Mkuu Charles2016, kwanza hongera kwa utambuzi wa juhudi za ujenzi wa miundombinu wa awamu ya 5, pili ni vyema unapotaka kumuelimisha mtu si vyema ukaanza na kumvujia heshima yake. Aidha napenda nikujulishe kuwa SGR imejengwa ili kuboresha miundombinu ya reli, ndio maana njia yake ni ile ile; bwawa la Rufiji linajengwa ili kuongeza umeme wa kutosha na limejengwa sehemu ileile iliyoelekezwa tangia miaka ya 70; Daraja la Ubungo limejengwa sehemu ileile ambayo ilikuwa na kero ya foleni za magari; nk. Sasa hivi vya International Airport kulikuwa na msongamano wa abiria na ndege? International Football Stadium - Tunataka kuchezesha KOMBE LA DUNIA siku za hivi karibuni? ama kuna Klabu ya ligi ya daraja la pili? nk.. Kwa mantiki hiyo, hayo sio matumizi mazuri ya fedha za Serikali, kwa maana ya fedha zitokanazo na KODI YA WATANZANIA.