mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Kupishana kauli ama kuwa na mitazamo tofauti juu ya jambo ama kitu fulani, ni kitu kizuri mno. Na wala hii haiwezi kuchukuliwa kama fukuto ama ugomvi katika ya viongozi hawa wa juu wa CDM.
Jambo lenye afya kwa chama ni kukubali kutofautiana kwa ajili ya maslahi mapana ya chama. Chama chochote kile ndani yake ni lazima kuwe na makada wahafidhina pamoja na wale wenye msimamo wa kati. Kwa hiyo basi kinapotokea ama kuibuka kitu ndani ya chama makundi haya mawili hayaachi kupishana kauli.