Kijakazi inaonyesha si mfatiliaji wa siasa za kenya, ukweli ni kwamba huyo aliye madarakani kama rais hivi sasa anamuunga mkono Kenyata hivyo wajua hata yeye alipata vipi urais wakati alipochukua kwa mara ya pili.
Lakini haitoshi kuna watu wanalalamika kama Odinga ndio alifanya matukio ya vurugu za wenyewe kwa wenyewe uchaguzi uliopita, hili nalo si kweli kwa kuwa si yeye aliye jiweka madarakani ila Mwakibaki hakuna mtu ambaye hafahamu kuwa Odinga alishinda uchaguzi huo ila walichukua nchi kwa nguvu.
Narudi tena kutoa mawazo yangu kwenye siasa za africa na hasa za wenzetu wa kenya, hoja si kushindwa ila unashindwa vipi huwezi kuona karatasi za kura zina peperuka barabarani wakati wa kupiga au kuhesabiwa kura na hata baada ya uchaguzi lakini hili kenya limetokea uchaguzi huu, pia kituo watu 500 wamejiandikisha kupiga kura lakini unakuta waliopiga kura kwenye kituo husika wako 3000.
Mimi na sema mtawala yoyote ambaye ameingia kwa njia ya haramu, basi utawala wake huwa ni washida sana na mifano tunayo hata hapa kwetu nyumbani, hivyo tumaini la wananchi wa kenya kwa kijana litakuwa kama hapa kwetu kwa baba riz one.
Ngoja tuone kwa kuwa utawala wa nchi si kitu kinacho fanyikia chumbani ila ni dhahiri.