Rais akiruhusu 'plea bargaining' kufanyiwa uchunguzi katika Serikali ya Awamu ya Tano atakuwa amekosea sana

Haina haja ya kufufua makaburi mkuu hayo raisi angeachana nayo
Duh! Duniani kuna watu...yaani hutaki kabisa hata uchunguzi ufanyike ili mashaka waliyo nayo wananchi yazikwe kama alivyozikwa muasisi wake. Pole sana kama matokeo ya ukweli yatakutesa na kukunyima usingizi.

Kama kweli wewe RWANDES una nia njema na hili taifa, huwezi kuja na upuuzi kama huu ukanyamaziwa na ndio maana hadi sasa post no. 24 hakuna hata mtu mmoja amethubutu kukuunga mkono...je huoni aibu?

Naanza kuwa na wasi wasi nawe RWANDES, bila shaka yoyote lazima utakuwa ama ni Biswalo mwenyewe au mojawapo katika walionufaika na uovu huo na kinachokusukuma hapa ni woga tu, uoga wa kuumbuliwa!

Ukweli hauwezi kufichika hata ukifanya jitihada gani, ukweli unaweza kuzikwa kwa muda lakini kamwe haukubali kufa...Truth lives for ever and only truth can set you free!
 
Kwanini tusianzie kuchunguza RICHMOND, EPA, ESCROW, DOWANS na mikataba ya gesi na madini?
 
biswalo siyo raisi kuguswa na hata cheo cha Dpp siyo rahisi kuguswa utaniambia zitabaki porojo za mitandaoni za kuchafuana

Ni kweli hawezi kuguswa, sio kwa kuwa ni msafi au uchafu alioufanya haufahamiki, lakini wanaopaswa kumchukulia hatua wote ni wafaidika wa uchafu aliokuwa anaagizwa na yule kiongozi muovu. Lakini ufahamu huku kulindana ni kwa muda tu, na jinai haiozi. Iko siku utawala wa haki utaingia madarakani na kila kitu kitarudishwa mezani.
 
Jengo la Wasafi HQ kodi anapokea ndugu wa karibu wa Biswalo baada ya mmiliki wa awali kuingia mkataba wa plea bargain, na jengo kutaifishwa.
 
Mwandiko wako unadokeza kwamba wewe ni mtu duni sana.
 
Mbona hueleweki unatishia serikali au unamtisha rais? We kweli nyau, umetumwa na Biswalo? Km kuna uhalifu na uonevu ulifanyika kwanini usichunguzwe.
 
Acha aruhusu Watu wamedhurumiwa Mali na Fedha zao Acha kutetea Dhuruma
 
Huyu wameshamuona dhaifu. Wamejua ukitaka umuwin we mseme Magufuli kwa ubaya.

Kabendera katumwa. Watakuja wengine wengi. Kuongoza nchi za kiafrica sio jambo rahisi kama mama anavyodhania ila muda utamuambia. Ama utengeneze maadui wapya ama utengeneze marafiki wapya.

Kwa sasa kila mtu ataibuka na lake, yaani kwa serikali dhaifu hata mvunja sheria huwa anajiona ana haki.
 
Yule ibilisi aliivuruga sana nchi ndiyo maana yuko motoni anateseka
 
Tulia dawa iwaingie vizuri, uchunguzi unafanyika kuangalia kama mliyofanya yaliakua na kwa mujibu wa sheria au la hasha.
 
Wewe ndio mbumbumbu kwelikweli! Magufuli hana legacy yoyote ya kuenziwa hata robo! Labda kama unataka kutuambia utekaji, mauaji, kubambika watu kesi, dhuluma na ubadhirifu navyo ni vigezo vya kumuenzi mtu huko kwenyu SUKUMAGANG!
 
Tulia dawa iwaingie vizuri, uchunguzi unafanyika kuangalia kama mliyofanya yaliakua na kwa mujibu wa sheria au la hasha.
DOWANS, EPA, ESCROW, RICHMOND na mikataba ya madini na gesi yalifanywa kwa mujibu wa sheria ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…