MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
kama mnayo katiba nzuri kiasi hicho, kwanini sasa kenya ni miongoni mwa failed states? 1. Rushwa imeshamiri 2. Njaa ndiyo nyumbani kwake 3. Ukame wa mara kwa mara unaosababishwa na ukataji hovyo wa misitu 3. kukosekana kwa umoja wa kitaifa unaosababishwa na ukabila na mgawanyo usiyo sawa wa rasilimali mfano ardhi ambayo ni rasilimali muhimu sana kwa maendeleo inashikiliwa na walio wachache kwa manufaa yao binafsi 4. Amani na utulivu hafifu, watu kutekwa ni jambo la kawaida 5. Kuwa na jeshi dhaifu lisilo na maadili hata raia anaweza kumtisha 6.
Kwa taarifa yako Kenya ndio inaongoza kiuchumi, kielimu ukanda wote huu, haya yote yalichangiwa sana na katiba mpya, awali tuliishi maisha ya hovyo sana chini ya uongozi wa chama kimoja hadi ile siku kilinuka mpaka ikabidi tufumue katiba na kuandika upya ndio Kenya ilipaa kwenye nyanja zote, pengo la kiuchumi baina ya Kenya na Tanzania liliongezeka kwa mwendo kasi mpaka leo tunakaribia kuwazidi mara mbili licha ya nyie kuwa na raslimali zote na kila kitu ikiwemo ardhi kubwa ambayo haina ukame wowote, tofauti na Kenya zaidi ya nusu ya nchi yetu ni kame tupu.
Nyie hapo mpaka mtakapozinduka na kuthubutu kubadilisha chama mtaendelea kuchelewa sana maana humo kwenye hicho chama ni system iliyojichimbia tangia uhuru na hujilinda sana na kulindana humo humo bila kujali maslahi ya wananchi.....