TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Baada ya kushindikana kukutana au kufanya mkutano kwa njia ya video call, hatimaye imefahamika nini kinaendelea chini ya zulia.
Kupitia vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, inaelekea viongozi wa nchi kadhaa za Afrika Mashariki wamekuwa na nia ya kukutana kama siyo kuongea na Rais wa Tanzania JPM ili kujadili issue ya covid-19 bila mafanikio wamekwama.
Kutokana na mkwamo huo, inaonekana viongozi hao kama Museven, Kenyatta na Kagame wamejitahidi kuwasiliana na mkuu lakini bila mafanikio yoyote, hali hiyo imepelekea kupata njia mbadala ya kuwasiliana naye.
Njia iliyopatikana ni kumtumia rafiki wa karibu wa Rais Magufuli ambaye ni Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga ambaye yeye mwenyewe amekili kumpigia simu mara kadhaa lakini bila mafanikio haikuweza kupokelewa.
Lengo la kutaka kufanya maongezi ni kuangalia njia mahususi inayochukuliwa au kuchukuliwa dhidi ya gonjwa hatari linaloendelea kupukutisha binaadamu hapa nchini na nchi za ukanda wa maziwa makuu.
Hata hivyo alichoweza kufanya Odinga ni kuandika ujumbe wa maandishi (sms) na kumtumia Rais Magufuri ili akiupata aweze kuwasiliana naye.