moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 142,674
- 743,909
Nani atalinda Ikolojia mbugani?Ndio maana ya EIA ,kabla ya kufanya hivyo lazima hiyo kitunifanyike kuonesha namna ikolojia italindwa.
Watanzania hawa wa mijini wanajenga kwenye service road, wanajenga mabondeni na hakuna anayewasimamia, utaewasimamia wachimba madini porini wasikate miti, wasiue swala nk?
Wao wameweza maana wametoa elimu ya kutosha kwa watu wao kulinda na kuheshimu raslimali zao hata kabla hawajafikiria kuchimba madini.Kwani ni Tanzania pekee ndio wa kwanza kuchimba Madini hitadhini? Huko Amazon inafanyika hivyo na kwingine.
Ndiyo maana leo wanavijiji wa Brazil wakivamiwa na Anakonda wanamkamata na kumrudisha porini.
Watanzania wakivamiwa na nyumbu watamuua kumfanya kitoweo.
Mkuu kwenye kusifu tutasifia, lakini kwenye makosa pia tutakosoa.Sijaona hoja ya msingi yaani Kila kitu ni kupinga tuu.
Tuliwaunga mkono kuhamisha wamasai kwa nia ya kulinda mapori yetu, lakini hili la kufukua fukua hifadhini tutalipinga.
Usilinganishe mradi mkubwa wa kimkakati kama ule na project za kuchimba Ruby, Tourmaline, Green Garnet au Dhahabu.Bwawa la Nyerere limefanyika hitadhini na hakuna kilichoharibika.
Hiyo ni vurugu hifadhini.
Haiwezekani.