Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Kwani posho ni nin mkuu? Me nazani chadema walijua kabisa kujiisolet watakosa posho na wamekubaliana na hilo...nachojua unalipwa posho baada ya kusaini mahudhilio pindi uingiapo bungeni sio otherwise....Jiwe anatafuta kiki tu za.kishamba kwenye hilii.
Hapa inaonyesha jinsi gani ana uwezo mdogo wa kuchanganua mambo.
 
Spika Bosi wake ni Mkuu wa CCM, ambaye ni Raisi wa JMTZ, na fedha yote ya Serikali ya JMTZ msimamizi wake ni Raisi wa JMTZ, Bunge linapewa fedha za walipa kodi wa JMTZ na msimamizi wa Kodi zetu ni Raisi wa JMTZ, ...
Msimamizi wa kodi na mapato ya nchi ni bunge

Mkaguzi na mdhibiti ni CAG

Mkusanyaji na mtunzaji ni serikali

Serikali pia ni mtekelezaji wa bajeti
 
Msimamizi wa kodi na mapato ya nchi ni bunge

Mkaguzi na mdhibiti ni CAG

Mkusanyaji na mtunzaji ni serikali

Serikali pia ni mtekelezaji wa bajeti

Bunge linaongozwa na CCM, Mkuu wa CCM ni Raisi wa JMTZ!
 
Ungejiuliza pia haya maswali

Je wabunge wanalipwa na nani mishahara na hizo posho?

Pia bunge linakusanya kodi?

Je maswali namba moja na mbili yakiunganishwa kwa pamoja unahisi kwa akili ya kawaida boss wao ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app

Swali la 1
Wanalipwa kwa kodi za watz

Swali 2.
Kwa mgawano wa madaraka siyo kazi ya bunge kukusanya kodi.

Hapo mwisho
Hutakiwi kuhisi kwa akili ya kawaida bali kuelewa kwa akili ya kawaida kwamba kila mhimili una boss wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli amejiabisha mno leo, ameuonesha Ulimwengu namna ambavyo Bunge letu lilivyo dhaifu.
Bunge ni dhaifu kweli maana souce ya mapato ya mishahara na posho inamtegemea Magufuli akusanye kodi
 
Usiwe negative kwenye kila kitu, kati ya mengi aliyoongea umeona hilo ndo jema, usiwe negative kwa kila kitu, kwa hotuba yake ile amejikita kutoa faraja na matumaini kwa Watanzania, na kisaikolojia ina maana kubwa sana.

Ukichukulia kila kitu kwa jicho la Negative hutaendeleza Taifa lako na wala familia yako. Badilika

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hivi ndugu unaimbia 'praise quoir' ipi vile? ya Chamwino, Chato au zote?
Kama huko kutoa faraja na matumaini hewa kwa Taifa, wewe waona ndio kuwa 'positive', ndugu yangu nina wasiwasi kama waielewa hata mantiki yenyewe.
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Hivi kuna watu walitarajia uchaguzi huru na wa haki oktoba? Kwa dalili zipi labda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio kbs mjuzi wa kariba yetu. Ila kwa uchache wa ninayofahamu bunge ni mhimili unaojisimamia kupitia Spika anayechaguliwa na Wabunge. Paskali Mayala, wewe ni Mwandishi na sio Mhandisi pia wewe ni Mwanasheria nguli. Je tamko la Rais la kusema ameagiza kutolipwa posho kwa Wabunge ambao watagomea kuingia bungeni kwa kinachoitwa kujitenga na maambukizi ya Corona, hii ina leta picha gani kiutendaji kati ya Bunge/ Spika na ofisi ya Rais. Naomba ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mishahara ya wabunge inatolewa na serikali
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
tuna mhimili mmoja tuu tanzania
 
Back
Top Bottom