Raia Mwema: Safari ya Halima Mdee na wenzake kuelekea ACT Wazalendo yaiva

Raia Mwema: Safari ya Halima Mdee na wenzake kuelekea ACT Wazalendo yaiva

Limeandika gazeti la Raia Mwema

View attachment 2525867

Pia niliiona tweet Ya Halima Mdee kule Twitter. Na baadae nikaikumbuka tweet ingine ya Mdee hukohuko Twitter.

Ndio nikaelewa kinachokuja kutokea 2025. Ni kwa mantiki hiyo, ndio nimeona kazi kubwa watakayokuwa nayo Chadema, pale itakapofika 2025.

Huku kutakuwa na CCM. Kwingine kutakuwa na wafuasi wa Magufuli. Na huku kutakuwa na Mliowaita COVID-19!

Halafu Zitto na ACT yake inaendelea kuwabinya taratibu muda wote. Hii ikiwa ni kabla hata ya 2025.

Ndio maana nikaja na jibu kwamba CHADEMA mtafika 2030 mkiwa hoi bin taaban baada ya mapambano hayo makali.

Siasa haina adui wa kudumu.
Halima na wenzake hawana chaguo jingine zaidi ya kwenda ACT au chama kingine cha upinzanj.

1) CHADEMA walikwishafukuzwa, hawatakiwi.

2) CCM aliyewapa ubunge alikwishafariki, na mlinzi wao kafukuzwa uspika, na ndani ya CCM, zile siasa za udikteta wa mtu mmoja zimepungua sana kiasi cha kutowapa uhakika wakienda huko watapata hata nafasi ya kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge.

Lakini kwa vyovyote, nafasi yao ya kuupata ubunge kwa njia halali ni finyu sana.

Kwa upande wa CHADEMA,nafasi yao ya kushinda majimbo mengi ya uchaguzi, hasa maeneo ya mijini, alimradi wawe na wagombea makini, ni kubwa kuliko chama chochote.
 
Back
Top Bottom