Malcom Lumumba hii kesi ilishafungwa na muhusika JF mods walimhukumu baada ya kujiridhisha alichotuhumiwa kakifanya kweli. Nimekusoma muda mrefu, nimekuwa mentioned lakini sikutaka kusema chochote.
Wapo rafiki zake wengine walikuja kama wewe na kashfa nyingi lakini mwisho wa siku waliumbuka sasa hivi wamebaki kutumia ID nyingine kuendeleza ujinga.
Ukiona nyani mzee jua kakwepa mishale mingi. Hatutaki kufukua hili kaburi hata alieanzisha hii thread alikuwa ana target watu fulani na kawapata!
Mkuu Rrondo wala usinielewe vibaya kabisa na tusigombane kwa hiki kitu kidogo.
Pengine hukuelewa nilichokisema; nimeuliza watu wanatoa wapi nguvu ya kumuita mtu tapeli ilhali hajawatapeli wao ??
Lengo langu lilikuwa ni kuwakumbusha watu wasikumbilie kuhukumu bila kuwa na ushahidi wa kutosha: Mwiko kufanya hivi.
NB 1: Kuna bandiko liliwekwa hapa kama hili na yule mhusika akaitwa tapeli lakini mwisho wa siku akarudisha zile pesa.
Sipo hapa kutetea ujinga alioufanya Mkuu Raimundo lakini na nawiwa kusema pole sana kwa mkasa uliokukuta.
Mtu yeyote mstaarabu hakutakiwa kufanya vile tena kwa watu wake wa karibu kama wewe.
NB 2: Tatizo kubwa ambalo mimi ninalo kuhusu hii hukumu ni
MOB VIGILANTISM watu waliacha kuzungumzia mada ya utapeli wakaamua kuanza kuchimba kuhusu maisha ya mtu binafsi. Hasahasa suala lake la mahusiano (
This is very wrong) na hawa moderators wakaamua kuliangalia tu hili suala hadi pale liliposababisha ugomvi na kuchafua baadhi ya members kama RUBI ambao walikuwa hawahusiki kabisa na huu Utapeli wa Raimundo (
Not fair at all)
Kibaya zaidi wakaufunga ule uzi kunafiki baada ya kuona mambo yamekuwa siyo mambo na hisia kutawala kuliko uhalisia wa mambo.
NB 3: Wewe ulikuwa na haki zote za kulaumu kuhusu pesa yako pamoja na wengine wote wenye mkasa kama wako. Lakini hao wanaosema kwamba walitapeliwa mapenzi hayo yalikuwa yanaingiaje hapa ?? Tena walioongoza kushabikia ule ujinga ni watoto wa kiume tena ukute wana hata familia. (
That was very disgusting)
Pole sana mkuu kwa mkasa uliokukuta: Naomba tufunge huu mjadala!