Raila Odinga ana hoja,Tume imeteleza. Fomu 34A na 34B zipo kisheria

Raila Odinga ana hoja,Tume imeteleza. Fomu 34A na 34B zipo kisheria

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mgombea wa Urais wa Kenya kupitia NASA,Raila Odinga amejitokeza na kupinga matokeo ya awali ya Urais ya Kenya yanayotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya yakimweka mbele Rais Uhuru Kenyatta.

Hoja ya Odinga ni kukosekana kwa Fomu 34A na 34B zinazopaswa kujazwa na kusainiwa,ikiwa ni pamoja na mawakala, kisheria kabla ya kutangazwa matokeo. Fomu 34A hujazwa na kusainiwa katika Kituo cha Kupigia kura. Kimsingi,Fomu 34A hubeba taarifa za kura za kituo kimoja.

Fomu 34A huwasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo. Taarifa zote za vituo vya Jimbo husika hujazwa kwenye Fomu 34B. Hatimaye,Fomu 34B huwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kutangazwa matokeo rasmi.

Kujazwa kwa Fomu nilizozitaja,ni sharti la kisheria. Lazima kuzijaza na kuziwasilisha. Inataarifiwa kuwa Tume ya Uchaguzi ilitangaza matokeo bila Fomu 34A na 34B. Kwasasa,Tume inakusanya Fomu wakati matokeo yameshatangazwa na kubishiwa.

Hivyo,Odinga ana hoja ya kisheria kuyabishia matokeo hayo. Je,atayapinga matokeo ya Urais kisheria au kisiasa? Matokeo yaliyotangazwa bila fomu husika yanabakije kama halali? Raila Odinga ataamua muda ukifika.Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya,Tume ya Uchaguzi ina siku 7 kumtangaza mshindi wa Urais.
 
Hizi ndizo tume zetu ''huru'' za Uchaguzi!

Tume ''huru'' ya Uchaguzi inatangaza matokeo ya Uchaguzi ''huru'' halafu baadaye inatuambia hayo sio matokeo rasmi ya Uchaguzi!

Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali.

Siku alipouwawa yule mkuu wa kitengo cha teknologia ya habari na mawasiliano kwenye tume ya Uchaguzi, Chris Msando ndio siku ambayo uchaguzi Mkuu ulihitimisha mwanzo wa vurugu za Uchaguzi Mkuu.
 
tume nayo ilikuwa na haraka ya nini kutangaza matokeo bila kusubiri izo form. yale yale ya kibaki kulazimisha atangazwe mshindi bila ya kupata majumuisho ya kura zote.

hawa tume ndo wa kulaumiwa kama kutatokea lolote la hovyo
 
Ebana patamu hapo!.

Lakini tume hii ya uchaguzi si inawabobezi wa hail ya juu katika uelewa?

Nini kilipelekea kutangaza matokeo bila form hizo za kisheria?

Ilikua ni hujuma?
Ndo kiss cha marehemu Cris Musando kuuwawa na kukatwa kiganja?

Damu ya Cris Musando haitakwenda bure kwa unyama waliofanyia kiumbe huyu.

It's matter of time.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndizo tume zetu ''huru'' za Uchaguzi!

Tume ''huru'' ya Uchaguzi inatangaza matokeo ya Uchaguzi ''huru'' halafu baadaye inatuambia hayo sio matokeo rasmi ya Uchaguzi!

Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali.

Siku alipouwawa yule mkuu wa kitengo cha teknologia ya habari na mawasiliano kwenye tume ya Uchaguzi, Chris Msando ndio siku ambayo uchaguzi Mkuu ulihitimisha mwanzo wa vurugu za Uchaguzi Mkuu.

Pamoja na kwamba huwa tunatofautina mambo mengi, kwa hili nakuunga mkono kwa 100%. Sipunguzi wala kuongeza neno bali napigia majibu mstari.
 
aibu kwa Uhuru kula vya kunyonga a.k.a vibudu
 
Tano tena,Muzeya akalee vitukuu tu.Nyota ya urais hana
 
Hadi dk hii tume imeanza kusesabu Manually kura upya...kwa kuzingatia Data za form 34A na 34B.

JPM KAMATA WEZI
 
Hizi ndizo tume zetu ''huru'' za Uchaguzi!

Tume ''huru'' ya Uchaguzi inatangaza matokeo ya Uchaguzi ''huru'' halafu baadaye inatuambia hayo sio matokeo rasmi ya Uchaguzi!

Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali.

Siku alipouwawa yule mkuu wa kitengo cha teknologia ya habari na mawasiliano kwenye tume ya Uchaguzi, Chris Msando ndio siku ambayo uchaguzi Mkuu ulihitimisha mwanzo wa vurugu za Uchaguzi Mkuu.
Ukweli Ambao Upinzani hawataki kuusikia ndio huu.Huwezi kutenganisha tume ya uchaguzi na Uongozi uliopo madarakani kwa nchi zetu hizi.

Raila hawezi kuwa Rais hata kama ameshinda.Ukweli mchungu kwake.
 
Back
Top Bottom