Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

By the way...yuko sahihi kabisa..

Ukitii sheria bila shuruti ...unafika mpaka kituoni pasipo kufungwa hata pingu...

Shida inakuja pale unapokaidi tu...na kuwaonyesha kiburi.

Mbona liko wazi kabisa hili.
 
Anaongelea polisi wa Tanzania upande wa Zanzibar.

Ni waungwana Hasa,

Kama huamini nenda kule, likitokea la Kutokea,

Polisi akija atakuomba ukimaliza KAZI zako uende kwenye we kituo Cha polisi wewe mwenyewe.

Kenya si Tanzania unapishana na police karibu, kule polisi na raia ni ni mbalimbali.
 
Wanasiasa ni hatari SANA
Unafiki mwingi
 
Mwambie huyo jamaa asituchefue, polisi walienda kusachi kwenye getho la Dereva bajaji kisa anasadikika alikodiwa kubeba mali ya uwizi wakakuta jamaa ana ki akiba chake cha elfu70 washenzi wakapita nacho, Sasa hao polisi au wezi tu
 
Aise
 
Mwambie huyo jamaa asituchefue, polisi walienda kusachi kwenye getho la Dereva bajaji kisa anasadikika alikodiwa kubeba mali ya uwizi wakakuta jamaa ana ki akiba chake cha elfu70 washenzi wakapita nacho, Sasa hao polisi au wezi tu
Hahahaa njaa tu
 
Japo kuna kaukweli, polisi wa Kenya makatili sana, rushwa kwa kwenda mbele, wa Tanzania hata kama wala rushwa ila utahisi kuna utu wa kiaina.
Weeee, hujaingia kwenye 18 zao, polisi afrika ni KERO kwa raia
 
Nafikiri kwa wale waliozunguka East Africa, Msumbiji, DRC na Zambia watapata picha kweli police wa Tanzania ni waungwana.

Uzuri wao, wanapotaka kukukamata unaweza ukawahoji na wakakupa majibu.

Sio hivyo kwa nchi nyingi, ni uhasama mbele kwa mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…