FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Neno "Uislam" linamaanisha "kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu."kwani uislamu ni nini?
Wafuasi wa Uislam wanaitwa Waislam.
Waislam wanaamini Mungu mmoja na wanaabudu Mungu mmoja, ajuaye yote, hajazaa waka kuzaliwa na hafanani na yeyote/ chochote ambaye kwa Kiarabu anajulikana kama Allah.
Wafuasi wa Uislam wanalenga kuishi maisha ya kujisalimisha kikamilifu kwa Allah (Mwenyezi Mungu). Wanaamini kwamba hakuna kitu kinachoweza kutokea bila idhini ya Allah (Mwenyezi Mungu) , lakini wanadamu wana hiyari huru (freewill).