Ndugu yangu
TUJITEGEMEE, kweli uvumilvu una mwisho...sikutegemea kabisa hata wewe kuna siku utaonesha kuishangaa serikali ya CCM na kukiri uovu kama huu dhidi ya Watanzania wenzako.
Anayedai kuwa na PhD ya heshima katika uchumi katu hawezi kubuni wizi kama huu dhidi ya wananchi ambao amebahatika kuwa kiongozi wao.
La pili hizo pesa zilizopatikana kwa njia hii ambayo hata yeye baada ya kuzidiwa hoja kakiri pengine haikuwa halali, je tulioibiwa tutarudishiwa?
Mtaalamu wa uchumi mwenye PHD hawezi kukata eti tozo kwenye akiba iliyo benki. Benki ndiyo inatakiwa imlipe faida kwa kutumia pesa zake kama mtaji.
Mtaalamu wa uchumi mwenye PhD hawezi kukata tozo kwenye hela iliyokatwa kodi zaidi ya mara moja, huo ni wizi na hata sheria za kodi haziruhusu kamwe.
Mtaalamu wa uchumi mwenye PhD hawezi kukosa uzalendo kwa taifa lake na kuwatishia wananchi ambao ndio walipa kodi wahamie Burundi kama wanahoji tozo.
Mtaalamu wa uchumi mwenye PhD, anayethubutu kubuni mbinu chafu kama alivyofanya Mwigulu, ni kuvuliwa hiyo PhD yake ya heshima na kuchunguzwa aliipataje?