Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

Angejua
 
Mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Odinga anasema kuwa polisi wa Tanzania wanapitia kwenye mafunzo ya kufundishwa utu kwa wananchi...
Hahahaha 😅😂🤣😭
Aiseee!

Aje kuishi hapa kama sisi. Awe wa kawaida. Aandamane, akutwe na kesi za kubambikwa. Hapo tutamuelewa. Au akutwe na madini yenye thamani. Atajuta..
 
Kama mtu alishaishi Kenya haswa na kufahamu vizuri nafikiri atakubali kuwa polisi wa Kenya daaah sijui niseme Nini, actually ukiingia anga zao utajuta kwanini ulizaliwa, wengi siyo friendly kabisa...huku Hadi unatukanana na polisi kabisa.
 
Siku akiwakuta wamepewa oda wa CCM!!
 
Sawa ni sawa na wa ulaya. Je wanaweza kulinda mashabiki wa mpira uwanjani bila kugeuza shingo kuangalia mtanange kwenye pichi?

Ukute polisi wenyewe ni mashabiki wa simba na yanga au timu zao za polisi. Hawa polisi wetu huwa wanaangalia mpira badala ya kuangalia mashabiki
 
Ni kweli, niliwahi ibiwa nyumbani upangajini nika msearch askari ambae tulipanga mpaka mfukoni ananiangalia tu.
 
Msimshangae Odinga, inawezekana kuna ukweli fulani. Kwenye kesi ndogo ndogo wanaweza kukuvumilia tu.

Kwani tumesahau udhaifu wa polisi wetu? Matatizo yao hayapo katika kukamata watuhumiwa hasa wenye kesi ndogondogo. Matatizo yao ni rushwa, wizi, ujambazi na kubambikiana kesi.
 
Katika kuwaponda Polisi wa Kenya kuelekea siku ya Maandamano Makubwa yanayoendelea, Mh Raila Odinga amedai kwamba Polisi wa Tanzania ni waungwana na werevu kama Polisi wa Ulaya na kwamba wakitaka kukukamata wanasema "NDUGU TUNAOMBA TUKUKAMATE"

Hivi kweli jamani hiki alichokisema Odinga ndicho wanachofanya Polisi wa Tanzania?

Toa maoni yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…