Raia wa Kawe kupigwa kininja na MPs wa kambi ya Lugalo walaumiwe Polisi kwa kukaidi kumkabidhi muuaji Kato kwa hao MPs

Nchi ina Katiba na Sheria zake sasa kwanini wamkabidhi huyo mtuhumiwa wakati Jeshi la polisi tayari limetimiza wajibu wa kuumpata mtuhumiwa kinachofuata ni Mahakama kufanya yake mleta mada unahalalisha haramu kuwa kuwa halali ili watu waone ni kawaida eti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata maandiko yamesema kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, malipo ya dhuluma ni kifo, kila mmoja wa hao MPs hio dhuluma itamuua na kutesa vizazi vyao vyote
 
Inchi hai operate kwa namna hiyo polisi wanamkabidhije kato kwa wanajeshi?Ni kato ni mwanajeshi kwamba ataenda kuhukumiwa kijeshi. Kinachofanywa na mps ni kuisafisha hilo eneo na hakuna njia nyingine ni kama kinachofanyika gaza tu wacha wawachuje mtaakaa kwa amani badae
 
Kaka kazi ya jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao na kazi ya jeshi la wananchi ni kulinda mipaka ya Nchi. Jeshi halina mamlaka ya kuingilia kazi ya polisi. Kwani raia wana mahakamani zao na jeshi wana mahakama zao. Mtuhumiwa ni raia lazima akamatwe apelekwe polisi hatua nyingine zifuate.
 
Wewe naye sijui umekunywa ulanzi asubuhi yote hii
Wamkabidhi kwa jeshi kwa sheria ipi?
Hilo ni jukumu la polisi hao wajeda washenzi wasiokuwa na akili ilitakiwa watulie huko kambini kwao
Na hao wakubwa wao vikosini wanawaendekeza askari wao kutumia nguvu uraiani kupiga watu ovyo.
 
Hii ni akili au matope, kosa la wananchi hapo ni nini?
Kwanza hiyo ni kesi ya kiraia police ndio wanahusika, lakini kubwa kuliko zote raia hawajamshikilia huyo muuwaji bali ni polisi, kama ndiyo hivyo, basi jeshi wakawatwange polisi.

Huu ni muendelezo wa tabia mbovu za wajeda kujifanyia MAKAME NGUVU.
 
Jaribu kutumia akili wewe!! Kwa mawazo haya ndio maana ccm wanawaona wananchi wote wa nchi hii ni HAMNAZO!! Polisi walitimiza jukumu lao la kikatiba, huo ni ushamba tu!! Mala ngapi hata inapotokea mwanajeshi amepigwa/ibiwa na wakamkamata mhusika, lakini bado wakapiga raia?!!
 
Wale ni maninja sio wajeshi, uthubutu wa Raia kumdhuru mwanajeshi bila onyo kali tena onyo mtambuka Raia hamuwezi kujirekebisha, sasa huo ni mfano tu, in an event of a similar scenario please just get away far away that place please kindly thank me later.
 
Jihadhari ni mwiko Raia kwa namna yoyote ile kumgusa pot jua hivyo, akikukosea chukua namba zake au ya gari yake nenda Kambini kashitaki nenda na barua ya mtendaji.
 
Wewe naye sijui umekunywa ulanzi asubuhi yote hii
Wamkabidhi kwa jeshi kwa sheria ipi?
Hilo ni jukumu la polisi hao wajeda washenzi wasiokuwa na akili ilitakiwa watulie huko kambini kwao
Wakikabidhiwa wanaweza wakamuua kifo kibaya kupitia adhabu kali watakayompa itakayopelekea afe kifo chenye maumivu makali
 
Kwa hiyo Katoto aliuwa mjeda?


Kama Polisi walishamkamata mtuhuhumiwa Mambo ya kupiga raia yanatoka wapi?
 
Wachangiaji muwe makini sishabikii ila nimeweka kitu fulani aina ya reciprocal opportunity to action
Kama katiba haiheshimiwi waTz pona yetu ipo pale ambapo tutapata viongozi wenye busara ya asili.

Mwenyezi Mungu atuepushe na watu kama wewe kwenye uongozi, imagine mtu anayeona walichofanya hao wajeda ni sawa 🗑️🚮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…