Rais anatumia kodi zetu vibaya, Royal Tour yake haina faida ni Ufujaji wa pesa za Maskini

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.

Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.

Huu ni wizi wa mchana kweupe
 
Hata tozo mlibeza...baada ya kusikia fedha zimepelekwa kujenga vituo vya afya,mkaombwa muandikwe kwenye vibao.

Mwacheni Mama Samia afanye kazi zake.
 
Sasa si bora huyo kuliko yule alikuwa anaelekeza miradi yote chato
 
Mbona hujaonyesha ushahidi wa kutokuwa na faida kwa Royal tour badala yake unabwabwaja kama uji unatokota?
 
Kupata watalii wa nje si lelemama , kuna ushindani mkubwa sana, lazima Tanzania ijitangaze- iwekee vivutio vyake hadharani, na hasa kama Rais anashiriki - lazima habari zitasambaa kwa haraka zaidi.
 
Ndiyo uwezo wake umeishia hapo
 
Rais ni taasisi bwashee!
 
Kupata watalii wa nje si lelemama , kuna ushindani mkubwa sana, lazima Tanzania ijitangaze- iwekee vivutio vyake hadharani, na hasa kama Rais anashiriki - lazima habari zitasambaa kwa haraka zaidi.
Hakuna lolote, tungemuweka Messi au Ronald kwa wiki moja tu watalii wangejaa mpaka kwenye nyumba za tembe Singida tena kwa gharama ndogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…