mnyika, Zitto Kabwe na Sugu na wengineo wengi ni nani sliwaleta Chadema?
usimfananishe Zito na akina Mnyika na Sugu..........Zitto amehama chama na bado ubunge amepata......Leo Mnyika na Sugu wakihama CHADEMA ubunge watausikia redioni tuMimi siyo Chadema lakini huijui Chadema kaa kimya.
Tangu vikao vya kuianzisha Chadema kwa siri vikao vilikuwa vinafanyika Masaki kwa Mzee Kimesera na kina Mtei Mbowe alikuwa ndio karani wao, Dr Slaa alikuwa bado anakula sadaka za waumini kanisani na alikuwa na kadi ya ccm.
Ukitaka kujuwa chama kinajengwaje muulize Zitto Kabwe leo na ACT yake, maana hata Zitto alikuwa anaamini yeye ndio kaijenga Chadema na siyo Chadema imemjenga yeye.
Kabla ya Jubilee ni chama gani kilikuwa madarakani na upinzaniTokea kenya wamepata katiba mpya yenye kurasa zaidi ya 1,000 upinzani haujagusa ikulu
Kwa wasanii na wapigaji hawa tulionao,hata ije katiba gani hawataiona ikulu
Kabla ya Jubilee ni chama gani kilikuwa madarakani na upinzaniTokea kenya wamepata katiba mpya yenye kurasa zaidi ya 1,000 upinzani haujagusa ikulu
Kwa wasanii na wapigaji hawa tulionao,hata ije katiba gani hawataiona ikulu
Alietegemea ccm ipo mfukoni mwake kumbe ccm ni taasisi kubwa yenye wabobezi,huyo ndie kati ya waliovuruga mchakato kwa kuzani angepewa nafasi ya kugombea urais ili aitumie katiba hii hii kuwakandamiza wapinzani na kuiibia nchi kama wanavyodai!Mchakato ulivurugwa na nani? Naomba nipe elimu.
Kwa kauli hii, mkuu unakubali katiba tuliyonayo haifai??? Na aliyepo kutuambia katiba si kipaumbele chake ina maanisha anataka kufaidika na mapungufu ya katiba iliyopo??? Kupitia katiba mpya, tume huru ya uchaguzi itapatikana na kama taifa tutakua tumepata faida. Bila kujali vyama, wote tuwe na nia njema ya kupata katiba mpya na hatimaye tume huru ya uchaguzi. Bila hivi vitu, wapiga kura watazidi kupungua na kama ndivyo, tuiache CCM iendelee na wananchi tuendelee na mambo yetu. Kwa mwendo huu, 2020 uchaguzi utaweka historia ya aina yake.Alietegemea ccm ipo mfukoni mwake kumbe ccm ni taasisi kubwa yenye wabobezi,huyo ndie kati ya waliovuruga mchakato kwa kuzani angepewa nafasi ya kugombea urais ili aitumie katiba hii hii kuwakandamiza wapinzani na kuiibia nchi kama wanavyodai!
Kumbe wewe kichwani ni hewa tupu, sina muda wa kujibizana na wewe kama akili yako inaamini Zitto amepata umaarufu kwenye kashfa ya Buzwagi, hii inamaanisha hukuwahi kumjuwa Zitto kabla ya Buzwagi.watanzania wengi hawakuwapenda wakina zitto kwa sura zao bali kwa hoja zao.........Zitto alipata umaarufu baada ya kuibua hoja ya buzwagi hii ndio imemtoa........Sugu na Mnyika siwezi kuwazungumzia hawa walipata ubunge baada ya CHADEMA kupata umaarufu Dr. Slaa ndio alieipa umaarufu CHADEMA
Hakuna sababu ya kushiriki mechi ambayo refa ni wao na uwanja ni wao, ukinyimwa goli au penati utamlaumu nani?Kung'ang'ania uchaguzi bila katiba wala tume huru ni kupoteza mda na kuumiza watu na kutia watu vilema. Lakini mbele ya dictotor huyu sio kazi rahisi. Sasa tupeane mbinu za kudai katiba katika utawala wa namna hii
Wamdai nani? Yaani tuwasaidienu kupata nguvu za kututoa? Hamuwezi kuwa serious, halafu kudai kwenyewe mnadai kiulauni kama mlenda au ndizi iliyoiva.
Mbaya zaidi viongozi weny wa upinzani mmeweka watu wenye hofu ya kupoteza vingi, umewahi kuona wapi uongozi wa aina ukafanikisha jambo? Unadhani Mugabe alikuwa ni Tajiri mpaka kufikia pale? Mandela? Nyerere? Hao wote hawakuwahi kuuza hata sindano lakini nyuma yao kulikua na matajiri na wafanya biashara wasioonekana.
Hiyo tabia ya siasa za kuhongwa na wanaotaka madaraka ndiyo zimepelekea watu wenye uwezo kifedha na wafanyabiashara ndiyo wajae kwenye uongozi wa kisiasa matokeo yake wanapohitaji kuongoza mabadiriko ya kweli wanajawa na hofu ya kupoteza vingi.
Mfano CHADEMA leo hii ingekuwa na vijana zero brain fulani na waliochoka kabisa kimaisha na wasio na cha kupoteza halafu mkawaweka hao kwenye uongozi, mngeona mtiti wake, kwa mseto huo nchi ingenyooka tu hii.
Hao vijana ndiyo wangekua wanaongoza vyama halafu serikalini ndiyo mnapeleka hao wasomi wenu. Nawaapieni mngeuona mziki wake.
Lakini kwa mtindo huu wa kuwakabidhi chama hao wafunga tai wenu wenye madili kibao mjini na biashara kadhaa, mtasubiri sana. Huu ni ushauri nimewapeni msingeupata popote pale. Tambueni kuwa nchi yetu bado ina jungle leaders, nchi yenye rais kama tuliye naye sasa anatakiwa kukabiliana na watu wehu siyo watu smart. Na yeyw kwa kuwaogopa wehu wenzake au waliomzidi na wasiohofia chochote ndiyo maana akaanza kwa kum neutraluze Prof. Lipumba kwanza