Rais alipaswa afikirie mambo makubwa ya msingi na kuachana na uigizaji anaoufanya kwa kutumia pesa zetu vibaya. Toka ameteuliwa kuwa Rais anazunguka tu.
Hatulii kufanya kazi. Nchi hii watu wanaiba ye hana hata habari ana talii tu. Haya mambo ni ufujaji wa pesa za umma. Badala yake ndo mnapandisha bei ya bidhaa na pia kodi mkiongeza na tozo.
Huu ni wizi wa mchana kweupe
Mkuu changamoto tuliyo nayo Ni kuwa tunaakili Kama imeegemeshewa kwenye kipago Cha mti, kwamba ikitikiswa tu tunadondoka,
Jaribu kuwaza watu m60, walio na maliasili zote, na ardhi kubwa Sana, Lkn mpka 2021 tunawaza kutangaza utalii?? Kwel tupo seriously?? Yaan toka 1961 mpka leo, awam zote hakuna aliejua kuwa utalii unakipato??
Anyway, hebu tuchulie tu bandali pekee yake, au tuseme mbuga za wanyama tu, tungekuwa na wat ambao si wanaojari matumbo yao, sa iv Wala tusingewaza hlo, yaan tusivyo na aibu tutakusanya tsh 10-9000 kwa watu ambao wanakipato kidg ila tunaacha pesa ambazo zipo tu, jaman hyo Ni akili kwel??
Leo kunamtu anasimama anasema anatangaza utalii, unamtizamaaa unajiuliza hiv tupo tz au nchi nyingne??
Bahati 1 tu ambayo viongoz wote wanayo Ni kuwa wanaongoza nchi ambayo haijazoea vulugu, yaan hata wakiamua kesho waseme tunakusanya 10000 kila mlango kila mwezi, watakusanya maana hakuna ambae anaweza kuthubutu kukataa.
Tunabunge butu, halina hata makali, pakunolea hakuna, mwisho wa siku nalo linaanza kulana lenyewe kwa lenyewe, hv kwel tumekosa mtu wakusema kuwa STOP...????????
Sasa mziki mnene Tena unakuja inakwenda kuzinduliwa usa, duh, yaan tumepigwa hapa na bado tunanyooshwa kule, Kisha tuna ambiwa mguu pandeee si nikuitika tu mguu sawa, nyuma geuka woteee, mbeleee tembeaaaa bila kujari kunashimoooo..
Tunahitaji Maombi Kama taifa, tukiendelea hvi itakuwa sawa na kutembea hatua 10 unarudi nyuma hatua 15 halafu unajipongeza..
Waswahili wanasema ukiona mziki unapigwa kwa jilan, unaweza kwenda kucheza au kusikilza ukiwa kwako, ukiwa yote huyawezi, nyamaza tu hata Kama unakereka.... Ili usiharibu sherehe ya watu...