Ni kweli unavyosema kuhusu tatizo la ukabila nchini Kenya. hili ni jambo ambalo alituonya Rais mstaafu Arap Moi kabla kuondoka kwake mamlakani. Hata hivyo, nina kila imani kuwa ndani ya miaka kama 15 hivi, ukabila hautakuwa tatizo tena, ukizingatia mfumo mpya wa serikali.
unafaa kudownload katiba ya Kenya uipitie kwanza. ipate hapa-
The Laws of Kenya
soma sanasana Chapters 11 na 12.
ukiisoma utaelewa katiba ilivyozingatia swala la ukaila kwa kuigawa Kenya katika kaunti 47, kila kaunti ikiwa na serikali yake, ambayo inashugulikia maendeleo katika eneo hilo. Ni vyema pia kuelewa kuwa kaunti zilivyogawwanyika kimsingi ni kulingana na mgawanyiko wa makabila katika maeneo tofauti.
Kaka umenichekesha sana, kwamba baada ya miaka 15 ukabila utapungua, ni sawa na kusema baada ya miaka 20 dini zitatoweka Afrika[emoji1] [emoji1] [emoji1].
Kwanza fahamu kwamba makabila ambayo baadae yamesababisha ukabila, yamekuwepo katika jamii zetu miaka mingi zaidi hata kabla ya hizi dini za kigeni kuja Afrika, na hakuna nchi yoyote duniani yenye tatizo la ukabila kama Kenya iliyofanikiwa kuufuta ukabila ndani ya kipindi cha kizazi kimoja, viwili au vitatu, ni mchakato unaochukua muda mrefu sana, Rwanda pale, usione kumetulia ukadhani ukabila umepungua, ukizungumza na watutsi wanatokota ndani kwa ndani, wanasubiri muda muafaka tu walipize, na vivyo hivyo wahutu.
Kuhusu katiba ya Kenya kuwa inasaidia kupunguza ukabila, kwa nadharia unaweza kusema hivyo, lakini kiuhalisia na hali ilivyo sio kweli hata kidogo, tangu Kenya imeanza kutumia katiba mpya, tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, ukabila na rushwa vimeongezeka zaidi, hii ni kwa sababu madaraka na mfumo wote wa usimamizi ambao ulikuwa katika malamka ya serikali kuu, mengi yamepelekwa katika gatuzi 47, hii pia inamaanisha kwamba sio tu mamlaka na resources zimegawanywa, bali hata uzembe, rushwa, ukabila na wizi pia vimegawanywa na kukua mara 47.
Kumbuka kwamba kitu kinachopiganiwa na muhimu ni urais wa nchi, achana na habari ya Gavana, pamoja na kwamba NASA imezidiwa na Jubilee katika nafasi zote hizo, lakini wamekubali, ila kiti cha rais pekee ndicho kinacholeta shida, kama Kenya mtaondoa kiti cha urais na kubakisha vyeo vya magavana, bunge, na mahakama, haya matatizo yatapungua sana kama sio kumalizika kabisa