mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Ruto did not attain 50+1 threshold, Azimio says in court papers!
Matokeo ni haya hapa:Last updated: 15/08/2022, 18:59:28 local time (GMT+3)
Final results from IEBC
| Candidates | Vote |
|---|---|
William Ruto 50% | 50.5% 7,176,141 |
Raila Odinga | 48.8% 6,942,930 |
Other Candidates | 0.6% 93,956 |
Asilimia ya Ruto: 7,176,141/14,213,027 x 100 = 50.4899%
Asilimia ya Raila: 6,942,930/14,213,027 x 100 = 48.8491%
Asilimia ya George: 61,969/14,213,027 x 100 = 0.4360%
Asilimia ya David: 31,987/14,213,027 x 100 = 0.2251%
JUMLA YA KURA HALALI: 14,213,027. = 100.0001%
Raila anakiri kuwa Ruto amepata kura 7,176,141 lakini HATAKI kukubali kuwa kura za Ruto ni sawa na asilimia 50.49% kama ilivyotangazwa na tume huru ya uchaguzi wa kenya. Raila anadai kuwa Ruto hajafikisha kigezo cha 50% + 1. Huko ndiko kutapatapa kwani mahesabu yanaonesha kuwa Ruto amepata 50% + 69,629.
BILA SHAKA Raila anandoto za kutaka kuishawishi mahakama ya juu kabisa ya kenya ili IBADILI KATIBA YA KENYA KUHUSU KIGEZO CHA KUWA RAIS WA KENYA KUPITIA KURA. Iko hivi: Kwa sasa mtu anahesabika kuwa ameshinda kama atapata kura 50% + 1 ya KURA HALALI ZILIZOPIGWA (VALID VOTES). Kwa tafsiri ya sasa, kura halali ni zile zinazoonesha KWA WAZI mpiga kura alikuwa anampigia mgombea yupi, kwa hiyo kura yake kuhesabiwa. Raila anataka kubadili TAFSIRI YA KURA HALALI kuwa ni kura zote zilizopigwa hata kama zimeharibika na hazikuhesabiwa kwa mgombea yoyote!! Ukifanya hivyo itapunguza asilimia ya kila mgombea na Ruto hatafikisha hiyo 50%+1. Huko ndiko kutapatapa maana Raila anataka mahakama ikubali kitu ambacho hakikubaliki duniani kote!! Kwa mfano mpiga kura kutokumpigia mgombea yoyote na akatumbukiza kura yake bila chaguo lolote, au anawachagua wagomea wote, hiyo nayo kwa Raila ni kura halali!!